Niliamua kumtembelea rafiki yangu baba
PAROKO Maganga wa kanisa la SINZA kufafanuliwa kuhusu pombe,niliamua kufanya hivyo kutokana kuwa na kauli tofauti toka kwa watu kuhusu pombe,wapo wanaosema pombe ni dhambi,wapo wanaosema unywaji wa pombe kupindukia ni dhambi,wapo waosema pombe ni haramu,lakini yapo madhehebu ya dini ambayo yanaruhusu unywaji wa pombe na yapo yanayokemea kabisa hata kugusa,na wote hao hutoa mistari toka katika Biblia takatifu kama kidhibitisho,Hii haimanishi mimi ni mnywaji wa pombe lakini ebu tujadili hili toka katika maisha yetu ya kila siku,toka katika maandiko ya vitabu vya dini lakini pia toka kwa wanafalsafa mbalimbali duniani na viongozi wetu.Katika utafiti wa kwanza niliofanya toka kwa Paroko yeye alisema....
''''Pombe ni kama kisu,ukikichukua kisu kukatia nyanya na vitunguu kisha ukapika chakula watu wakala hapo kisu ni kizuri,....ILA ..ukichukua kisu hicho hicho na kwenda kumchoma mtu na kumjeruhi hapo kisu ni kibaya,hivyo basi hata pombe ukinywa na kwenda kufanya yasiyofaa hapo ni mbaya kwako lakini ukinywa na bila kufanya mabaya hapo si mbaya hivyo inategemea na unavyoitumia yenyewe haina ubaya.'''''Jamani wanywaji na msiowanywaji ebu tuchangie hapa...............

Nikiwa ofisini kwake akinielekeza mambo mengi kuhusu Dunia

Mimi huwa napenda sana kudadisi kwa kuuliza maswali hapo nikiuliza swali?

Akinifafanulia jambo kwa umakini zaidi

Ukiwa katika ofisi za watumishi wa Mungu mda wote unajihisi kutakasika...

Baada ya maongezi alinisindikiza na tukapata picha ya pamoja

Hakika nilijifunza mengi sana hivyo nikawa nimeongeza vitu kichwani ila kwa leo tu naomba tujadili kuhusu POMBE...