Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Jan 4, 2011

MTOTO JENIFFER APATA TUZO YA MWIGIZAJI BORA KUTOKA ZIFF.

Mtoto Hanifa Daudi maarufu kama JENIFFER jina nililompa katika filamu ya This is it na Uncle jj,amepewa tuzo ya mwigizaji bora kutoka katika tamasha fupi la filamu(Mini-ziff)lililokuwa Zanzibar kuanzia tarehe 31 Dec hadi 2jan 2011.Jennifer alipewa tuzo hiyo usiku wa tarehe 2 zanzibar katika ukumbi wa Ngome kongwe kupitia filamu yangu ya THIS IS IT ambayo nayo ilipewa tuzo kama filamu bora,hivyo kupelekwa katika tamasha lingine la filamu nchini Bukinafasso katika mashindano.Lakini pia kwa taarifa nilizopewa juzi na kutumiwa e mail mtoto Jennifer kupitia mtandao wa FILAMU CENTRAL amepewa tuzo ya msanii bora chipukizi kwa mwaka 2010 kupitia filamu hiyo hiyo yangu ya THIS IS IT.Mimi Steven Kanumba nikiwa kama producer na director niliyevumbua kipaji cha Jennifer,nikiwa mkurugenzi wa KANUMBA THE GREAT FILMS (kampuni inayoshugulika na maswala yote ya sanaa ya Jeniffer)na Mmiliki wa BLOG hii nachukua nafasi hii kumpongeza Jennifer kwa hatua aliyofikia akiwa bado na umri mdogo hakika najivunia hili. Jennifer na uncle jj kazini

Jeniffer akiwa location akishoot filamu ya uncle jj

Filamu ya This is it iliyoshinda na kumwezesha jeniffer kuchukua tuzo ya msanii bora.HISTORIA FUPI KUHUSU JENIFFER....Mwanzoni mwa mwaka 2010 chini ya kampuni yangu nilianzisha zoezi la kusaidia watoto wenye vipaji vya kuigiza ambao hawajaonekana kabisa katika tv au filamu hivyo niliitisha watoto zaidi ya 40 nikiwafundisha na kuwachuja mpaka akapatikana Jennifer na Patrick ambao chini ya uangalizi wa wazazi wao niliingia makubaliano nao ya kutocheza filamu yoyote ile mbali na kampuni yangu na zoezi hilo nikilisimamia sawia,pia kuhakikisha maendeleo yao shuleni yanapanda tulikubaliana kwamba mtoto atakaeshika namba tano kushuka chini namuondoa katika orodha na hatoshoot tena movie na mimi hivyo niliwapa nafasi ya kushika namba moja mpaka 4 kitu ambacho wanakitimiza maana kwa mihula 2 sasa Jennifer anaongoza kwa kushika namba moja na juzi kabla ya kuenda nae Congo alishika namba 2 darasani.Wakati Parick wakati wote aking'ang'ania namba 3,ambayo si mbaya.this is it.

10 comments:

Anonymous said...

Hapo mwisho sasa ndo umeharibu ulipoweka kizungu ndivyo sivyo

Majoy said...

Hongera Steve kwa hatua uliyofikia lkn kikubwa nakupongeza kwa kusimamia na kufatilia pia maswala ya shule kwa watoto hao nina hakika utakua unawafundisha pia maadili ya kuishi ukiwa staa hivyo hawatakuja kutia aibu kama lulu.unastahili sifa kwa hilo,ubarikiwe sana.

Joyce aka Majoy!

Anonymous said...

kwa kweli nimefurahi sana kama unafatilia vema mwenendo wa watoto hao. Tafadhali sana huyo binti uzidi kumfatilia asije akaharibikiwa kwa baadae kama lulu kwani nae alianza kuigiza akiwa mdogo zaidi ya jenifer. TAKE CARE

Anonymous said...

Kanumba....amini msaada wako ni mkubwa kwenye sanaa hii, lakini amini pia watanzania hatupendani ndiyo maana hatuendelea, kwenye siasa, uchumi, sanaa na chochote kile, yaani hata ushoga..... chuki mbaya.

Anonymous said...

Hili la kushuka kielimu umtimue ndiyo zuri zaidi, maana bila hivyo wanaojidai haki za minaadam unge dili nalo... Big Up

Anonymous said...

Yakweli hayo

Anonymous said...

SASA AMEHARIBU NINI HAPO? YAH THIS IS IT, WATOTO WANAFANYA VIZURI SHULENI NA KWENYE FILAMU WAKO JUU, BIG UP KANUMBA, YANI MIMI MWENYEWE NIKIANGALIA HII FILAM HUWA NAFURAHI MPAKA NALIA KWA FURAHA HONGERA SANA KAKA KAZA BUTI MWAYA, SI UNAJUA KWENYE MAFANIKIO LAZIMA WATOTEKEA WA KUKUSHUSHA USIKUBALI KUSHUKA KWA MANENO YA WATU WASIOPENDA MAENDELEO YAKO.

ney said...

Kanumba please huyo mtoto mumlee katika maadili mema na shule aendelee tena uwe mkali sana ktk hilo pia umwambia na mama yake rose amsimamie sana mtoto asije akawa kama lulu maana kashindikana,plz tunaomba tasnia ya filamu isije ikaonekana kuwa tishio kwa watoto hata wazazi wakawakatalia watoto wao kuingia ktk filamu kwa kuogopa watoto wao kuacha shule na kufanya ufuska kaam wa lulu maan kasoma shule zaidi ya mia na mpk sasa hajulikani anasoma wapi maana alikokuwa kakimbia na kujifanya kamaliza form four kumbe term nzima ya form 3 hajaonekana shule. plzzz mtulelele watoto wetu vizuri

Stella said...

Yes brother K, nimekupata vizuri kupitia cv yako. Hongera sana kwa kuinua kipaji cha mtoto Jenipher na patric. Jenipher anatisha kimasomo na kisanii pia. Kaza buti kaka. Ushauri wa bure: Wasanii undeni tume ya kumuonya Lulu kwani anawaaibisha watoto wenzie wasanii, tunahis nao watakuwa km Lulu.

Stella Kunambi

Anonymous said...

Congaratulations Mr.Kanumba for the good work you are doing..am a good fan of yours and always miss your vituus when I watch a bongo movie without u being featured...anyways Movie industry is growing in our country, there a lot of copying ang lack of creativity and an advise to you guys who are in movie industry,tafadhali msilipue kazi kwani this is a project undertaking...ni bora utumie miezi kadhaa ukiwa project watengeneza filamu kuliko hii kutoa kila wiki filamu zisizokuwa na ubora...mfano mtu anaigiza akiwa anaishi maisha ya taabu kijijini lakini nywele ameweka wave...amescrub uso...no ways... hapo hamna kuvaa uhusika kabisa..ni ulipuaji wa kazi...be seriuos and in fact am not blaming u but I understand that the industryis still growing and we r in the right track....Hongera sana Kanumba na wengine wanofanya vizuri kama ww.