Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Nov 14, 2010

OFF SIDE YAZIDI KUPAMBA MOTO

Wadau bado twazidi kuisuka movie yetu mpya mimi na swahiba wangu ya OFF SIDE ambayo kwa sasa tumezidi kuongeza mastaa wengine ili kuboresha na kuongeza radha tofauti katika movie hii.Hapa hatuna masihara kabisa ni moto wa gesi. Chopa mchopanga nae yumo

kazini

The great kazini

Hili ndilo dude ambalo The great pioneer natumia katika movie hii

Kazi ikiendelea

Kuna wakati ambao msanii husika hawezi kucheza kipande chake kwa ufanisi mfano kuendesha gari kwa kasi,kuogelea nk...hivyo inabidi kuvaa nguo za mhusika huyo na kujifanya yeye ili kuipa nguvu scene kama anavyoonekana The great hapo alipomsaidia msanii fulani scene fulani japo ktk editing sitoonekana mimi bali msanii husika.

Swahiba akiwa makini sana maana hataki nimfunike hivyo anakaba hadi penati.

Mtu na kaka yake wakielekea mjini kutanua

Kikazi zaidi

Jamani hapa ilikuwa BALAA kuna hisia na makamuzi ya aina yake

Wee unafikiri hapa ilikuwaje ahahahahah i wish muone

Simba na Chui......Hatari...moto wa gesi wauzimaje?

Nov 10, 2010

OFF SIDE BADO NI PATASHIKA NGUO KUCHANIKA,FULL KUFUNIKANA.

The greatest na The great pioneer

Tukishauriana jambo

The great nikijiandaa kupita ktk camera,

Irene Uwoya na The great makamuzini

I wish muone hii scene ni balaa

Hapa ndipo nilipomkubari zaidi Uwoya maana alionesha uwezo wake wa ziada kama msanii

Kazi ikiendelea

JB na Irene Uwoya

Naomba nisiseme kitu ila fikiria mwenyewe hapa JB,Uwoya,Ray,Kanumba,huo moto ukoje hapa?

Next level hii

Nov 8, 2010

PICHA ZAIDI KATIKA HARUSI YA THEA NA MIKE

JB na mke wake (Qeen)

Swahiba na Mwanamimi

The great nikimpongeza Bi harusi Thea

The great nikimpongeza bwana harusi Mike

Swahiba nae hakuwa nyuma kuwatakia kheri maharusi

Picha ya pamoja maharusi na wasanii

Ilifika wakati wa wasanii wa filamu kucheza mziki hapa JB akionesha staili yake ya Kadanse mpunda.

Ilifika zamu yetu maswahiba kila mmoja akisubiria tutafanya nini?

Kazi ikaanza si kitoto

Pastor Myamba na Johari kwa pamoja

The great,Dr.cheni na Ray katika mazungumzo ya safari

Nov 7, 2010

HARUSI YA THEA NA MIKE YAFANA SANA

Harusi ya wasanii wenzetu wa filamu Ndumbagwe Misayo(Thea) na Mike Sangu(Mike) iliyofungwa leo kanisani na kusheherekewa vizuri ukumbini na watu mbalimbali imefana sana,The great na blog hii twawatakia maisha ya amani na upendo daima. The great na Nteze

Bwana na bi harusi na wapambe wao wakisikiliza vizuri nasaha za wazazi

Baba wa Thea akitoa nasaha zake

Chiki ndiye aliyekuwa MC wa shughuli hiyo nae pia hivi karibuni anataraji kufunga ndoa

Wazazi na maharusi ktk picha ya pamoja

Monalisa na mdau toka America

The great,Emmanuel myamba na Coco

Wanameremeta

Wasanii mbalimbali maarufu walikuepo

Immaculate,Mwanamimi na Johari

Nov 6, 2010

POSTER LA OFF SIDE JINSI LILIVYO

Poster la OFF SIDE ndio hilo wadau,ni moto wa gesi huooo upo hapo mdau wetu Albert Felix Birashoboka wa Australia?Dada Sanura Dernmark,Abou Dernmark.Dada Sharifa kalala Washington Dc?na wadau wote popote pale mlipo tumefanyia kazi maoni yenu.

Nov 1, 2010

WADAU WENGI WATABIRI SAWIA....HII NI MIMI NA SWAHIBA

Hivi juzi niliandika GUESS WHAT?nikatoa na picha za mimi na swahiba tukiwa na Irene Uwoya nikiitaji wadau mtabiri,na wengi wamepatia ni kweli kwa mda wa karibia miaka 2 mimi na swahiba hatujakutana katika filamu yoyote mpaka hii ya sasa ambayo ni moto wa kuotea mbali saaaaaaaaana ni KANUMBA VS RAY.Wadau tumeingia ulingoni hasa hasa kutokana na maoni ya mashabiki wetu wengi ambao kila mara wamekuwa wakiomba tukutane kama zamani nasi tumeamua kuweka mkakati wa kila baada ya mwaka mmoja tutakuwa tunakutana na swahiba katika filamu moja tu kama hii ya sasa,filamu yetu ya mwisho ilikuwa ni OPRAH ambayo tulimshirikisha Irene uwoya mwaka 2008 na ya sasa ni hivyo hivyo.hapa ni kampuni mbili za production zinazoshirikiana yaani RJ COMPANY NA KANUMBA THE GREAT FILMS.Jina la filamu nitawatajia siku ingine wadau.. The great na swahiba tukiwa tayari kwa kushoot

Katika movie hii tunae pia JB ambae kaongeza utamu katika movie

The great na JB on set,Toka nianze kuact sijawai kukutana na kaka yangu JB movie hii ndio ya kwanza kukutana mimi na yeye.Ni msanii ninayemkubari sana.

Swahiba na JB kazini

Swahiba akipitia script kwa uyakinifu

The big two kazini....hapo ni makamuzi ya hatari

mmmmh?

Katikati ya scene

The great kazini

Ebu fikiria hii scene itakuwa vipi hapa The great pale swahiba pale JB...hatariiii