Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Jan 7, 2011

MTOTO JENIFFER APOKEA TUZO YAKE YA MUIGIZAJI BORA

Jana katika ofisi za STEPS ENTERTAINMENT mbele ya waandishi wa habari mtoto Jeniffer alikabithiwa tuzo yake aliyopewa kama muigizaji bora kupitia filamu ya This is it iliyotolewa na MIN-ZIFF(Min Zanzibar international film festival).Lakini pia The great nilipokea tuzo ya filamu yangu This is it iliyoshinda kama filamu bora.Zoezi hili lilisimamiwa na wawakilishi wa kampuni ya STEPS ambao ni Mr.Kambarage na Bi. Simbizo.Pia kampuni ya STEPS ENTERTAINMENT CO LTD ilimpatia zawadi Jeniffer kama pongezi. Sajuki na Wastara walijumuika na wana habari kwa pamoja katika zoezi hili

Wana habari mbalimbali wakiwemo na TBC.Jeniffer akishukuru kwa tuzo hiyo mbele ya waandishi na wawakilishi wa Steps,Shukrani zake nyingi alimshukuru UNCLE KANUMBA na WAZAZI WAKE.

Akikabithiwa tuzo yake toka kwa Mr.Kambarage

Akiionesha juu kwa wana habari

The great nikielezea furaha yangu juu ya Jeniffer

Nami nikabeba tuzo ya filamu yangu iliyoshinda

Mmoja wa mabosi wa STEPS,Mr.Jairad (wa pili kushoto)akimkabithi Jeniffer zawadi yake iliyotolewa na kampuni hiyo.

Jeniffer akiwa na wazazi wake(mama na baba mzazi)baada ya zoezi kuisha

Jeniffer na wazazi wake wakihojiwa na mwandishi maalum toka gazeti mojawapo la serikali.

Mama yake na Jeniffer(Rose)kwa furaha alilia na Jeniffer nae akalia

Mama alinyamaza lakini Jeniffer aliendelea kidogo,moja ya sababu zilizomfanya alie kwa uchungu ni alibeba mimba ya Jeniffer akiwa mdogo umri wa miaka 17 hivyo alitamani sana kuitoa hiyo mimba,alienda hospital kutoa mara 3 bila ya mafanikio matokeo yake mtoto aliyetaka kumtoa ndio Jeniffer ambae ni staa mwenye umri mdogo na leo anapokea tuzo ya muigizaji bora,Uncle jj na Jeniffer tukipata picha ya pamoja na tuzo zetu bwana

4 comments:

Stella said...

Hongera sana mtoto Jenipher kwa kuonesha kipaji chako cha sanaa ukiwa na umri mdogo sana. Kaza buti katika masomo ili uendelee kuuza sura katika runinga.

Stella Kunambi

Stella said...

Hongera kwa wazazi wa jenipher kwa kumlea vema mtoto wenu mpaka amefikia hapo. Mungu awabariki muendelee kumtunza vizuri ili afanikiwe maishani.

Stella Kunambi

Stella said...

Uncle JJ big up sana! Nimekukubali katika movie unatisha. Na movie zako ni za ukweli asiye zipenda achimbe shimo ajifukie.

Stella kunambi

Albert said...

Hongereni sana Uncle JJ na Jennifer, kweli mna deserve tuzo hizo kila mtu anakili kwamba huu mtoto ni zaidi ya muigizaji. This is it ni movie yake ya kwanza na ameonesha kiwango cha hali ya juu na amepata tuzo ya muigizaji bora; na hadi sasa najiuliza itakua je kwenye movie yake ya tano au ya kumi?
Mungu azidi kumuongezea maisha, hakika mtoto huu ni zaidi ya muigizaji, na kila mtu anakiri!
Pole sana Mama-Jennifer, ujinga huo wa kutoa mimba umekua sugu kwa wasichana wengi, hii iwe fundisho kwao, wajuwe kwamba wale watoto wachanga wanaoua na kuwatupa chooni, ni watu wa thamani kubwa wenye vipaji ambavyo vinaweza kubadilisha dunia, ndiyo maana laana itakua juu yao mile daima!
Mungu bariki mtoto Jennifer na umlinde, umuongezee miaka.
Amen!