Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Dec 31, 2009

Buriani mzee KAWAWA (1926-2009)


Mzee Kawawa tutakukumbuka kwa mengi, kwa sisi wacheza filamu tutakukumbuka kama muasisi wa filamu wa enzi zile za zamani. Kati ya filamu alizocheza ni kama "MUHOGO MCHUNGU",  "MELI INAKWENDA, FIMBO YA MNYONGE n.k.
Kwangu mimi kama Steven Kanumba nitakukumbuka kwa heshima uliyowahi kunipatia mwaka juzi 2007 kwa kunialika kwako kwa kitafrija kidogo cha kunipongeza mimi kwa kazi zangu za filamu, hiyo ilikua ni heshima kubwa sana kwangu katika maisha yangu ya Sanaa. Mungu ailaze roho yako mahala pema peponi, Amina.

Dec 30, 2009

Mojawapo ya scene katika lovely Gamble naelekea kupanda Treni (underground railway)


JAMANI TUSIACHE KUONGEA!!Lovely Gamble


Moja ya scene ya Lovely Gamble katika Treni

Dec 29, 2009

Swahiba


Swahiba The greatest akiwa amepozi katika gari lake

Bonanza letu lilivyofana siku ya Boxing Day...


Kutoka kushoto Dude, The Great,  Beka, Hartman, Masanja na wadau katika Bonanza letu leaders Club.

The great pioneer, Chekibudi na Swahiba The Greatest siku ya Bonanza.

The Great na Yusuph Mlela wakiwa kiwanja flani

The great & Kinyaiya


Ben Kinyaiya (Kushoto) na The Great (kulia) wakiwa katika pozi

Dec 28, 2009

Hongereni YANGA


Hatimaye yale mashindano yanayoandaliwa na Bia ya Tusker (Tusker Cup) yamemalizika jana kwa wanajangwani Dar Young African (YANGA) kuchukua ubingwa huo kwa mara ya pili kwa kumkandamiza Sofapaka ya Kenya mabao 2 - 1. Yanga ambayo ilionekana kutawala zaidi mpira katika vipindi vyote viwili ilipata pigo la gori la kwanza kwa mpira wa adhabu uliopigwa moja kwa moja na kujaa wavuni katika kipindi cha kwanza. Yanga iliendelea kulisakama lango la sofapaka bila ya Mafanikio hadi wanakwenda kupumzika ikiwa nyuma kwa bao moja. kipindi cha pili yanga ilionesha uhai zaidi kwa kuendeleza mashambulizi yake lakini hayakuzaa matunda mpaka Papic (Kocha wa Yanga) alipoamua kumtoa Nsajigwa na Kumuingiza Fred Mbuna, na Jerryson Tegete kumpisha Boniface Ambani ambao kwa kushirikiana na Mrisho ngassa, Athumani Idd (Chuji) na wengineo katika safu ya Ushambuliaji wakaandika bao la kusawazisha mnamo dakika ya 86 kupitia kwa boniface Ambani. Muda sio mrefu mnamo dakika ya 90 yanga iliandika bao la Kuongoza kupitia kwa Mrisho Ngassa.

kutokana na hayo tunaipongeza Yanga kwa kuonesha mchezo mzuri na hata Kuchukua Ubingwa huo.

Dec 27, 2009

TUNAOMBA MAONI YAKO

Naomba utusaidie kukuletea taarifa haraka bila ya usumbufu wa kusubiri taarifa kwa muda mrefu. Je! kuna uchelewaji wa Page hii ku-load? au inashindwa kabisa ku-Load? au Afadhali? au Safi sana?  Akhsante sana!

Dec 26, 2009

Kwaya ya Vijana AIC Makongoro-Mwanza


Hii ni kwaya ya Vijana AIC Makongoro Mwanza. Walikuja nao kujumuika na wenzao wa Dar-es-salaam katika kusherehekea sikukuu ya Christmass

Mambo ya Christmass jamani Kanisani


unaweza ukaanza kujiuliza hapa ni wapi? Hapa ni kanisani AIC Chang'ombe siku ya Christmass, watu walijitokeza wengi sana katika ibada siku hiyo mpaka ikaamuliwa Ibada ifanyike nje kutokana na kwamba ndani kulikuwa hapatoshi

The Great kanisani AIC Chang'ombe


We unadhani mi sikuwepo? Hapa nikiwa katika ibada ya Christmas asubuhi na rafiki yangu wa siku nyingi (Bayuka). Tuliwahi kuimba wote katika kwaya enzi hizo........ yeye alikuwa akipiga kinanda, mimi nikipiga Gitaa la Bass.

Wakumsifu Mungu nao hawakua nyuma


Hii ni kwaya ya Neema Gospeli....., nilikua nikiimba katika kwaya hii hapo Chang'ombe enzi hizo. Hapa wakiimba katika ibada ya X-mass asubuhi.

Sety Mgusi akiimba kwa hisia

Dec 25, 2009

The great na Frank


Steven Kanumba (Kushoto) Akiwa na Produza wa Filamu ya Lovely Gamble Frank Yembe a.k.a mzee wa nyuki

Katika Boti


"...Hapa nikiwa pamoja na Meckisha katika Mojawapo ya Scene zilizopo katika Filamu ya Lovely Gamble"

On the Scene"...hapa nikiwa katika hekaheka za kushuti filamu ya Lovely Gamble nchini Uingereza"

Michezo; Simba na Yanga


Eeh Bwana daaah! Kweli Papic Noma!! yaani yale majigambo yote ya makocha wawili wa Simba na Yanga jana yalitupa majibu sahihi kwamba nani mkali zaidi ya mwenzake. Papic ndie aliyeibuka kidedeaa baada ya Timu yake ya Yanga kuifunga Simba ya Msimbazi mabao 2-1 na kufanikiwa kuingia fainali ya Kombe la Tusker itakayofanyika siku ya Jumapili na timu ya Sofapaka ya Kenya. Ambapo Simba itakutana na Tusker ya Kenya katika kugombania mshindi wa tatu mechi itakyopigwa siku ya Jumamosi kabla ya fainali J'2

Mmemuona MECKISHA?


Meckisha Macha; Msanii mpya wa kike anayekuja juu nchini
Uingereza akiwa katika Pozi la Kifilamu zaidi

Dec 22, 2009


Akiwa "ON-SET" (Mkao wa Kuanza Kushuti)

Jinsi ilivyokuwa ktk Filamu ya Lovely Gamble nchini UK


Kanumba; hapa akiwa location katika hekaheka za Kushuti filamu
 ya Lovely Gamble...

Dec 20, 2009

Kutoka kwa Kanumba:

"....nilikuwa Mwanza katika uzinduzi wa Filamu ya watu wa huko huko Mwanza iitwayo Mr. Contractor, ambapo nilialikwa kama mgeni rasmi. Kweli vijana sasa hivi wanafanya kazi hasahasa katika wigo huu wa filamu nadhani tutafika mbali baada ya kipindi si kirefu", asemavyo Kanumba baada ya kuwasili kutoka Mwanza.

Dec 19, 2009

Kaa tayari na Filamu mpya ya Crazy Love

....Steven Kanumba sasa yupo jikoni akiandaa kitu kipya ambacho kwa namna moja au nyingine nadhani kitaleta msisimko mkubwa kwa washika dau mbalimbali wa filamu na sanaa kwa ujumla.