Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Mar 31, 2010

DR.CHENI AJA KIVINGINE KABISA KATIKA MOVIE YAKE MPYA YA ONE BY ONE

Hii si ya kukosa jamani mbali na kuwa muigizaji mzuri sana katika tasnia yetu ya filam hapa Africa mashariki lakini ni producer mzuri wa filamu hii si ya kukosa kaonesha uwezo mkubwa sana pata nakala yake halisi yaani original na si fake saidia kunyanyua maisha ya wasanii wako TZ.

Thea na Cloude kama kawaida yao uwezo wao huwa ni mkubwa sana katika acting na ni wakongwe katika industry hii.

Cloude na Cheni katika moja ya matukio katika movie hii

Sajuki a.k.a baba Wastara kaonesha kiwango cha juu sana na hili nalijua maana nimeshafanya nae kazi katika Hero of the church.

Hapa katikati ya scene lazima tuukubali ukweli kuwa jamani vijana wetu wanajitaidi sana

Unaweza kudhani kisu kimezama kabisa kumbe ni mambo ya ma utundu tu ili kuwapa radha nzuri mashabiki wake

Hongera sana Dr.Cheni The great na blog hii twakupa hongera kwa kazi nzuri hakika penye nia pana njia.

Mar 30, 2010

KANUMBA THE GREAT FILMS mambo bado yanapikwa leo ilikuwa ni siku ya kupiga scene za MONTAGE ktk movie

Cameraman wangu kutoka GRM PRODUCTION Lusubiro Mwanguku Akiwasili location tayari kwa kuanza ku set vifaa ili shooting ianze.

Huyu dada ni shabiki yetu mkubwa na mdau toka UK alifurai sana kukutana nasi maeneo hayo hivyo akaomba kupiga nasi picha mimi na Aunty lakini pia tulimualika katika set ashuhudie jinsi tunavyorekodi

Kazi imeshaanza bila kupoteza mda.

mmmmmmh ni acting tu jamani na si vinginevyo katika kupata montage nzuri

Unaweza kudhani ni BRAD PITTY na ANJELINA JOLIE ahhahahahah

Duh?Gwantwa utaniangusha bwana

Jamani katika movie hii nimejiandaa vizuri sina haraka na sikurupuki kama kawaida yangu ni kubring the best and great

Sio siri kwa sasa kiwango cha Aunty Ezekiel kimeongezeka zaidi mbali na kuwa directed pia kutumia script lakini yeye kama msanii ana vitu vyake vya ziada ambavyo kwa hakika vimeongeza utamu wa movie

Kazi ikiendelea sawia

The great na Gwantwa katika mapozi kuntu

Baharini tukiendesha pikipiki ya majini ni montage mojawapo katika movie hii

Tukipiga masafa huku camera imefungwa katika crain ikitufata

Kuna wakati Aunty alikuwa muoga pindi nilipokuwa nikikimbiza pikipiki ikabidi nimshushe kwanza nirekodi peke yangu huku nikiwa katika spidi kali katikati ya bahari

Maya akimfungua boya Aunty mara baada ya kumaliza kurekodi montages

Aunty Gwantwa akifungwa boya na kupewa maelekezo jinsi ya kulitumia kabla ya kuanza kazi.

BIRTHDAY YA NICE CHANDE YAFANYIKA KATIKA BOAT KATIKATI YA BAHARI YAFANA SANA

Tino akicheza mara baada ya kutoka kuogelea katika visiwa vya bongoyo

Hapa mzuka ulimpanda akacheza sana wakati boat inakwenda

Alianza hivi kabla ya kuvua shati

Watu mbalimbali maarufu walikuepo,watangazaji wa tv.waigizaji,wanamziki na wadau

The great nilichukua tahadhali mapema kwa kuvaa boya japokuwa safari na party nzima ilikuwa shwari kabisa

Nice chande akimlisha keki mdogo wake Neema chande

Akikata keki tayari kwa kuliwaKeki yenyewe kabla ya kukatwa

Watu wakiparty

Nikiteta jambo fulani la kazi na production manager wangu Maya

The great nilipewa nafasi ya kuongea machache

Musa wa kipindi cha USWAZI eatv ndiye alikua MC wa party nzima hakika alimudu vilivyo

Wadau wakubwa wa RJ COMPANY na KANUMBA THE GREAT FILM walikuepo,kwa mbali mwenye miwani ni mdogo wangu Yusuph Mlela

Hii ndio boat yenyewe ambayo shughuli nzima ilifanyika humo.

Mar 26, 2010

MASTAA NI WENGI KTK MOVIE HII PIA UBORA NA TEKNOLOJIA VIMEZINGATIWA SANA.

Tino nae yumo akiwa na AuntyMonica Malaki nae ndani kwa sana tu.

Nice Chande nae kakamua kuliko kawaida

Kwa mara ya kwanza nitaonekana nikicheza pamoja na Flora NvungiHapa ilikua ni patashika huyu dada kumbe ni mkali balaa katika kuact.Toka nimeanza hii sanaa ya film nilikuwa na hamu na ndoto ya kuja kuact na wewe The great hakika leo ndoto zangu zimetimia ni maneno yake Flora Nvungi star wa Bongo Dar es salaam


Kazi ikiendelea

Hakika Patcho Mwamba ni mwamba imara katika acting kafanya vizuri sana katika movie hii pia ni mtu mwenye ushirikiano sana.

Ameen...

Scene za nje ambazo pia huitaji magari mazuri kulingana na story

Crain ikifanya kazi yake huku Lusubiro akiiongoza kunifataHakika najivunia kuwa muigizaji

Katikati ya scene nikiitendea haki scene na story kwa ujumla

Hii ni gari niliyotumia katika baadhi ya scene kama mnavyoona hapo imepambwa kwa ajili ya harusi huku vijana wa kazi wanaoshoot kama walinzi wangu wakilinda....kwa jina la Mungu hii movie itavunja rekodi ya zote jina bado kapuuuuuuuuuuni.