Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Dec 31, 2010

BAADA YA NDOA YA KIMILA MIKE EZURUONYE AKAMALIZA KWA NDOA YA KANISANI

Jumamosi ya tarehe 13 November 2010 msanii wa filamu wa Nigeria aliyefunga ndoa ya kimila mwezi wa tano alidhihirisha nia yake kwa kufunga ndoa yake kanisani na mkewe Nkechi Nnorom a.k.a Keke.(si msanii wa filamu)Uhusiano wao ulianza miaka 2 iliyopita wakati Mike alipokuwa akishoot movie kwao na Nkechi wakati huo Nkechi alikuwa akisoma nchini Canada hivyo alikuwa amekuja rikizo ndipo mambo yalipoaanza.Mike alimsuprize Nkechi siku ya birthday party yake kwa kumvalisha pete ya uchumba tayari kuelekea katika ndoa,,,hatimae tarehe 13 ya Nov chini ya bestman wake ambae nae ni star wa movie Nigeria (Nonso Diobi)akatimiza andiko. Bestman Nonso Diobi akitoa shukrani kwa waalikwa ukumbini

Mmmmhh.....

Mr&Mrs Mike Ezuruonye

Wakikata keki..hakika ni keki ya aina yake

LovelyWapambeWakionesha vyeti vya ndoa

Pete kidoleni

Kanisa lilipambwa hivi

Gari ya kifahari hummer limozin ndio alikuja nayo bwana harusi

Hii alikuja nayo bibi harusi...Picha na Bella Naija...Thank u Bella.

HAPPY BIRTHDAY DADA SANURA HUSSEIN

The great na blog hii twakutakia maisha mema na baraka huko Dernmark.... Dada Sanura ktk pozi

The great na Da Sanura siku aliponitembelea location kwangu nilipokuwa nikishoot movie yangu ya YOUNG BILLIONAIRE na yeye akashoot scene mojawapo humo.

NDOA YA KIMILA YA MUIGIZAJI MIKE EZURUONYE

Nyota wa filamu nchini NIGERIA Mike Ezuruonye tarehe 22 May 2010 alifunga ndoa ya kimila kijijini kwao Mbano-Imo state na mkewe Nkechi Nnorom.Nchini Nigeria ndoa ya kimila huwa ni muhimu sana ifanyike kuliko hata zile tulizozoea hapa kwetu..hivyo kwa wenye uwezo hulazimika kufanya ndoa mara mbili yaani ya kimila na ile ya kanisani au msikitini kama alivyofanya hata msanii Ini Edo...Tizama picha zake hapo chini na wasanii wenzake walivyompa sapoti ya nguvu. Nkechi na Mike

Wapambe wakiwa katika sare

Wasanii wa kike waliokuja kumsapoti Mike,kutoka kushoto ni Ini Edo,Chioma chukwuka,Tonto Dikeh,Jack Apiah,Uche Jombo na rafiki yao

Jack Apiah akiwasili kijijini

Ini Edoh nae akiwasili kijijini

Tonto Dikeh nae akiwasili kwa haraka

Desmond Elliot moja kwa moja alienda kumkumbatia rafiki yake mara baada ya kuwasili kijijini.

Chika Ike mwenye top nyekundu nae alikuepo

Mchekeshaji maarufu katika filamu Chinedu Ikedieze nae alifika

Chioma na Uche

Dec 25, 2010

ASET YAMFANYIA HITMA MAREHEMU ABOU SEMHANDO

Katika ofisi za ASET ndipo ilipofanyika hitma ya aliyekuwa mwanamziki na meneja wa bendi ya African stars(twanga pepeta) Abou Semhando,ambayo ilihudhuriwa na watu mbalimbali maarufu. Dua ikisomwa

Mzee Mapili nae alikuwa na machache ya kusema

Swahiba,The great na Fargason tulikuepo

Watu mbalimbali

Mkurugenzi wa ASET mama ASHA BARAKA akihojiwa na wana habari

Mambo ya msosi

BAADA YA KUMALIZA ZIARA YETU CONGO TULIRUDI NYUMBANI TANZANIA

Tukiwa ktk uwanja wa ndege wa Dar es salaam tukitokea Congo tulipokelewa na wana habari mbalimbali waliotuhoji mambo mbalimbali juu ya ziara yetu.

Me na Swahiba tulipewa maua kama pongezi

Baada ya hapa tulipanda magari yetu kuelekea majumbani kwetu.

SHOW YA PILI UWANJANI GOMA-CONGO

Jenipher akielekea kuwasalimu mashabiki

Akiwa mbele tayari kwa kutoa salamu

mmmh?

Aunty akielekea kusalimu mashabiki

Johari akisalimu mashabiki

Irene Uwoya akiinuka kuwasalimu

AkiwakaribiaNikitoa salamu kwa mashabiki

Swahiba nae akitoa salamu

The great nikifungua show kuanza..

Mambo yameanza..

Swahiba nae akafata kama unavyomuona

SAFARI YETU NA MAPOKEZI YAKE MJINI GOMA-CONGO

Baada ya kumaliza vizuri maonesho yetu mjini Bukavu-Congo tulielekea mjini Goma mji mwingine ulioko nchini Congo,huko mapokezi yake yalikuwa zaidi ya Bukavu.Huku nako watu 5 walilazwa hospitali kwa kuumia,na mtu mmoja alifariki dunia.Pia inasemekana wanawake 7 waliachwa na waume zao kutokana na kwamba waliwaacha watoto nyumbani na nyumba zao kuja katika onesho kutuona. Mtoto Jennipher akihojiwa na wana habari,kushoto ni mama Vero mwenyeji wetu,kulia swahiba.

Furaha kwa mapokezi mazuri

Msafara barabarani ulikuwa hivi.Tathimini mwenyewe ni kiasi gani sanaa hii ya filamu tulivyoitangaza ndani na nje ya nchi,Huku tunasimama kama ma balozi wa nchi yetu tukipepea bendera yetu kupitia filamu zetu.Swali Je Serikali yetu inayatambua haya?Viongozi wetu wanayajua haya?kama wanajua mbona kimya kutetea kazi zetu za filamu?kama hawajui ni kwanini hawajui wakati wapo hapo kwa ajili yetu?

Tukiwa juu ya gari ili mashabiki watuone kwa ukaribu

Hali ndio ilikuwa hivi..

Jenipher na Aunty wakiwapungia mashabiki mikono huku wakilindwa

Ukumbini kulikuwa hivi

Tukifatilia onesho kwa umakini

The great nikikaribishwa stejini na Mc