Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Nov 30, 2010

FILAMU YA UNCLE JJ YAINGIA MTAANI KWA KISHINDO YAVUNJA REKODI YA THIS IS IT

Wadau ile filamu yenu mlioisubiri kwa hamu ya UNCLE JJ niliyocheza na wanangu(watoto)iko madukani kote sasa,na mpaka sasa imevunja rekodi ya ile ya mwanzo ya THIS IS IT,Pata nakala yako original ktk dvd,vcd na vhs. Poster la UNCLE JJ

Nilitembelea duka moja kariakoo ambapo wamachinga walifurai kuniona na kuomba picha na mimi.

UNCLE JJ dukani

Hili ni duka mojawapo ambalo wamenihakikishia movie hii imevunja rekodi ya filamu bongo ikiwemo This is it maana duka hili tu copy 4000 za dvd na vcv 200 zimekwisha siku hii tu ya kwanza.Nawashukuruni sana mashabiki wangu bila ninyi hakuna Steve kanumba,nami ntazidi kuwakonga nyoyo maana nina kipaji toka moyoni.

Nov 28, 2010

MMMH PICHA YETU YA WEEK

TOKA OPRAH NA SASA OFF SIDE

Mwaka 2008(OPRAH) Irene Uwoya na Kanumba

Ray na Kanumba

Maeneo ya Zanzibar,Uwoya,kanumba,maya,ray na Aunty.

Mwaka huu 2010(OFF SIDE) Uwoya na Kanumba

Kanumba na Ray katika Off side

HAPPY BIRTHDAY MDAU WETU INO BARCHARD

Mdau mkubwa wa Rj company na Kanumba the great film ndugu Ino Barchard amesheherekea kuzaliwa kwake maeneo ya sinza mori jirani na ofisi ya Rj,watu watu wamekula na kusaza,The great nami nilikuepo kumpa sapoti mdau wetu maana yeye kila tukiwa location tukishoot huakikisha anatembelea mara kwa mara na kutoa mchango wake wa hali na mali.Happy Birthday Ino. The great,Ino Barchard,SwahibaWaalikwa wakijipiga vinywaji

The BIG TWO wakipata msosi ulioandaliwa na mdau Ino.

Chopa mchopanga,Slyvia,na Maya

Slyvia &Ino

Nov 26, 2010

SEND OFF YA FAIDA EZECKIEL GRAYSON

Send off ya dada yake na muigizaji mwenzetu Aunty Ezeckiel Grayson ilifanyika ukumbi wa E stana kijitonyama,ilijaza watu wengi na watu maarufu,Matron wake alikuwa muigizaji mwenzetu Mayasa Mrisho..tizama picha chini. Maya na bi harusi mtarajiwa Faida
Watu wakiserebuka

Faida na Maya

Waigizaji wa kike walishirikiana vizuri na Aunty hakika hili ni la kujivuniaBOZI BOZIANA NDANI YA BILCANAS

Mwanamziki toka Congo akiwa na wanamziki wake akiimba moja ya nyimbo zake zilizovuma enzi zile alipokuwa na akina Skola Miel

Bozi Boziana jukwaani

Nov 23, 2010

Nov 18, 2010

PICHA ZAIDI ZA OFF SIDE


Nov 14, 2010

GARI YANGU YA PRODUCTION(KANUMBA THE GREAT FILM)

Wadau,ndugu zangu na mashabiki zangu hii ndio gari yangu katika kampuni yangu ninayotumia katika shughuli zangu za production(movie)wasanii au crew yangu na mambo mengine yahusuyo production basi huwa humo hivyo kurahisisha mambo ya usafiri kwenda location na kurudi,hivyo wakati wa kazi itatumika gari ya kazi na wakati wa matanuzi(matembezi)itatumika gari ya matembezi.Asanteni sana mashabiki wangu wa kweli toka moyoni kwa upendo na ushirikiano wenu kwangu hasa hasa kwa kununua kazi zangu original na si feki,endeleeni hivyo nami nawaahidi kuzidi kuwapa kazi nzuri na bora maana bila ninyi nisingekuepo mimi Steven Kanumba,Mungu awabariki sana na abariki sanaa ya filamu Tanzania.Upendo wangu wa dhati u katika mashabiki wangu wa kweli toka moyoni,walio wazalendo,wenye kuheshimu na kupenda sanaa ya nyumbani.Ubavuni inavyoonekana

Upande wa pili yake

Kwa mbele

Kwa nyuma

Pembeni The great nikitabasamu kwa mbaliiiiiiiiiii