Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Dec 12, 2010

PICHA ZAIDI KATIKA HARUSI YA CHIKI

Kama nilivyoahidi kuwapa picha zaidi za matukio katika harusi ya msanii mwenzetu Salum Mchoma(Chiki)nazo ndio hizi... Mzee wetu Kipara alikuepo

Ngoma ya asili toka kaole sanaa group ilisisimua sana watu



Sajuki na mkewe(Wastara)nao walitumbuiza kwa wimbo mzuri

Kwa furaha Nova alimbeba juu juu bwana harusi

Bi mwenda akilisakata rhumba na Nova

The great nikipata picha na maharusi

William Mtitu na Bi mwenda

Umoja wa wasanii wa filamu ulionekana

Raisi wetu wa shirikisho letu la wasanii wa filamu Simon Mwakifwamba akitangaza zawadi ya wasanii kwa maharusi ambayo ni kulala katika hoteli ya kifahari ya Sunrise beach katika honeymoon yao kuanzia leo.

wasanii na maharusi

Dude akitangaza zawadi ya mabati toka kwa wasanii.

Dec 11, 2010

HARUSI YA CHIKI YAFANA SANA.

Harusi ya msanii mwenzetu na kiongozi wa kaole sanaa group Salum Mchoma(Chiki)imefana leo katika ukumbi wa new msasani beach(makuti).Harusi hii imehudhuriwa na watu mbalimbali maarufu na wadau mbalimbali wa tasnia hii ya filamu.The great na Blog hii inamtakia maisha mema na mazuri Chiki na mkewe yenye furaha na amani. Mama Dotinata akiwasimamia maharusi kwenda ktk chakula

Bi harusi akikinga chakula



Furaha ya ndoa maana hata sahani unabebewa







The great nikimpa mkono wa pongezi Chiki kwa kupata jiko nikimtania kidogo kuwa nami ipo siku nitatimiza maandiko ya Gehova.

Mike na mkewe(Thea)waliofunga ndoa yao juzi tu nao wakisogea katika chakula

Dr.Cheni ndiye alikuwa MC wa shughuli hii,hapo akiwa na Steve baunsa(mwana poto)

Mzee wetu Kipara nae alikuepo

Burudani mbalimbali zilikuepo nami nawaahidi kuendelea kuwaletea picha mbalimbali za matukio ktk harusi hii ya kupendeza...endelea kutizama blog hii yako kila mara.....kwa sasa wacha nilale kwanza tuonane kesho.

Dec 8, 2010

FABAK FASHION YAJA NA MITINDO NITE..25 DEC..

BEHIND THE SCENE ZA VAN VICKER

Van Vicker(Ghana)akiwa na Tonto Dikeh(Nigeria)katika love scene.

Van on the set.

Kazi hii ina ugumu wake jamani kama unavyoona

On the set

DALADALA ZATAPAKAA POSTERS ZA UNCLE JJ MTAANI

Posters za filamu ya UNCLE JJ ambayo imetoka hivi karibuni zimetapakaa katika daladala mbalimbali jijini hii ikionesha kuwa kazi hii imewakuna vilivyo mashabiki wangu...







Dec 7, 2010

URBAN PULSE YATOA SHUKRANI ZAKE ZA DHATI KWA WOTE WALIOHUDHURIA ANNIVERSARY YAKE

Uongozi mzima wa Urban Pulse unatoa shukrani za dhati kwa wadau na watu mbalimbali waliojitokeza katika anniversary ya mwaka mmoja katika biashara. Actress Linda wa Lovely Gamble alikuepo

Amina,Frank na Nocha kwa pamoja

Dj Wailala kama kawaida alikamua

Hakika palikuwa hapatoshi

Wadau mbalimbali wakiwa na mzee wa nyuki Frank Eyembe



James na Salim wakishow love

Jesse na Gerald nao walikuepo

Watu wakiserebuka

Safina na Salim kwa pamoja walikuepo

Wadau,Jesse,Baraka na Chriss kwa pamoja wakiwakilisha

Dec 5, 2010

THE GREAT KANISANI(A.I.C.T CHANG'OMBE)

Juma pili ya leo The great nimesali kanisani katika kanisa langu la kila siku.Wahumini tukiwa kanisani

Muhubiri akihubiri neno la Mungu

Baada ya ibada the great nilipanda juu kupiga gitaa katika kwaya niliyowai kuimbia enzi zile,nilikuwa nikipiga gitaa la bass.

Tukishauriana tupige mziki katika key gani?G,F,D au?

Mziki umekolea,The great nikicharaza gitaa la bass kwa utaalamu

Baada ya ibada na kupiga gitaa niliingia katika gari langu na kuelekea home

Dec 1, 2010

MASHABIKI WETU WA CONGO OFF SIDE HIYO TWAWALETEA

Mashabiki wetu wa Goma,na Bukavu nchini DRC ndio watakuwa wa kwanza kuiona OFF SIDE pamoja na baadhi ya wasanii walioshiriki humo na wengine ambao mashabiki mmeomba kuwaona,ni December hii,nani anakuja ni The great na swahiba,Irene Uwoya,Aunty Ezeckiel na Mtoto Jeniffer,lakini pia tutawapa burudani jukwaani kwa mda wa dakika 30 mara baada ya kuzinduliwa OFF Side.kazi kwenu sasa.