Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Apr 28, 2011

NAWAONJESHA TU.....

Vipi tuanze kazi??????

Apr 25, 2011

KUTOKANA NA E MAIL NA MAONI YALIYOTUMWA MSHINDI NI HUYU..

Ramsey Tokunbo Nouah(Nigeria)....,Filamu iwe katika lugha mchanganyiko(kiswahili na kiingereza,...hayo ndio majibu nami nayafanyia kazi....Angalizo yale maoni au e mail zilizotumwa kwa lugha za matusi na kejeli hazikuhesabiwa kabisa maana humu sio sehemu yake.

Apr 17, 2011

TUKAMALIZA ZIARA YETU BUNGENI KWA KUHUDHURIA BUNGE LA JUMATANO ASUBUHI.

Ziara yetu tukaimaliza kwa kutembelea bunge letu siku ya jumatano asubuhi na kutambulishwa bungeni na spika wa bunge kisha tukarejea Dar....... Mheshimiwa Amosi Makala na The great
Swahiba na mbunge wa mvomero
Steve Nyerere kama kawaida yake na vichekesho vyake kwa mheshimiwa

Tukipiga story na mheshimiwa Shibuda(kati kati yetu)
The great na mama Rita Mlaki tukipata picha ya pamoja,

SIKU ILIYOFUATA TUKAONANA NA RAISI WETU MHESHIMIWA JAKAYA KIKWETE

Siku ya jumanne saa sita mchana mjini dodoma tulipata mwaliko wa kuonana na Raisi wetu wa Tanzania ambapo mheshimiwa alitualika mezani tukapata chakula cha mchana pamoja nyumbani kwake hapo na hapo ndipo tulipopata nafasi ya kuzungumza yetu ya moyoni yahusuyo tasnia yetu ya filamu kwa ujumla,la kufurahisha zaidi Raisi alianza kuyafanyia kazi yale tuliyomwambia hapo hapo mezani tukiwa tunakula akiagiza ufuatiaji wa karibu sana katika masuala tuliyowakilisha kwake..hii ikawa ni siku nzuri kwetu.....

Baada ya chakula mheshimiwa alimwita mpiga picha wake na kupata picha ya pamoja nasi.
PichaaaMheshimiwa akaagiza kupiga picha ya mmoja mmoja akaanza JB..
Richie akafata
The great ikabidi nimshike mkono kabisa Raisi
Odama akiwa haamini kama yuko na Raisi
Swahiba nae kwa kuniiga nae akamshika mkono....
Steve Nyerere na ukatuni wake kama kawaida
Jack Wolper akamaliza...

Apr 16, 2011

JIONI TULIALIKWA NYUMBANI KWA WAZIRI MKUU NA MAMA TUNU PINDA..

Ilipofika jioni tulipata mwaliko wa kutembelea nyumbani kwa waziri mkuu mwaliko tuliopata toka kwa mke wa waziri mkuu mama Tunu Pinda huko dodoma lakini pia tukapata mda wa kupata chakula cha jioni pamoja..... Shilole na The great baada ya kushiba
mama Tunu Pinda na swahiba
Jack wolper nae akafata
Odama nae
Richie nae akafata
JB na mama Tunu Pinda
The great nami sikuwa nyuma kuweka kumbukumbu
Steve Nyerere kama kawaida yake akaweka comedy zake
Picha ya pamojaaaa kwa umoja

ZIARA YA WASANII WA BONGO MOVIE DODOMA...

Jumamosi iliyopita wasanii kadhaa wa movie Tz tulielekea dodoma kuonana na waheshimiwa kwa ajili ya kujadili mambo kadhaa juu ya tasnia yetu ya filamu na mambo mengine zaidi tuliyotumwa kupeleka na wasanii wenzetu.......baada ya kufika tu dodoma tulikaribishwa na mheshimiwa mbunge wa Ifakara Abdul Mteketa... Shilole na Odama nao walikuepo
The great na Mh.Abdul Mteketa
Mdau na Jb..
Nyama ya nundu tulijipendelea
The great na Steve Nyerere katika story za hapa na pale
Katika maisha yangu napenda sana kucheka..

Apr 6, 2011

NI NANI KATI YA WASANII HAWA KWA MWAKA HUU WEWE KAMA SHABIKI WANGU WA KWELI UNGEPENDA NIFANYE NAE KAZI??

Kwa mwaka huu nimepanga kufanya kazi na msanii mmojawapo kati ya hawa hapa chini(DESMOND ELLIOT,RAMSEY NOUH na VAN VICKER) sasa nakupa nafasi kwa wewe shabiki wangu kunichagulia ni yupi ambaye ungependa kuona nafanya nae movie kwa mwaka huu nami NITATIMIZA AHADI HII,tuma maoni yako kwa kupendekeza jina la msanii,ni wapi utapenda movie hiyo ichezwe yaani TANZANIA,GHANA AU NIGERIA?Lugha ipi itumike?filamu itahusu mambo ya secret society yaani jamii fulani ambayo haiamini Mungu kabisa bali shetani na wamefanikiwa kuiteka dunia kwa power,pesa,umaarufu na technology nk ambao pia wana ishara zao na ibada zao sasa pendekeza ni jina gani litakalofaa kuwa jina la movie?Kwa muonekano na uigizaji wote hapo wanaweza sasa chagua mmoja majibu nitayatoa tarehe 25 ya mwezi huu...kama mkereketwa wa sanaa hii ya filamu unaona utataka kuchangia chochote kwa hali na mali kufanikisha zoezi hili basi wasiliana nami kwa e mail info@kanumba.com (ila sio lazima)shukrani nitaandika katika movie lakini pia kama ni kampuni basi nitaweka tangazo lako katika movie hiyo kulingana na mchango wako iwapo zoezi litafanikiwa maana si kazi ndogo....asanteni.. DESMOND ELLIOT(NIGERIA)
RAMSEY NOAH(NIGERIA)
VAN VICKER(GHANA)..

THE SHOCK sasa yakamilika na yamalizika kuwa mtaani jumatatu...

Filamu yangu ya The Shock ndugu wadau imekamilika kwa sasa hivyo jumatatu kaeni mkao wa mezaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii kumuona SHAZ SADRY..... Kazini The great na Shaz huku cameraman wangu Zakayo akishoot


camera ninayotumia DSR SONY 390......
Shaz akipiga picha na camera iliyokuwa ikimshoot
mmmmmmh mie sisemi....
Zakayo Magulu(cameraman) na Shaz Sadry mara baada ya kumaliza kazi
Shaz na Afande Kiuno location manager wangu na soundman mara baada ya kazi....