Omotola Jalade katika pozi kabla hajapanda stejini kuimba maana mbali na kuact pia ni muimbaji mzuri tu,Albam yake inayowika inaitwa GBA.
Star Times
Mercy Beauty Parlour
Jan 16, 2010
Jan 15, 2010
Mengi yalisemwa, lakini nilifika...... ahh hah hah hah!
Jan 14, 2010
Nadia Buari a.k.a "BEYONCE"

Nadia Buari a.k.a Beyonce Mbali na kuigiza pia ni Mchumba wa mwanasoka wa Chelsea Michael Essien
Hapa akiwa na Essien

...Hapa akiwa na Van Vicker
Jan 8, 2010
Happy Birthday "THE GREAT"
HAPPY BIRTHDAY KAKAAAA, The great leo ni siku yangu ya kuzaliwa yaani wadhungu wanathema "Hepi bethidei"
Namshukuru Mungu kwa kunipa uhai mpaka kufikia siku hii ya leo, napenda kuwashukuru watu woote waliochangia katika maendeleo yangu kwa namna moja au nyingine pamoja na washika dau wangu woooote mliopo popote pale Duniani. Mungu awabariki sana.
Jan 6, 2010
Mercy Johnson & Femi Ogedegbe

Mercy & Femi into one of the events in Nigeria (I've been working with them) and Mercy Johnson is an Actress who inspired me in acting from Nigeria.

Jan 5, 2010
Ujio wa Ivory Coast nchini Tanzania...

Jana kulikua na kipute cha mpira kati ya Timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) na Ivory Coast (The Elephant) kilichofanyika katika uwanja wa Taifa Mkuu. Timu ya Ivory Coast imeomba kuweka kambi katika nchi yetu kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Kombe la mataifa ya Africa yakayofanyika Nchini Angola kuanzia tarehe 11 mwezi huu. hii ni mechi ya kwanza ya kirafiki ambapo mechi ya pili watacheza na Rwanda katika uwanja huu huu siku ya Al'hamis kabla ya kwenda mashindanoni.
Watu wengi walijua kwamba taifa stars tungepigwa 4 or 5 O'clock kutokana na hawa wajamaa kuwa na wachezaji walioshiba na maprofeshno katika kandanda. Lakini mambo yalikuwa siyo kama watu walivyodhani, drogba alitumia uwezo binafsi hadi kupata gori la kuongoza lakini huo mpira waliokuwa wanaupiga hawa watoto wa KIKWETE jamani tuache masihala, MPIRA TUNAUJUA. Sio kama ilivyokuwa miaka ya nyumba. Hasahasa kipindi cha pili wajamaa walianza kwa kasi kumbe si tulikuwa tunawasoma, si tukawachenjia kidogo kocha wao awatoe wachezaji wote awaingize tena wakina Drogba. (alituchezeshea vikosi viwili, kimoja kipindi cha kwanza na cha pili kikosi kingine jumla wachezaji 22)
kwa matokeo yangu ya harakaharaka sisi tungekuwa na magori 2 wao moja. Ngassa alikosa Gori la wazi yeye na kipa, na lingine Tegete alipiga mkwaju uliogonga mwamba na kurudi uwanjani....mpira Tumecheza sio mchezo.
Drogba alichukua maujiko ile kishenzi...

Hapa tuwaona wachezaji wa Ivory Coast wakiingia kwenye basi kwa ajili ya kuondoka muda mfupi baada ya kutoka katika mahojiano na waandishi wa habari katika chumba cha Habari Uwanjani Taifa. watu waligoma kuondoka mpaka wamuone Drogba akiondoka. alipotoka tu walipiga watu kelele Drogba!... Drogba!!... Drogba!! ama kweli ulikuwa ujio wa aina yake....
Taifa stars na The elephant katika hekaheka..

Wachezaji wakiendelea kukipiga katika uwanja wa Kimataifa wa Mpira wa Mguu wa taifa Tanzania.
Tuache masihala huyu jamaa ana nguvu...

Didier Drogra, mwenye jezi namba 11 akiwa makini kusubiria mpira kutoka wingi ya kulia. hivi hebu jaribu kuangalia we mwenyewe hapa mdau, huyu beki wetu mwenye jezi namba 5 kama sikosei (kushoto) anamfikia Drogba kwenye bega!! sasa anza kulinganisha ukubwa wa mwili... we acha
...kwa harakaharaka nilipoitembelea timu ya Cote D'voire walipofikia kwenye Hotel aliyokaa Bush (Kempinski/Kilimanjaro Hotel) nilikuta jamaa anapiga Plate 4 za Ubwabwa na Juice jagi moja yeye peke yake,
wachezaji wetu plate 2 tu mtu chali. lakini mi naamini tumejifunza kitu fulani kutoka kwa hawa jamaa.
ila...... mpira tumewaonesha! achilia mbali na kagoli alikotufunga Drogba.
Sumry walikula Shavu...
Aisee, hawa wajamaa (Sumry) wana kausafiri kweli Classic, hii ndo basi iliyowabeba wachezaji wa Ivory Coast kwenda na kurudi uwanjani kwa ajili ya mechi ya kirafiki kati yao na Taifa Stars (Tanzania)
Mmemuona KALOU?

Solomon Kalou akiwa na mwenzake nyuma ya basi wakioneshana kitu kwenye simu, muda kidogo kabla ya kusepa.
Jan 4, 2010
...hii ni Hummer jamani!

...still tukiendelea na scene mbalimbali, ndani ya Filamu ya Lovely Gamble.
Dec 31, 2009
Buriani mzee KAWAWA (1926-2009)

Mzee Kawawa tutakukumbuka kwa mengi, kwa sisi wacheza filamu tutakukumbuka kama muasisi wa filamu wa enzi zile za zamani. Kati ya filamu alizocheza ni kama "MUHOGO MCHUNGU", "MELI INAKWENDA, FIMBO YA MNYONGE n.k.
Kwangu mimi kama Steven Kanumba nitakukumbuka kwa heshima uliyowahi kunipatia mwaka juzi 2007 kwa kunialika kwako kwa kitafrija kidogo cha kunipongeza mimi kwa kazi zangu za filamu, hiyo ilikua ni heshima kubwa sana kwangu katika maisha yangu ya Sanaa. Mungu ailaze roho yako mahala pema peponi, Amina.
Dec 30, 2009
Dec 28, 2009
Hongereni YANGA

Hatimaye yale mashindano yanayoandaliwa na Bia ya Tusker (Tusker Cup) yamemalizika jana kwa wanajangwani Dar Young African (YANGA) kuchukua ubingwa huo kwa mara ya pili kwa kumkandamiza Sofapaka ya Kenya mabao 2 - 1. Yanga ambayo ilionekana kutawala zaidi mpira katika vipindi vyote viwili ilipata pigo la gori la kwanza kwa mpira wa adhabu uliopigwa moja kwa moja na kujaa wavuni katika kipindi cha kwanza. Yanga iliendelea kulisakama lango la sofapaka bila ya Mafanikio hadi wanakwenda kupumzika ikiwa nyuma kwa bao moja. kipindi cha pili yanga ilionesha uhai zaidi kwa kuendeleza mashambulizi yake lakini hayakuzaa matunda mpaka Papic (Kocha wa Yanga) alipoamua kumtoa Nsajigwa na Kumuingiza Fred Mbuna, na Jerryson Tegete kumpisha Boniface Ambani ambao kwa kushirikiana na Mrisho ngassa, Athumani Idd (Chuji) na wengineo katika safu ya Ushambuliaji wakaandika bao la kusawazisha mnamo dakika ya 86 kupitia kwa boniface Ambani. Muda sio mrefu mnamo dakika ya 90 yanga iliandika bao la Kuongoza kupitia kwa Mrisho Ngassa.
kutokana na hayo tunaipongeza Yanga kwa kuonesha mchezo mzuri na hata Kuchukua Ubingwa huo.
Dec 27, 2009
TUNAOMBA MAONI YAKO
Naomba utusaidie kukuletea taarifa haraka bila ya usumbufu wa kusubiri taarifa kwa muda mrefu. Je! kuna uchelewaji wa Page hii ku-load? au inashindwa kabisa ku-Load? au Afadhali? au Safi sana? Akhsante sana!
Dec 26, 2009
Kwaya ya Vijana AIC Makongoro-Mwanza
Hii ni kwaya ya Vijana AIC Makongoro Mwanza. Walikuja nao kujumuika na wenzao wa Dar-es-salaam katika kusherehekea sikukuu ya Christmass
Labels:
christmass
Mambo ya Christmass jamani Kanisani
unaweza ukaanza kujiuliza hapa ni wapi? Hapa ni kanisani AIC Chang'ombe siku ya Christmass, watu walijitokeza wengi sana katika ibada siku hiyo mpaka ikaamuliwa Ibada ifanyike nje kutokana na kwamba ndani kulikuwa hapatoshi
Labels:
christmass
The Great kanisani AIC Chang'ombe
We unadhani mi sikuwepo? Hapa nikiwa katika ibada ya Christmas asubuhi na rafiki yangu wa siku nyingi (Bayuka). Tuliwahi kuimba wote katika kwaya enzi hizo........ yeye alikuwa akipiga kinanda, mimi nikipiga Gitaa la Bass.
Labels:
christmass
Wakumsifu Mungu nao hawakua nyuma
Hii ni kwaya ya Neema Gospeli....., nilikua nikiimba katika kwaya hii hapo Chang'ombe enzi hizo. Hapa wakiimba katika ibada ya X-mass asubuhi.
Dec 25, 2009
The great na Frank
Steven Kanumba (Kushoto) Akiwa na Produza wa Filamu ya Lovely Gamble Frank Yembe a.k.a mzee wa nyuki
Subscribe to:
Posts (Atom)

















Mojawapo ya scene katika lovely Gamble naelekea kupanda Treni (underground railway)














