Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Jan 7, 2011

MTOTO JENIFFER APOKEA TUZO YAKE YA MUIGIZAJI BORA

Jana katika ofisi za STEPS ENTERTAINMENT mbele ya waandishi wa habari mtoto Jeniffer alikabithiwa tuzo yake aliyopewa kama muigizaji bora kupitia filamu ya This is it iliyotolewa na MIN-ZIFF(Min Zanzibar international film festival).Lakini pia The great nilipokea tuzo ya filamu yangu This is it iliyoshinda kama filamu bora.Zoezi hili lilisimamiwa na wawakilishi wa kampuni ya STEPS ambao ni Mr.Kambarage na Bi. Simbizo.Pia kampuni ya STEPS ENTERTAINMENT CO LTD ilimpatia zawadi Jeniffer kama pongezi. Sajuki na Wastara walijumuika na wana habari kwa pamoja katika zoezi hili

Wana habari mbalimbali wakiwemo na TBC.



Jeniffer akishukuru kwa tuzo hiyo mbele ya waandishi na wawakilishi wa Steps,Shukrani zake nyingi alimshukuru UNCLE KANUMBA na WAZAZI WAKE.

Akikabithiwa tuzo yake toka kwa Mr.Kambarage

Akiionesha juu kwa wana habari

The great nikielezea furaha yangu juu ya Jeniffer

Nami nikabeba tuzo ya filamu yangu iliyoshinda

Mmoja wa mabosi wa STEPS,Mr.Jairad (wa pili kushoto)akimkabithi Jeniffer zawadi yake iliyotolewa na kampuni hiyo.

Jeniffer akiwa na wazazi wake(mama na baba mzazi)baada ya zoezi kuisha

Jeniffer na wazazi wake wakihojiwa na mwandishi maalum toka gazeti mojawapo la serikali.

Mama yake na Jeniffer(Rose)kwa furaha alilia na Jeniffer nae akalia

Mama alinyamaza lakini Jeniffer aliendelea kidogo,moja ya sababu zilizomfanya alie kwa uchungu ni alibeba mimba ya Jeniffer akiwa mdogo umri wa miaka 17 hivyo alitamani sana kuitoa hiyo mimba,alienda hospital kutoa mara 3 bila ya mafanikio matokeo yake mtoto aliyetaka kumtoa ndio Jeniffer ambae ni staa mwenye umri mdogo na leo anapokea tuzo ya muigizaji bora,



Uncle jj na Jeniffer tukipata picha ya pamoja na tuzo zetu bwana

SALAMU ZA GENEVIEVE NNAJI





Omotola na Genevieve katika scene














Warembo wa Nollywood pamoja na Genevieve

MC GEORGE ARUDI TENA KATIKA MZIKI

Mwandishi maarufu wa Global publisher maarufu kama MC George amerudi tena kwa kasi katika game ya mziki aliyoiacha takribani miaka nane iliyopita hivi sasa ametoa nyimbo 2 ikiwemo ya Historia zinazopigwa redioni na katika Tv station...hongera sana broh onesha kipaji chako toka moyoni.....konga nyoyo. Mc George akipiga gitaa

Akiweka sauti katika nyimbo zake

Jan 5, 2011

HAPPY BIRTHDAY ABOU HERMIS-DERNMARK

The great na blog hii twaungana na familia yako yote kukutakia maisha mema na furaha....Happy birthday Abou... ABOU HERMIS katika pozi

Jan 4, 2011

MTOTO JENIFFER APATA TUZO YA MWIGIZAJI BORA KUTOKA ZIFF.

Mtoto Hanifa Daudi maarufu kama JENIFFER jina nililompa katika filamu ya This is it na Uncle jj,amepewa tuzo ya mwigizaji bora kutoka katika tamasha fupi la filamu(Mini-ziff)lililokuwa Zanzibar kuanzia tarehe 31 Dec hadi 2jan 2011.Jennifer alipewa tuzo hiyo usiku wa tarehe 2 zanzibar katika ukumbi wa Ngome kongwe kupitia filamu yangu ya THIS IS IT ambayo nayo ilipewa tuzo kama filamu bora,hivyo kupelekwa katika tamasha lingine la filamu nchini Bukinafasso katika mashindano.Lakini pia kwa taarifa nilizopewa juzi na kutumiwa e mail mtoto Jennifer kupitia mtandao wa FILAMU CENTRAL amepewa tuzo ya msanii bora chipukizi kwa mwaka 2010 kupitia filamu hiyo hiyo yangu ya THIS IS IT.Mimi Steven Kanumba nikiwa kama producer na director niliyevumbua kipaji cha Jennifer,nikiwa mkurugenzi wa KANUMBA THE GREAT FILMS (kampuni inayoshugulika na maswala yote ya sanaa ya Jeniffer)na Mmiliki wa BLOG hii nachukua nafasi hii kumpongeza Jennifer kwa hatua aliyofikia akiwa bado na umri mdogo hakika najivunia hili. Jennifer na uncle jj kazini

Jeniffer akiwa location akishoot filamu ya uncle jj

Filamu ya This is it iliyoshinda na kumwezesha jeniffer kuchukua tuzo ya msanii bora.HISTORIA FUPI KUHUSU JENIFFER....Mwanzoni mwa mwaka 2010 chini ya kampuni yangu nilianzisha zoezi la kusaidia watoto wenye vipaji vya kuigiza ambao hawajaonekana kabisa katika tv au filamu hivyo niliitisha watoto zaidi ya 40 nikiwafundisha na kuwachuja mpaka akapatikana Jennifer na Patrick ambao chini ya uangalizi wa wazazi wao niliingia makubaliano nao ya kutocheza filamu yoyote ile mbali na kampuni yangu na zoezi hilo nikilisimamia sawia,pia kuhakikisha maendeleo yao shuleni yanapanda tulikubaliana kwamba mtoto atakaeshika namba tano kushuka chini namuondoa katika orodha na hatoshoot tena movie na mimi hivyo niliwapa nafasi ya kushika namba moja mpaka 4 kitu ambacho wanakitimiza maana kwa mihula 2 sasa Jennifer anaongoza kwa kushika namba moja na juzi kabla ya kuenda nae Congo alishika namba 2 darasani.Wakati Parick wakati wote aking'ang'ania namba 3,ambayo si mbaya.this is it.

HII NDIO KEKI ALIYOKATA ELIZABETH GUPTA

SEND OFF YA ELIZABETH GUPTA YAFANA SANA

Aliyekuwa mshiriki wa Big brother mwaka juzi Elizabeth Gupta juzi tarehe 2 january kulikuwa na send off yake yenye hadhi ya juu iliyofanyika katka ukumbi wa Diamond upanga,na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wakwe zake toka Nigeria.

Wakati wa chakula

Kevin and Eliza

The great sikuwa mbali katka wali

Mastaa mbalimbali waliitwa kupiga picha na Eliza na Kevin



Imaculate,The great,Eliza,Kevin na uncle Lundenga



Kulikuwa na red carpet nami nilipita kwa raha zangu

Mboni na Shamim zeze nao walikuepo



Kamati

Mama Eliza akitunzwa

Eliza,Me na Kevin



The great nikipata picha na warembo Penny na Naima

Jan 2, 2011