Star Times
Mercy Beauty Parlour
Mar 24, 2010
Mar 22, 2010
SWAHIBA WANGU THE GREATEST ATEMBELEA LOCATION KWANGU LEO KUONA KAZI INAVYOKWENDA.
Mkurugenzi wa GRM PRODUCTION Ndg GABRIEL MAKUBA nae alikuepo kusaidia mambo kadha wa kadha katika kuhakikisha movie yangu inakuwa na ubora wa kisasa.kama unavyoona hapo picha yangu ukutani ni moja ya kazi alizonisaidia upesi katika scene za ofisini kwangu na kuhakikisha kunakuwa na picha ukutani ili kujenga uhalisia.
Mara baada ya swahiba kufika nilimkabithi kiti cha u director ili anidirectie scene mojawapo hapo nae alikubali kufanya hivyo,hii ni kampeni tuliyoianzisha ya kutembeleana location ili kutiana moyo na kuifanya tasnia ya filamu kusonga mbele kwa ubora na kwa umoja hasahasa tukifahamu kuwa"There is nothing can't be done if we raise our voice as one"
Swahiba akichukua picha za matukio kwa ajili ya blog yake ya www.raythegreatest.blogspot.com
Swahiba akiwa makini katika kudirect scene niliyompa ambayo nilikuwa nikicheza mimi.
Lusubiro Mwanguku akiwa makini na camera
Swahiba alidirect kwa moyo wote na kwa furaha hakujali kama movie ni yangu bali alifanya kama ni yake au ya RJ COMPANY nilijisikia furaha sana moyoni nikakumbuka enzi za filamu zetu za mwanzo za Game 1st quality Tz Ltd kama Johari 1&2,Sikitiko langu,na Dangerous desire.
Baada ya kumaliza scene hiyo tulipata picha ya pamoja
Mara nyingi tukikutana huwa ni lazima vicheko vitawale na utani wa hapa na pale maana tumetoka mbali jamani ukweli tunaujua wenyewe.
MAYA production manager wangu, make up artist wangu na continuity manager wangu huwa makini sana katika kazi yake chini ya kampuni yake ya vipodozi ya MAYA ENTERTAINMENT kama mnavyomuona hapo akiandika kila shot inayopigwa katika scene na miendelezo yake hii humsaidia editor wakati wa kuhariri movie kazi kuwa nyepesi maana hutambua ni shot zipi zitumike na zipi ziliharibika kwa kutumia hilo daftali analoandika Maya.
Kaka yangu kiumri na kaka yangu kiroho(JB) nae alikuepo pamoja na swahiba kuona jinsi The great ninavyosukuma gurudumu la filamu Africa na kuendeleza kampeni yetu ya kutembeleana location,jamani ukiujua ugumu wa kazi hii lazima utamtia moyo mwenzako pale alipokata tamaa,utamkosoa kwa njia ya amani ili kujenga na si kuponda au kutukana kazi yake na kutukuza za nje,utamshika mkono na kumwinua pale alipojikwaa ili asonge mbele na si kumkanyaga tena ili adidimie,utampa pongezi zinazomstahili pale alipofanya vizuri ili kumpa tumaini la kesho lakini haya yote hayawezekani kama hatuna upendo wa dhati kati yetu.Mungu atusaidie sana ili jamii yetu tupendane kwa dhati na kuwa wazalendo katika kazi za wasanii wetu wa Tanzania maana ni "Ni heri uzee wa simba kuliko ujana wa fisi"WADAU NAMBA MOJA WA RJ COMPANY NA KANUMBA THE GREAT FILMS WATEMBELEA LOCATION KWANGU.
Mdau namba moja INNO BACHARD,(kushoto)Pink,Slyvia na Ally Yakuti waliponitembelea location kwangu kuona jinsi kazi inavyokwenda,asanteni sana jamani kwa kunitia moyo wadau.Mar 21, 2010
KANUMBA THE GREAT FILM bado tupo mzigoni tukipika kitu kipya jina bado kapuni ila shughuli yake ni pevu.
Aunty Ezeckiel na Kijana wangu Suma wakionesha uwezo wao katika scene ya mapenzi kitandani.kama ilivyo kawaida yangu mbali na kuweka mastaa katika movie lakini pia huwa naweka na vipaji vipya vinavyochipukia ili nao wapate nafasi ya kuonesha uwezo wao kama unavyoona hapo juu.
Baada ya kumaliza scene Gwantwa aliamua kupozi kwa picha kidogo huku kijana Suma akichekelea kwa kumaliza scene yake vizuri.
Aunty Gwantwa na Patcho Mwamba wakipokea maelekezo toka kwa director kabla ya kuanza kurekodi
Kazi imeshaanza Aunty na Patcho.
Katika movie hii Patcho kaonesha kiwango cha juu sana huwezi amini kama ni mkongoman tena mwanamziki wa bendi maarufu jijini ya FM ACADEMIA.
The great kazini mbele ya kamera.
Huwa sina masihara kabisa ninapokuwa mbele ya kamera ninashukuru sana Mungu maana kila filamu huwa naonesha maajabu na hii itakua funga kazi
Patcho na Aunty walijisahau wakalala kweli nilipowagusa na fimbo yangu walishtuka kwa kelele sana ikabaki vicheko kama unavyoona hapa hivyo ikabidi turudie.
Hapa wamelala kabisa wamejisahau hii utokea mara kadhaa wakati setting za taa na kamera zinapochukua mda mrefu wakati wasanii wako tayari hupitiwa na usingizi.
Hapa nikikagua setting ya kila kitu wakati wasanii wangu wanakoroma.
Picha ya juu na chini nikiwapa maelekezo juu ya nini wafanye katika scene hiyo nao husikiliza kwa makini sana.

Ni picha tu jamani
Kutokana na makamuzi anayoyafanya Aunty katika movie hii kwa sasa pindi anapomaliza kila scene hata crew yangu nayo hutaka kupiga nae picha maana humuona ni mpya tena.
Lusubiro akipiga shot ya kiatu namkumbuka director wangu wa kwanza katika tamthilia anaitwa Chrissant Mhenga hizi alikua akiziita shot za upendeleo kipindi hicho tukiwa kaole sanaa group.
Nikishauriana jambo na cameraman wangu Lusubiro.
Wakati fulani huwa inabidi nitizame katika screen ya camera ili nione kama monitor yangu inanipa picha sawa na ya kwenye camera maana kama monitor setting yake si nzuri basi huweza kukudanganya na kukupa picha usizozitaka lakini pia kuwa na uhakika na angle ya kamera kama hujacross angle.
Nikitoa maelekezo kwa crew jinsi scene tunayoelekea kushoot ilivyo ili tujue kamera na taa vikae sehemu gani.
Kazi ikiendelea
Jicho langu la kushoto limekua jekundu baada ya lenzi ya macho niliyokua nikitumia kudondoka chini na aliyeniweka akuiosha vizuri katika maji yake hivyo ikaingia na vumbi na kusababisha jicho langu kuniwasha sana hivyo nikaamua kushoot bila lenzi lakini kazi inakwenda vizuri...ni mambo ya kawaida mkiwa shooting.
Gwantwa akaona bora asiache mbachao kwa msala upitao muone alivyofanya macho yake na ulimi.
Kutokana na wingi wa taa ukijumulisha na hali ya hewa ya DAR basi joto huwa kali sana hivyo mtu wa make up huwa busy sana kuakikisha kila unapotoka jasho kuja kuliondoa maana huwa hatuwezi kuwasha air condition au feni maana hutoa kelele ambazo hualibu audio ya movie,Maya akinisaidia yeye ndie make up artist wangu na Production manager.Mar 20, 2010
Mar 19, 2010
KATIKA SHOOTING YA LEO AUNTY EZEKIEL KATUALIKA MLO WA USIKU NYUMBANI KWAKE.
Crew yangu yote tulijumuika nyumbani kwa Aunty kupata makulaji ya nguvu,asante sana Aunty.
Kutoka kulia ni mmoja wa waandishi wazuri sana wa script za movie anaitwa Ally Yakuti nae alivamia gafla sijui alijuaje,siku hizi amekuwa mgumu sana kupatikana wakati fulani simu huwa hapokei au huzima kabisa.
Subscribe to:
Posts (Atom)
















