Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Jun 30, 2010

Katika maisha yangu napenda sana ADVENTURE.....

Hapa The great nilitembelea maeneo ya Shaka marine yaliyopo hapa Durban(south africa)kuona baadhi ya viumbe au nyoka hatari sana tulionao Africa. huyu ni hatari

Hawa sikuwaelewa ni viumbe gani

eti niliambiwa huyu ni nyoka mpole sana...mmh?

Ulishawai kuona nyoka Albino??ndio huyo hapo joka albino na mwingine ndio original yake

Hapa mwili ulinisisimka maana sijawai ona joka nene kiasi hiki......huyu niliambiwa hujivilingisha ktk mwili wa kiumbe chochote anachoshambuliana nacho alafu anajivuta ili kuvunja mifupa ya mwili tayari anakuw3a kashaua......

Eneo lenyewe kwa nje laonekana hivi....

Hiki ni kibao kinachokukaribisha hapa SHAKA MARINE(ZULU KINGDOM)

Umaarufu hauna mipaka,hapa nilikutana na mashabiki wangu ambao ni walinzi wa hapa shaka marine wakaomba kupiga picha na mimi...nami nikaona niwape haki yao.

kama nilivyosema napenda sana adventure hii ni milima ambayo imekuwa ni kivutio kikubwa sana kwangu hapa ni nje ya mji wa durban.


hapa utadhani uko juu ya ndege maana nyumba zinaonekana ndogo sana pamoja na gari..kama una roho ndogo kizunguzungu lazima ukipate.

Hivi ndivyo uumbaji wa Mungu ulivyo...hakuna kama yeye.

Jun 26, 2010

THE GREAT NDANI YA AFRICA KUSINI...

SAMAHANI JAMANI KWA KUTOWAAGA,NIKO SOUTH AFRICA KIDOGO KATIKA SHUGHULI ZANGU ZA HAPA NA PALE HIVYO SIJAPATA MDA WA KUWAHABARISHA MAMBO ILA NIKIPATA NAFASI NITAFANYA HIVYO PAMOJA NA PICHA...JANA NILIKUWA JOHANNESBURG NA LEO NIKO DURBAN NA NTAKAA KWA SIKU KADHAA KABLA SIJAELEKEA JOHANNESBURG TENA.CHEERS.

Jun 24, 2010

ZIARA YA THE GREAT BURUNDI-BUJUMBURA

NIKITOKEA AIR PORT NILIKUWA NIKIKUTANA NA MASHABIKI WANGU NAMNA HII

HAPO NAITWA UNCLE JJ JINA NILILOTUMIA KTK THIS IS IT

WAKATI FULANI ILIBIDI KUSIMAMISHA GARI ILI NIONGEE NA BAADHI YA MASHABIKI HUYU BABA ALIKODI TAX IKIMBIZE GARI NILILOPO ILI ANISALIMIE

WATOTO NDIO MASHABIKI WANGU WAKUBWA SANA DUNIA NZIMA HAKIKA NAJIVUNIA HILI HAPO NAULIZIWA WAPI JENIFA MTOTO ALIYECHEZA THIS IS IT..

HII NDIO HOTEL NILIPOFIKIA

THE GREAT NIKIINGIA UKUMBINI TAYARI KWA KUKONGA NYOYO ZA MASHABIKI WALIOKUWA WAKINISUBIRIA KWA HAMU

STEVE KANUMBA LLLLLLLLIVEEEE

THE GREAT STEJINI NIKIDHIHIRISHA KUWA SI KTT CAMERA TU HATA LIVE HUWA NIKO MAKINI

SEHEMU MOJAWAPO YA UMATI WA WATU ULIOFURIKA KUMUONA THE GREAT NA IRENE UWOYA

THE GREAT NA UWOYA LIVE STEJINI TUKIPAFORM BAADHI YA VIPANDE VYA FILAMU YA OPRAH AMBAYO INAPENDWA SANA HUKU...MFANO KILE KIPANDE CHA AAH CHURA..

HAPO NILITIA NJAA YANGU STEJINI MPAKA IRENE AKASHINDWA KUJIZUIA IKABIDI ACHEKE MPAKA AKAKAA CHINI KABISA

NYUMA YA STEJI ILIKUWA NI KUPIGA PICHA NA MASHABIKI

THE GREAT KAZINI..HAPO NILISHIRIKISHA BAADHI YA WAIGIZAJI WACHANGA WA BURUNDI PAMOJA NA MIMI HAKIKA WALIFURAI SANA KU ACT LIVE NA MIMI.

THE GREAT NA IRENE UWOYA MARA BAADA YA SHOW TULIALIKWA NA MHESHIMIWA FULANI JINA KAPUNI TUKAPATE MAKULAJI

THE GREAT NA SHEMEJI HAMAD NDIKUMANA KATAUTI MME WA IRENE UWOYA NAE ALIKUEPO

Jun 22, 2010

HAPO VIPI??THEGREAT KAZINI..AHAHAH MORE THAN PAIN

NIKIKIPENDEZESHA KIATU ILI MTEJA WANGU ANG¨¨AAE BWANA

WASHKAJI WAMEPITA KUNITEMBELEA KIJIWENI

Jun 21, 2010

MY DIRECTOR FEMI OGEDEGBE NA MTOTO WAKE SHARON OGEDEGBE

CONGRATULATION MY BROH....NICE... DIRECTOR WANGU WA MOVIE KAMA DAR TO LAGOS,MY SISTER,CROSS MY SIN,UNFORTUNATE LOVE,RIPLE OF TEARS,THE DIRECTOR,NA HERO OF THE CHURCH..OLUFEMI OGEDEGBE AKIWA NA MWANAE SHARON......

Jun 19, 2010

THE GREAT NA IRENE UWOYA NDANI YA BUJUMBURA(BURUNDI)

SAMAHANI JAMANI NILIONDOKA BILA KUWAAGA KIFUPI MIMI NA MSANII MWENZANGU IRENE UWOYA(OPRAH)KAMA ANAVYOITWA HUKU BURUNDI TUKO HUKU BURUNDI KWA MWALIKO MAALUM WA MAONESHO MAWILI YAANI LEO JUMAMOSI KTK UKUMBI WA BAMBULA NA KESHO JUMAPILI.NIKIPATA MDA NITAWAWEKEA PICHA NA HABARI YA YANAYOJILI HUKU.

Jun 18, 2010

THE GREAT NA WANANGU WA THIS IS IT...

patrick akiwa kazini katika more than pain kafanya makubwa katika this is it na sasa humu yumo

Nikiangalia rehasal yao

Patrique kazini

akiwa na uncle wake JJ.

Jenifa nae kanitembelea location kuona kazi ninayofanya na kaka yake patrick,nae namuandalia yake baada ya kuvunja rekodi katika This is it.

Jenifa na uncle jj

Ntamleta kwenu tena na kitu kingine hakika huyu mtoto kafanya kazi katika This is it hapa alinitembelea location ninaposhoot MORE THAN PAIN.

Jun 15, 2010

THE GREAT KAZINI...''MORE THAN PAIN''

KAZI KAZI NI KAZI NYUMA YANGU KUNA MASHABIKI WANGU AMBAO KWAO KUNIONA LIVE NIKISHOOT ILIKUWA KAMA SURPRISE SIMU ZAO ZIKAWA CAMERA

AAH MWANAUMEEEE

WANAUME TUMEUMBWA MATESO,KUHANGAIKA

POZI LA KAZI

NIKIPOKEA POSHO YANGU BAADA YA KAZI YA ZEGE KUMALIZA

NIKIJISAFISHA NIRUDI KATIKA HALI YA KIBINADAMU

BAADA YA KAZI NI CHAKULA...WALI,NYAMA,MAHARAGE NA MCHICHA...

Jun 12, 2010

THE GREAT NA LISA JENSEN KATIKA SCENE ZA SHULENI NDANI YA ''MORE THAN PAIN''

Wanafunzi haoooooooo

Hili kosa sijui tutali solve vipi?

Lisa akiwaza mbona tumetolewa gafla darasani?bila shaka ndio nafukuzwa shule...

Vijana wangu wa kazi toka GRM PRODUCTION wakiandaa vifaa tayari kwa shooting

Back shot..

Lusubiro na Hamidu wakiitendea haki stead cam yaani camera ya kuvaa kifuani ii uweze kutembea nayo

Headmaster akitoa speech kali..

Wakati fulani huwa naisaidia crew yangu kama unavyoona maana production huitaji ushirikiano wa dhati ili kazi iwe bora zaidi

Tukisoma matokeo hapo ni Seth,Tino na mimi

Lisa akitoloka shule kwenda kwa.....


mmmmh mapenzi shuleniiiii ni hatari..

kwa pamojaaa wanafunziii

Darasani Tino ndie anayeongoza kwa kupiga kelele na utundu.....

muda wa kantini huu kila mwanafunzi anatabasamu saana