Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Nov 29, 2011

CHINEDU IKEDIEZE(AKI) AFUNGA NDOA....

Msanii maarufu mfupi toka Nollywood,anayeigiza sana comedy Chenedu wa AKI na Ukwa,,jumamosi iliyopita tarehe 26 mwezi huu amefunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Nneoma Nwajah katika kanisa la St.Theresa-Imo state.The great kupitia mtandao wa BBM nilimtumia ujumbe wa kumpongeza nae akashukuru sana.


oooh Chalee congratulation my broda.....

TWANGA PEPETA WAFANYA KUFURU LONDON...KAMA KAWAIDA YAO....

UMATI WA MASHABIKI WA TWANGA LONDON ULIVYOFURIKA KUSUGUA KISIGINO....


KIBOSHO KAMA KAWAIDA KTK DRUMS

Nov 9, 2011

MUONEKANO WANGU WA SASA HIVIIIIII.....

NIENDELEE AU NIISHIE HAPO???NILIAMUA KUFANYA HIVI BAADA YA MASHABIKI WANGU WA KWELI WENYE MAPENZI YA DHATI NA MIMI KUNISHAURI KUWA NILINENEPA SANA HIVYO MWILI KUKOSA MVUTO KAMA WA AWALI WALIOUZOEA KATIKA FILAMU ZANGU LAKINI PIA HOFU YAO IKAWA KATIKA UNENE WANGU ULIOELEKEA HATA KUNILETEA KITAMBI KWA MBALI HIVYO KUHISI BAADHI YA SCENE SITOZICHEZA TENA,NDIPO KWA DHATI KABISA NIKAANZA KUFANYIA KAZI MAONI YENU KWA KUPUNGUZA KULA(DIET) MAANA HII ILIKUWA NI UGONJWA WANGU NA HAIKUWA RAHISI,LAKINI PIA NIKAANZA MAZOEZI KWA KASI JAPO NA HII NAYO HAIKUWA RAHISI MAANA UBUSY MWINGI MARA SHOOTING MARA SAFARI ILA NIKAWEKA NIA,NA LEO HAPO NDIPO NIMEFIKIA SASA JE NIISHIE HAPO?AU NIENDELEE TENA?AU NIRUDI KULE KTK UNENE??

MARA TU BAADA YA KUANZA DIET NA MAZOEZI KWA NGUVU MUONEKANO WANGU UKAWA HIVI.....

HAPA NIKISHOOT ''BECAUSE OF YOU''ILIYOTOKA HIVI KARIBUNI......
MWANZONI MWA MWAKA HUU KABLA SIJAANZA DIET NA MAZOEZI KWA NGUVU..MUONEKANO WANGU ULIKUWA HIVI....

WAKATI WA THE SHOCK...


WAKATI WA DEVIL KINGDOM....

Nov 7, 2011

BAADA YA KUTUA TU BONGO THE GREAT NA STARA THOMAS WAUNGANA NA MAMA SALMA KIKWETE KATIKA CHARITY WALK-SAIDIA WATOTO WENYE KANSA.

Matembezi yalianzia mnazi mmoja mpaka Movenpick.na kiasi cha pesa zaidi ya milioni 40 zilichangwa kusaidia watoto.The great kama balozi wa OXFAM GROW nilichangia milioni mbili na Stara milioni moja.


Nikisalimiana na mheshimiwa Zhakia Megghi


Nikisalimiana na maafande

Ilituongoza.....

Mama Salma Kikwete akifungua matembezi rasmi..

Watoto toka shule mbalimbali walikuepo.....

THE GREAT ALIVYOTEMBELEA SOKO LA FILAMU GHANA...

Nilipata muda wa kutembelea soko la filamu Ghana na kuweza kununua baadhi ya movie kwa ajili ya kutizama ila pia kuongea na mtayarishaji na msambazaji mkubwa wa filamu Ghana na mkurugenzi wa VENUS FILMS PRODUCTION,ndugu Abdul Salam.ndiye mmoja wa waasisi wa Ghallywood(Ghana movie industry).moja ya maongezi yetu ni ushirikiano wa filamu za bongo na Ghana lakini pia kutanua soko letu la filamu n.k.maongezi yalikwenda vizuri sana. The great nikichagua filamu


The great na Prince Richard Nwaobi


Kibao kinachoonesha ofisi yake.


The great,Monalisa na Abdul Salam from VENUS FILMS PRODUCTION mara baada ya kumaliza maongezi.


Monalisa nae alinisaidia kuchagua filamu....


Katika ndege nikirudi bongo


Masaa 6 angani yanachoooooshaaaaaaaaaStaa anayependwa sana kwa sasa Ghana John Dumelo,Mona,Prince Richard,kabla ya kufika Ghana nilijua anayewatingisha huku ni Van Vicker kumbe kwa sasa ni huyo kaka na Michel Majid yaani wanapendwa sana,Van Vicker hayuko sana katika movie zao na kama vile amebaki kucheza movie za Nigeria na za kwake ambazo hazifanyi vizuri sokoni Ghana.kwa tetezi nilizosikia ni kuwa alianza kuwa msumbufu hivyo maproducer na directors wakaamua kuacha kumpa kazi jambo ambalo linazidi kumshusha.

Nov 1, 2011

IN ACCRA-GHANA.......................

Monalisa kazini akiwa na CHRISS ATTOH,
Huyo dada ndiye main character uigizaji wake naufananisha na Leleti Khumalo(Sarafina) yaani anakamua ni balaa.
Kwa taarifa niliyopewa hapa huyu ndiye aliyechukua tuzo ya best cinematograph katika American cinematograph awards mwaka jana anaitwa CHASE BOWMAN mlioko huko Marekani mnaweza kunisaidia hapo.
Picha ya pamoja katika kuwaaga CHRISS na OMARY ambao wamemaliza scene zao na hapo hapo wanaelekea airport kwenda Nigeria kuanza kushoot series ya Tinsel session two.Watu wako busy na kazi hawana mda wa majungu,chuki,roho mbaya,roho ya kwanini,kupondana na kutukanana mda wote wanawaza mafanikio tu, I wish hii hali ingekuwa kwetu bongo maana hali iliyopo siku hizi imegeuka kuwa ndio utamaduni wetu.
Monalisa kazini......

Monitor...
Pusher kazini.....


MONA NA CHRISS MARA BAADA YA SCENE KUISHA.

BADO TUPO GHANA.....

Monalisa-TZ,Ommy-Ghana
Mona na baadhi ya washiriki....
The great kazini,ndani ya camera aina ya RED,ni mara ya pili sasa nashoot ktk camera hii,ya kwanza ilikuwa Nairobi wkt narekodi tangazo la Zantel ambao wao walitoka Bollywood,na sasa hawa Hollywood.Hapo naelekea mlangoni kumpokea mtu camera ikinisubiria mlangoni.
Tizama setting ya mwanga,utajua wanataka ionekane saa ngapi hapo,nikisubiri actiiiiion niingie.....
The great,Ommy na Adjeteh a.k.a Pusher ndiye winner wa tuzo ya AMAA mwaka jana kama Best Actor in suporting role...
Ki Ghana zaidi....
The great kazini......
Gari la vifaa

The great na Monalisa tukiwa na Mr.Angell,huyu ndiye anayeshikilia kile kibao kinachoandikwa scene no,take nk.
Monalisa akiwa na director wetu Bi.Yaa Boaa Aning anayeishi Los Angelos-Hollywood-Marekani,kwa miaka 8 mpaka sasa ni Assistance wa Jimmy Foxx-Hollywood.
Kwa wenye DSTV na mnaotizama tamthiliya ya TINSEL sura hiyo si ngeni kwenu ni Mr.Omary Captan,staa wa Ghana ila mara nyingi anakuwa Nigeria kwa sababu ya kurekodi TINSEL nae yumo.