Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

May 26, 2011

KAJALA MASANJA KAMA GENEVIEVE NNAJI NA RAMSEY NOUAH

Msanii mpya katika filamu Kajala ameendelea kukamua vilivyo akiwa na Ramsey Nouah katika scene za ma love wakicheza kama mtu na mpenzi wake hivyo Kajala kuendelea kushika nafasi ya Genevieve Nnaji wa Nigeria. Kajala aki-rehasal na Ramsey


Kajala mwenzako yuko busy na kushika mistari wewe wasubiria picha?

wewe usicheze na mimi...ndio maneno anayosema hapo

Ramsey akisaidia kudirect baadhi ya sehemu


Ramsey akitazama ninavyokamua scene...


The great nikiwa kazini,,,kipaji toka moyoni.

UMEME UNAPOKATIKA LOCATION HALI HUWA HIVI...

Tatizo la umeme wetu wa Tz linavyoathiri hata tasnia yetu..... umeme hakuna hapo tunasubiri kudra za Mungu...


Ikabidi zianze story za Nigeria,Ramsey akisema mbona nyie hapa mna afadhali sie movie zote huwa tunashoot kwa generator maana umeme Nigeria unaweza kuwaka kwa dakika 20 na ukazimwa kwa siku 2 bila sababu na wananchi kwa sasa wameshazoea ndio maana kila nyumba za wenye uwezo huko zina Generator kubwa.


Ramsey na Samm(light man)


Ramsey akipakwa make up na Maya


The great na mimi nikila mapouuuudahh


Tukataka tupige scene hiyo nje lakini kelele za watu na magari yakazidi tukaacha,na ndani umeme hakuna basi ikawa ni kukaa tu.


Tukaingia ndani ili labda tutumie generator kushoot ndani lakini kelele za generator nazo zikatushinda tukabaki kupiga story tu....


Tukatoka nje ili tufanye mazoezi maana Ramsey anapenda sana kabla ya kushoot awe amerehasal mara kadhaa ili maneno yote awe ameyashika,movement,na hisia katika scene vyote viwe sahihi.


Akijaribu kuongea maneno ya kiswahili....


kutoka kushoto ni Msungu,dada alitutembelea kumuona Ramsey kidogo,Ally Yakuti ambaye ndiye mwandishi wa movie hii na ndiye mshindi wa tuzo ya uandishi bora wa script kutoka filamu central,Samm mzee wa light.

May 22, 2011

BONGO MOVIE FC YATOKA SARE NA WAANDISHI WA HABARI MWANZA

Katika uwanja wa CCM KIRUMBA -MWANZA kulikokuwa na mechi kari ya mpira wa miguu jioni ya leo kati ya BONGO MOVIE FC DAR ES SALAAM na WAANDISHI WA HABARI NA MA DJ MWANZA matokeo ni ngoma droo,japo sisi ndio tulikuwa wa kwanza kuliona lango lao kipindi cha kwanza,wao wakasawazisha kipindi cha pili,matokeo ni sareeeeee.... Steve nyerere na Jb wakipasha


Mashabiki walivyojaa uwanjani..


Maya akishangilia mara baada ya bongo movie kufunga goli la kwanza


Wadada zetu wa bongo movie tulionao mwanza...


Timu nzima ya bongo movie...The great nikiwa katikati..


MH.Highnes kikwia mbunge wa Ilemela akisalimia kikosi

BAADA YA KUMALIZA ZIARA YANGU SHINYANGA NA OXFAM NIMEKUJA MWANZA KUJUMUIKA NA WENZANGU WA BONGO MOVIE.

The great niko jijini Mwanza kujumuika na wenzangu wa bongo movie club katika mpambano wa mpira wa miguu dhidi ya ma Dj,na waandishi wa habari mwanza. Tayari niko na wenzangu katika basi linalotuzungusha hapa na pale


kwa pamoja tukiwakilisha


NIKAELEKEA WILAYA YA KISHAPU-SHINYANGA

Nikiwa nje ya ofisi ya OXFAM SHINYANGA,nikimsubiria dereva aje tayari kwa kuelekea wilaya ya Kishapu.


Nimefika kishapu nikiwa na dada Mwanahamisi(Mishy) toka OXFAM akinisaidia mambo kadhaa hapo,tulianza kwa kuongea na baadhi ya wakazi wa hapo kuhusu tatizo la chakula.


Hakuna mvua kwa mda sasa hivyo hakuna chakula kabisa mlo ni mmoja kwa siku,serikali ilitoa debe 2 kwa kila kaya lakini familia ni kubwa wapo walio 10 wengine 15 hivyo kwa msaada huo bado hautoshi,mifugo inakwisha kwa ukame.


Mzee akiomba watengenezewe mabwawa ya kuhifadhi maji alafu wenyewe watatengeneza mifereji ili ktk kipindi kigumu kama hiki wasiwe wanakosa chakula,


Mzee akijibu swali langu nililomuuliza kwanini wasilime mazao yanayostahimili ukame?akasema hata kama yanastahimili ukame lakini bado yanahitaji maji japo kidogo ili yastawi kitu ambacho hakipo hapo


Umri wa huyu mzee na mwonekano wake ni vitu viwili tofauti,njaa imewakumba,ana familia ya watu 11,asubuhi wanakoroga uji lita 20 hawana sukari wanaweka ubuyu au ukwaju wanakunywa,jioni saa moja ndio wanakula mlo wa mwisho siku imepita.


Huyu mama ana watoto 8 wa kwanza ana miaka 15 yuko darasa la saba wa nane ndio huyo aliyembeba,kutokana na njaa mme wake alimkimbia miaka 2 iliyopita akidai anakwenda kutafuta hadi leo,huyu mama hana kazi yoyote na familia ni kubwa,kuna siku inabidi watoto wasiende shule maana jana yake hawakula chochote mpaka akipata chakula wanakula ndio wanaenda shule hata kwa kuchelewa,shule za huku hakuna mabasi kama mjini ni kutembea sawasawa..


Nikijaribu kuongea nao kwa kisukuma kidogo maana ndio kabila langu....


Nikirekodi video ya mambo ninayoyaona huku,video inayotakiwa kusambazwa duniani kote nikihimiza mfumo wa chakula wenye usawa na haki uwe sawa kwa kila mtu duniani kote.


Ebu tizama ardhi ilivyokauka na huku ndiko waliko wakulima,unafikiri bei ya chakula itakuaje mjini,suala zima kilimo limewekwa nyuma vijana wengi wenye nguvu wanakuja mjini na kuwaacha wazee kijijini wasio na uwezo wa kulima sehemu kubwa,


Popote niendapo duniani watoto ndio huwa mashabiki wangu namba moja nami nawapenda sana maana huwa hawana chuki,majungu,roho ya kwanini,majivuno,matusi,kejeli na dharau huwa kama malaika wanionapo furaha iliyopo moyoni ndio hiyo huionesha usoni bila ya kificho wala kujishtukia nami ucheza nao na kufurai nao hujihisi niko na malaika,ndio maana niliamua kuwa nawatengenezea movie zao ili wajione tuko pamoja mfano THIS IS IT,na UNCLE JJ


Hapa fuhara yangu huwa inatoka moyoni,hunifanya kukumbuka enzi za utoto wangu ambapo sikuwai kufurai kiasi hiki wala kucheza na wenzangu bali mateso tu..


Baada ya mazungumzo kumalizika na wakazi wa wilaya hii ya Kishapu,kijiji cha ISOSO,na baada ya kumaliza kusalimiana na watoto nikaagana na huyu babu ambaye alitupa ushirikiano mzuri kabisa nikiwaahidi kuwa nitarudi tena na OXFAM kwa msaada zaidi.