Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Jul 14, 2010

THE GREAT KATIKA KAZI ZA KIJAMII ZANZIBAR.

Jina la shule nimesahau kidogo ila hii ni moja ya shule tuliyoitembelea na kuongea na wanafunzi ambao walikuwa wanatusubiri kwa hamu ili kuongea na sisi lakini pia walikuwa na maswali yao ambayo tuliwajibu kwa ufasaha. wakitusikiliza

Tukiwa mbele yao wakihoji maswali na kuelezea furaha yao kuonana nasisi live

The great nikijibu maswali yao ambayo mengi yalikuwa yakihusu film yangu ya THIS IS IT...unce jj na Jenifa.

Picha ya pamoja na wanafunzi

Monalisa akisaini autograph..

The great pioneer nikisaini Autograph ya mwanafunzi huyu aliyeniomba nifanye hivyo

Jul 13, 2010

SHEREHE FUPI YA ZIFF YA KUWAKARIBISHA WADAU NA DIRECTORS MBALIMBALI WA FILM YAFANYIKA

Mkurugenzi wa ZIFF akifafanua jambo huku msaidizi wake(LINDA-kushoto)akimsikiliza kwa umakini.


Directors na wadau toka sehemu mbalimbali duniani wakisikiliza

Cloud,Bi Nadine Louise Feser(artistic director)Prof.Martin na The great kwa pamoja

Watu wakibadilishana mawazo



Vinywaji vilikuepo vya kutosha

INTERVIEW MBALIMBALI ZETU JUU YA ZIFF

Tumekuwa na interview mbalimbali katika radio na tv juu uwepo wetu wasanii wa filamu bongo hapa katika tamasha la ZIFF,Hapa tukiwa ZCTV ila upande wa radio yake. swahiba akihojiwa

The great na Gervas kasiga tukihojiwa redioni

Mahojiano yakiendelea

Baada ya mahojiano kuisha sasa ilikuwa ni zamu ya kuingiza baadhi ya matangazo ya vipindi mbalimbali vya radio hiyo

Swahiba nae akitimiza wajibu

UPENDO NA UKARIMU WA MASHABIKI WA ZANZIBAR

Tulipata mwaliko wa kupata chakula cha mchana mimi,ray,cloud na wadau wengine toka katika familia moja ambayo ni wapenzi sana wa movie zetu hakika chakula kilikuwa kitamu sana..The great natoa shukrani zangu za moyoni kwa familia hii.

Yaani dakika 10 nzima swahiba namsubiri amalize kupakua

Punguza upakuaji wako swahiba bado tupo wengi....

Picha ya pamoja sisi na baadhi ya wanafamilia waliotualika

Baada ya mlo kulikuwa na mahojiano mbalimbali ta TV kama unavyoona,swahiba akihojiwa baada ya yeye nilifata mimi

USHINDI WA SPAIN,RAY AMNYOOSHEA MIKONO JUU YULE PWEZA WA UJERUMANI

CLOUD AKISHANGILIA USHINDI WA SPAIN KATIKA KOMBE LA DUNIA WAKATI SWAHIBA HAAMINI ANACHOKIONA

SWAHIBA MWENYE MAJONZI BAADA YA TIMU YAKE (NETHERLAND)KUFUNGWA MOJA BILA

CLOUD AKIOMBA PESA ZAKE TOKA KWA SWAHIBA MAANA KABLA YA MECHI KUANZA WALIPINGA KWA KUWEKEANA DAU LA PESA.

THE GREAT NA DANNY MOJA WA STAFF WA ZIFF TUKIFURAIA USHINDI WA SPAIN,HII ILIKUWA JANA KATIKA UKUMBI WA NGOME KONGWE HAPA ZANZIBAR.

Jul 11, 2010

STEVE KANUMBA NA VICENT KIGOSI NDANI YA ZIFF ZANZIBAR

LEO SAA MBILI USIKU LIMEZINDULIWA RASMI TAMASHA LA FILAMU LA KIMATAIFA LA 13 LIJULIKANALO KAMA ZANZIBAR INTERNATINAL FILM FESTIVAL(ZIFF)AMBALO KWA MARA YA KWANZA MIMI NA SWAHIBA TUMEPEWA MWALIKO WA V.I.P KUHUDHURIA KATIKA TAMASHA HILI BAADA YA MCHANGO WETU KUONEKANA KATIKA FILAMU ZETU NCHINI NA AFRIKA KWA UJUMLA,HAKIKA NAWASHUKURU ZIFF KWA KUTUKUMBUKA NA KUTAMBUA MCHANGO WETU. LIKIZINDULIWA RASMI KTK UKUMBI WA NGOME KONGWE HAPA ZANZIBAR

WATU WAMEJITOKEZA KWA WINGI SANA

SWAHIBA NA THE GREAT KWA MARA YA KWANZA NDIO TUMEHUDHURIA TAMASHA HILI BAADA YA KUPATA MWALIKO MAALUM.

SHAMRASHAMRA ZA UFUNGUZI ZILIKUWA HIVI

THE GREAT NIKIWA NA ID YANGU YA ZIFF

KUMEKUWA NA BURUDANI MBALIMBALI TIZAMA MWENYEWE MAMBO YA KIHINDI

HAWA VIJANA WALISHAMBULIA JUKWAA VILIVYO KWA STAILI TOFAUTI ZA MIZIKI DUNIANI

MICHAEL JACKSON WA ZANZIBAR NAE ALIKUEPO

ULIFIKA MDA WA STEVE KANUMBA NA RAY KUONGEA MACHACHE MBELE YA WAGENI HAPO RAY NDIE ALIYEANZA KUZUNGUMZA,ALIWAPONGEZA ZIFF KWA KUWAKUMBUKA WASANII WA FILAMU WA BONGO AMBAO WALISHAKATA TAMAA NA TAMASHA HILI NA KUONA KAMA SI LAO NA KUWASIHI WATANZANIA WOTE KUPENDA KAZI ZA NYUMBANI.

THE GREAT NAMI ILIFIKA ZAMU YANGU..

ILIANZA KUONESHWA FILAMU YA ''I LOVE U''TOKA JURRY,IKIFATIWA NA FILAMU YA HISTORIA YA MAISHA YA MZIKI YA MWANAMZIKI YOUSSOU N'DOU

TULIPATA PICHA YA PAMOJA NA KIONGOZI MKUU WA ZIFF..

Jul 9, 2010

MWEZI HUU MDA WOWOTE NTAWALETEA YOUNG BILLIONAIRE...KAENI MKAO WA KULA KWA MASHABIKI WANGU WA KWELI.

KWANGU MIMI BURUDANI TOKA MOYONI,HUWA NAKONGA NYOYO VILIVYO KATIKA TASNIA HII.MWEZI HUU FILAMU HII ITAKUWA MADUKANI MSIACHE KUPATA NAKALA YAKO ORIGINAL NA SI FEKI,WACHA KUAZIMANA NUNUA YAKO BEI IKO SAWA KWA WOTE,IMETENGENEZWA CHINI YA KAMPUNI YANGU YA KANUMBA THE GREAT FILMS.. POSTER LAKE.

Jul 7, 2010

THE GREAT ATEMBELEA MNET-AFRICA(SOUTH AFRICA)

Nimefanya ziara kidogo ya kutembelea ofisi za mnet na africa magic ambao hurusha movie zetu kupitia DSTV..Hivyo nikaona niwape picha japo kidogo. The great na Elnest ndani ya ofisi za mnet

Hapa nikiwa na mmoja wa staff wa Africa magic channel

Hapa nikiwa na baadhi ya staff wa Africa magic plus ambao wengi wao kwa sasa ni wapya tofauti na wale waliozoeleka kama dada yetu Hamida Suleiman ambaye hayupo tena ktk ofisi hizi pamoja na Nashon.

The great na Lilian nje ya ofisi za MNET.Lilian kwa sasa ndiye mkuu wa kitengo cha movie upande wa Africa magic plus hivyo kwa wale producers mnaopeleka movie huku lijueni hili lakini pia ofisi za ununuzi wa movie umeamishiwa Nairobi Kenya hii ni kutokana dada yetu Hamida kuacha hapa.

Lilian akimsihi mpiga picha apige picha kubwa ili nembo ya MNET ionekane

Ofisi za mnet kwa nje zinavyoonekana nchini africa ya kusini-johannesburg

THE GREAT IN DURBAN

WATOTO WA KIZULU WAKICHEZA NGOMA YAO YA KIASILI KATIKATI YA MJI WA DURBAN


HAWA DADA WANARUSHA MIGUU KISAWASAWA

NIKIWA NA MASHABIKI WANGU AMBAO WALINIOMBA KUPIGA PICHA NAMIMI

HAWA WATOTO WALISHINDWA KUVUMILIA IKABIDI WAJE KUNIOMBA KUPIGA PICHA MASKINI KUMBE NI SHABIKI WANGU WAKUBWA NAMI NIKAWAKUBALIA



HUYU NI DADA WA KIZULU AMBAE ALIAMUA KUNILETEA ZAWADI KABISA KAMA PONGEZI YA KAZI ZANGU PIA AKANIPA NA BENDERA YA NCHI YAO AFRICA KUSINI KAMA KUMBUKUMBU.