Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

May 31, 2010

THE GREAT NA ADOLPHE DOMINGUEZ WA WENGE MUSICA

The great niliamua kumtembelea hotelini alipofikia mwanamziki mkongwe kutoka CONGO ambae pia ni muasisi wa wenge musica bcbg kabla ya kujiengua na kuunda kundi lake la wenge tonya tonya,nikaamua kumtoa kidogo kwenda sehemu kadhaa kama... Hapa ilikuwa katika studio za GRM PRODUCTION tukipiga picha za kumbukumbu ambapo pia video camera ilikuwa ikishoot ambayo nayo nilimpatia aondoke nayo.


Hapa akiwa na mkurugenzi wa GRM PRODUCTION Nd.G.Makupa ambae zoezo zima la picha aliliongoza yeye hapo studio.

Hapa nikimkabithi zawadi ya simu mpya kama kumbukumbu pindi afikapo kwao

mdau,adolphe,the great na G.Makupa kwa pamoja baada ya kumpatia zawadi ya simu Adolphe

Hapa nikimkabithi zawadi ya movie yangu mpya inayosumbua kisawaswa THIS IS IT 1&2 ambayo aliomba maana kwao bado haijafika

kwa pamoja tukiimba wimbo wake wa VOYAGE alioutunga na kuimba zamani akiwa na wenge bcbg akiwa na JB MPIANA,BLAISE BULA,WERRASON,AIMELLA,ALLAIN MPELLA,ALLAN MAKABA,nk.

aliniomba kabla ya kumkabithi movie zangu nisaini kwanza nami nikafanya hivyo

Nae pia baada ya kumrudisha hotelini alinipa zawadi ya albam yake mpya aliyoimba na KOFFI OLOMIDE(audio na dvd)inayoitwa SUSPENSION

Hii ni moja ya picha tulizopiga na kuzikuza na kutoa picha kubwa2 ambazo kwa upande wake alisema anaenda kupamba nyumbani kwake lakini mimi nilisema ntaweka ofisini kwangu ambapo nilimpitisha akapaona.

May 29, 2010

SUPRISE YA ADOLPH DOMINGUEZ KWA THE GREAT

Katikati ya wimbo msanii huyu alisimamisha kuimba na kuniita mwanzoni nilidhani kakosea jina lakini alizidi kusisitiza kuwa namuomba yule mucheza movie wa hapa akataja tena jina Steve Kanumba,nikaenda mbele nae akasema hivi nanukuu...''Njo vile huyu jamaa anatafutwa sana Congo,vile namuonaga ku movie Congo wanamupenda sana mimi nitapeleka yeye Congo,napeleka yeye ZENITH wanamuona wanafurai sana steve kanumba'' mara nilipofika mbele nae ndio akaanza kuongea nikagundua kuwa sanaa inatembea sana nilidhani mimi tu ndio namjua kwa mziki wake toka wenge musica kumbe hata yeye anaona kazi zangu twajuana ila hatujawai onana tu.

''mimi napeleka yeye congo,napeleka zenith......akisema

Gafla tukawa marafiki na baada ya kumaliza kutumbuiza tukabadilishana namba za simu

hapa aliniita tena akiwa na swali anataka kuniuliza juu ya movie na tangazo fulani congo.

tukazidi kupeana mawasiliano mengine zaidi ili baadae tukae tujue tunafanya nini katika sanaa zetu hizi.

UTAMBULISHO WA BENDI YA EXTRA BONGO WAFANA SANA MSASANI CLUB

PROFESA JAY ALIKONGA NYOYO ZA MASHABIKI VILIVYO

THE GREAT NA STEVE NYERERE AMBAE NAE ALIVUNJA MBAVU ZA WATU SANA

MATONYA NAE ALIFANYA KWELI

HUSSEIN MACHOZI NAE ALIKUEPO

MWANAMZIKI TOKA CONGO ADOLPH DOMINGUEZ ALIFUNIKA VIBAYA SANA HASAHASA KATIKA KUCHEZA ALIKUMBUSHIA ENZI ZA PENTAGONI NA WENGE MUSICA

MC MAIMATHA AKIMSIHI ADOLPH DOMINGUEZ AMKARIBISHE ALLY CHOKY NA BENDI YAKE

KAMA KAWAIDA YAKE ALIINGIA KWA STAILI INGINE TOFAUTI NA YA FARASI SASA KAMA CHIFF.

CHOKY AKIKONGA NYOYO ZA WASHABIKI KWA MARA YA KWANZA CHOKY NILIMUONA AKICHEZA SANA TOFAUTI NA TULIVYOMZOEA AKAWA KAMA WERRASON

ADOLPH ALIPANDA JUKWAANI KUMSAPOTI CHOKY HATA KATIKA KUIMBA HUYU JAMAA HAKIKA NI MTU WA WATU SANA MAANA ALIKUWA AKISALIMIANA NA KILA MTU.

ONE BY ONE YA DR.CHENI YAZINDULIWA VIZURI UKUMBI WA GRM-MWENGE.

Wadau tukitazama kwa umakini zaidi movie

Dada Sharifa Kalala akitoa maoni yake kuhusu movie ya one by one

Gm wa Global publishers Abdallah Mrisho nae alitoa maoni yake

mama Dotnata kama mshiriki wa movie hiyo nae alitoa mchango wake

Mzee Yusuph Kalala na mwalimu mzuri wa Lugha ya Kiswahili ambae anaishi Washington-Marekani alisisitiza matumizi sahihi ya lugha ya kiswahili hasahasa katika majina ya movie zetu

The great pioneer nikitoa yangu ya moyoni

Swahiba nae akitoa yake ya moyoni kikubwa tulimpongeza rafiki yetu Dr.Cheni kwa kujitaidi sana

G.Makupa mkerugenzi wa GRM PRODUCTION alitoa mchango wake wa moyoni

wote kwa pamoja na dada Sharifa

Hakika ilipendeza sana na sanaa yetu yakuwa sasa

THE GREAT NA AUNTY EZECKIEL KTK KUPIGA TANGAZO LA SUNRISE BEACH KIGAMBONI

hapa ni mapozi ya baharini sunrise beach

huduma ingine inayopatikana hapo ni massage hivyo nayo tuliipigia tangazo

hapa aunty akiendelea kuonesha jinsi utamu wa massage ulivyooooooo

ilifika zamu ua The great mmmh nikalala kabisaaaaa

mapokezi kabla ya kupelekwa chumbani hupewa juice kupoza koo kama unavyoona

Juma tano iliyopita usiku wa mwafrica club bills

Twanga pepeta kama kawaida yao walikonga nyoyo

wazee wa filamu kama kawaida tuliandaa meza maalum kwa ajili ya kumkaribisha dada yetu aishie marekani washington dada Sharifa Kalala akiwa na mmewe mzee Yusuph Kalala

mzee kalala na dada sharifa wakilitizama sebene la twanga vizuri

cheni,swahiba,the great tukiwasindikiza dada sharifa na mzee kalala nje baada ya kushiba burudani ya twanga pepeta

May 26, 2010

JARIDA LA FILAMU ZA KIBONGO LAJA...KAA MKAO WA KULA.

KATIKA KUONESHA KUWA TASNIA YA FILAMU BONGO IMEKUWA SASA JARIDA KALI LIITWALO FILM LINAKUJA HIVI KARIBUNI.LITAKUWA LIKIZUNGUMZIA MAMBO YOTE YA FILAMU HAPA BONGO NA WAIGIZAJI WAKE WOTE...SI LA KUKOSA.

HIVI NDIVYO LITAKAVYOONEKANA KWA MBELE..

BABU YANGU AFARIKI DUNIA USIKU HUU...

Ni yule ambae mwanzoni mwa mwaka huu mwezi wa 3 nilikwenda kumsalimia sasa amefariki dunia'Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la MUNGU wetu libarikiwe...amen,nakumbuka siku aliponiona alilia sana na kusema 'nilidhani nitakufa bila ya kukuona tena mjukuu wangu Kanumba''sasa nimekuona hata nikifa sawa'' hatimae yametia.. hapa siku aliponiona baada ya miaka mingi sana akalia sana nilipombembeleza anyamaze tukapiga picha hii.

hapa akilia sana kama mtoto mara gafla aliponiona akisema''nilidhani nitakufa kabla ya kukuona mjukuu wangu''marehemu babu yangu enzi za uhai wake aliwai kuwa daktari mkuu katika mikoa kadhaa kama mwanza,tabora nk,pia baada ya kustaafu alipewa cheti toka kwa aliyekuwa raisi wa awamu ya pili TZ Mh Ally Hassan Mwinyi cha kutoa huduma ya afya popote pale atakapokuwepo nchini katika kustaafu kwake kazi ambayo aliifanya mpaka mauti ilipokaribia kumchukua.


The great siku nilipotua kijijini kwenda kumsalimia babu....sifa na utukufu namrudishia mweza wa yote......GEHOVA

May 24, 2010

THE GREAT NA LISA JENSEN

Leo nilikutana na Lisa Jensen kwa maongezi maalum kuhusu kazi,nimeshafanya nae movie moja ya UNFORTUNATE LOVE,na sasa chini ya KANUMBA THE GREAT FILMS tuko katika maongezi na Lisa ili apige movie yangu ingine mpya nitakayoianza hivi karibuni,tukifikia makubaliano mtamuona Lisa shooting ambae baada ya mzigo huu ataelekea India kuendelea na kazi zake za modeling. hapa nikimsimulia story ilivyo na yeye akichangia mada

akisifia story jinsi inavyoliza

akinisikiliza kwa makini mpaka sura yake ikawa inafata hisia za ninayomsimulia

nikiendelea kumpa uhondo wa hadithi ilivyo

huwa ni kawaida yangu nikishamsimulia msanii story ilivyo namuuliza ameelewaje?ndivyo nilivyofanya hapo na Lisa akinielezea jinsi alivyoelewa