Star Times
Mercy Beauty Parlour
Dec 23, 2010
Dec 22, 2010
BAADA YA KUMALIZIKA KWA KISHINDO SHOW YETU YA MWISHO BUKAVU MBUNGE WA BUKAVU ALITUKARIBISHA KWA CHAKULA NA VINYWAJI HOTELINI KWAKE MIMI NA SWAHIBA.
Honorable DAVID OMBENI Mbunge wa Bukavu akiwa mjini Kinshasa katika kikao chao cha mwisho cha bunge la DRC alipata habari kuwa katika jimbo lake vijana tumefika hivyo basi kutokana na kwamba alishindwa kuhudhuria show zetu zote za Bukavu jioni yake alipanda ndege na kutualika mimi na swahiba katika Hotel yake ya kifahari ijulikanayo LE V.I.P HOTEL kwa ajili ya chakula cha jioni.
Kutoka kushoto wa kwanza ni dereva aliyetumwa kutufata,wa pili nae ni mbunge,Swahiba,The great,Honorable David Ombeni na Socrates.
Kutoka kushoto wa kwanza ni dereva aliyetumwa kutufata,wa pili nae ni mbunge,Swahiba,The great,Honorable David Ombeni na Socrates.SHOW YETU YA PILI BUKAVU
Show yetu ya pili mjini Bukavu ilifanyika uwanjani ambapo umati ulikuwa ni mwingi sana kitu ambacho kilipelekea watu wawili kufariki,na wengine saba kulazwa hospitali kama majeruhi.Mungu alaze pema roho za mashabiki wetu waliopoteza maisha yao(Bukavu) maana lengo lao lilikuwa jema kutuona sisi,Na walioko Hospitali twawaombea uzima na afya tele zaidi ya yote twawapenda sana,lakini twashukuru kwa upendo wa dhati mliotuonesha,MUNGU IBARIKI BUKAVU.
Irene Uwoya akiingia uwanjani huku akilindwa na askari polisi na wanajeshi.Huku anajulikana sana kama Oprah.
Irene Uwoya akiingia uwanjani huku akilindwa na askari polisi na wanajeshi.Huku anajulikana sana kama Oprah.SAFARI YETU KUELEKEA OFISINI KWA WAZIRI WA UTAMADUNI BUKAVU.
Tukiwa Bukavu tulipata mwaliko kumtembelea waziri wa utamaduni Bukavu,hivyo msafara mzima ulikuwa hivi.
Baadhi ya mashabiki waliokuwa wakituona waliyazonga magari tuliyomo hivyo kusababisha foleni kubwa barabarani kama unavyoona.
Safari ikawa ngumu kidogo maana mashabiki walitaka kutuona na tuwasalimu kidogo nasi ikabidi tufanye hivyo kama unavyoona Jeniffa akiwa juu ya Gari kuwaridhisha mashabiki.Kwa upande mwingine Jenifa amekuwa kivutio kikubwa sana kwa watu na amejizolea mashabiki wengi sana Congo.
Tukiingia ofisini kwa Waziri
Nami nikiingia
Baadhi ya mashabiki waliokuwa wakituona waliyazonga magari tuliyomo hivyo kusababisha foleni kubwa barabarani kama unavyoona.
Safari ikawa ngumu kidogo maana mashabiki walitaka kutuona na tuwasalimu kidogo nasi ikabidi tufanye hivyo kama unavyoona Jeniffa akiwa juu ya Gari kuwaridhisha mashabiki.Kwa upande mwingine Jenifa amekuwa kivutio kikubwa sana kwa watu na amejizolea mashabiki wengi sana Congo.
Tukiingia ofisini kwa Waziri
Nami nikiingiaSHOW YETU YA KWANZA BUKAVU-DRC
OFF SIDE KUINGIA MTAANI KESHO KUTWA TAREHE 24.
Wakati Congo wakiwa tayari wameshaanza kuiona filamu hii niliyocheza na swahiba wangu hapa kwetu bongo itakuwa mtaani tarehe 24 yaani kesho kutwa ili mashabiki wetu wakila x-mass huku wakitazama OFF SIDE..Hakikisha unanunua nakala yako ORIGINAL na SIO FEKI au KUMUAZIMA JIRANI YAKO,NI VYEMA UKAWA NA NAKALA YAKO,TUWE WAZALENDO KWA KUPENDA KAZI ZANYUMBANI. 
Poster la movie Off Side linaonekana hivi......nikiwemo mimi,Swahiba,Irene Uwoya,Jb nk.

Dec 20, 2010
ZIARA YETU NCHINI CONGO katika uzinduzi wa filamu yetu ya OFF SIDE.
Jumatano iliyopita saa sita za mchana,The great,swahiba,Jenifa,Johari,Aunty na uongozi wa STEPS tulielekea nchini Congo kupitia KIGALI-RWANDA katika kuzindua movie ya OFF SIDE,Blog hii inakuletea matukio ya safari nzima na jinsi ilivyovunja rekodi kwa umati wa watu na mapokezi ya nguvu,mpaka sasa bado tuko huku Congo na hali imekuwa ni ya kushangaza.
Tukiwa uwanja wa MWL JK Nyerere tukisubiri kuondoka
Ndani ya ndege Johari,Jennifa,na Aunty katika pipa kwenda Congo kupitia Kigali
Pritesh kushoto na Jairad kutoka Steps
Me na Swahiba pipani
Jennifa alianza kutapika wakati ndege ilipoanza kushuka
Tukiwasili uwanja wa ndege wa Kigali na mapokezi yakawa hivi
Katika basi tukitoka airport sasa Jennifa yuko fiti hatapiki tena
Tukiwa uwanja wa MWL JK Nyerere tukisubiri kuondoka
Ndani ya ndege Johari,Jennifa,na Aunty katika pipa kwenda Congo kupitia Kigali
Pritesh kushoto na Jairad kutoka Steps
Me na Swahiba pipani
Jennifa alianza kutapika wakati ndege ilipoanza kushuka
Tukiwasili uwanja wa ndege wa Kigali na mapokezi yakawa hivi
Katika basi tukitoka airport sasa Jennifa yuko fiti hatapiki tenaPICHA ZAIDI KATIKA FUNGA MWAKA PARTY YA STEPS ENTERTAINMENT CO.LTD
Subscribe to:
Posts (Atom)




Tukiwa stejini tukiwapa raha mashabiki wetu
Hii ni sehemu mojawapo ya umati wa watu uliofurika uwanjani

































