Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Mar 29, 2011

HII NDIO THE SHOCK na SHAZ SADRY......SCENE ZA MWISHO MWISHO ZA THE SHOCK........

Wadau The Shock ndio inamaliziwa maliziwa location katika scene za mwisho mwisho hivyo jiandaeni kwa kuipata tayari .......verry sooooooooooooooooooooon....

Mar 16, 2011

WATOTO WA UNCLE JJ WAMTEMBELEA UNCLE JJ...

Katika pitapita wanangu waliocheza katika THIS IS IT,UNCLE JJ na DECEPTION waliamua kupita nyumbani kwangu kunitembelea kidogo,lakini pia kujua kwa mwaka huu nimewaandalia movie gani?... Umeme ukikatika basi ndani hakukaliki,kushoto ni msaidizi wangu(PA)Seth,mtoto LAUREN JOHNSON aliyecheza katika DECEPTION,anayefuata alikuja na Jenifer nayeye akiomba nafasi awe kama wenzake...nyuma yao ni Patrick..anyepiga picha mbele yao ni Jenifer.

Ikabidi Patrick aje kupiga picha ili Jenifer nae awepo kama unavyomuona katikati yao

Lauren akiwa katika pozi katika movie atakayoshoot ni mpambano kati yake na Jennifer ambapo movie itaitwa IRENE and AUNTY,Lauren ataigiza kama Aunty na baba yake ataitwa Ezeckiel,wakati JENIFER ataigiza kama IRENE na baba yake ataitwa Uwoya,katika movie hiyo wote wana ndoto za kuja kuwa waigizaji wakubwa nchini,PATRICK yeye ataigiza kama RAY KIGOSI mwenye ndoto za kuja kuwa director wa filamu nchini...

Patrick akifanya mazoezi ya sauti kama Ray.

Jenifer katika pozi,yeye ataigiza kama Irene na baba yake ataitwa Uwoya wakiwa watoto.

Baada ya kutambiana nani atamfunika mwenzake Jenifer(Irene)au Lauren(Aunty) au director Patrick(Ray)...wakapata picha ya pamoja,,,nami nikawaahidi pindi kila kitu kikiwa tayari nitawaita na kuanza mazoezi kisha kushoot ila wakati wa likizo zao bila kuadhiri masomo yao.

Mar 12, 2011

PICHA ZAIDI ZA KAOLE DAY-MAGOMENI

Bi Mwenda,Nina,Kemmy wakicheza ngoma

Kwakweli Chopa sijakuelewa bado....

Nami niliingia ulingoni....

Wana wa Kaole haooooo

Wapiga ngoma wakiwa makini

The great na Nina peke yetu ulingoni...chezea ngoma ya asili wewe..

Mzee Pembe na Kemmy peke yao ulingoni

Chopa na Rechal sijawaelewa bado ulingoni

Mboto,Bupe na Kadada sasa zamu yaoooo

Ikafika wakati wa kuimba tukapanda kuimba nyimbo tulizopenda kuimba sana katika bendi yetu ya Kaole kipindi kile,nyimbo kama Pesa position ya Franco na TP ok Jazz,Afro,Dunia tunapita,Kitambaa cheupe ya King Kiki,na Siwema.

Katika vocal nipo mimi,Chiki na MC kenyata....hakika hata mpangilio wa sauti ulikuwa ni mzuri sana japo hatujafanya mazoezi kwa mda mrefu

Johari alikuwepo,enzi zile Kaole alijulikana kwa jina la Naima au Mande kabla ya kuitwa Johari

Maya akaona akae counter kabisa asisubirie kuletewa....

PICHA ZAIDI ZA KAOLE DAY.....

Cheni akitoa mawazo yake namna ya kukiboresha kikundi chetu cha Kaole...

Hivi ndivyo tulivyokuwa tukikaa wakati wa mazoezi

Bi Star akisimama kutoa yake....utamkumbuka huyu dada katika scene za kijijini akiwa na Muhogo Mchungu ilikuwa patashika...

Mwenyekiti wa Kaole wa sasa..MR.CHIKI.

The great nikisisitiza tuendelee kuwa na KAOLE DAY na Kurudisha heshima ya kundi hili kama zamani

Bi hindu

Dr.Manyaunyau...

Rahim Khatibu(Kiuno) alikuwa location manager kipindi hicho na sasa anaendeleza kazi hiyo katika filamu

Kwa juu ni NINA,ZAWADI na BUPE..

Joyce Kiria akichukua matukio

Kulia ni Maya..enzi zile alikuwa na mwili kama wa Aunty Ezeckiel na alicheza scene kama wanazocheza sasa akina Aunty lakini sasa LOH kauwacha mwili kama Queen Latifa

Kiuno,The great na Cheni

Chopa nae alitoa yake

Ikafika wakati wa kucheza ngoma sasa,,,wote uwanjani maana enzi zile za kaole ya zamani kucheza ngoma ilikuwa ni lazima kucheza kwa kila msanii

Wote uwanjani......cheza sindimba...