Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Oct 30, 2010

UNCLE JJ MDA WOWOTE ITAKUWA MTAANI..KAENI TAYARI

HAPPY BIRTHDAY ZENA..

The great na Zena katika sherehe yake kariakoo

Tabasamu

Maya na Zena

Zawadi za mtoto aliyezaliwa leo..

Oct 28, 2010

HAPPY BIRTHDAY AUNTY EZECKIEL

Leo ni siku ya kuzaliwa dada yetu na msanii mwenzetu maarufu wa filamu Aunty Ezeckiel Gwantwa Greyson Jujuman.The great na blog hii inakutakia maisha mema na marefu uzidi kuongoza vyema kampuni yako ya Cream entertainment na Pub yako ya Cream pub. Aunty katika pozi

Aunty na The great katika mojawapo ya scene katika shooting..

Oct 27, 2010

REGGAE CONCERT

HALLOWEEN GROOVE CRUISE

Oct 25, 2010

GUESS WHAT????????????

Kuna nini hapa wadau? Uwoya

The swahiba's with Uwoya

Kanumba&Uwoya

Swahiba&Uwoya

Uwoya&The great pioneer

Oct 22, 2010

URBAN PULSE CREATIVE WAIVAMIA SPORAH SHOWKutoka kushoto ni Mzee wa nyuki Frank Eyembe,Mdau,Sporah na Baraka baraka

Pose la kumsubiri Diamond

Oct 20, 2010

KEVIN WA NIGERIA ATUA BONGO KUKAMILISHA MIPANGO YA HARUSI YAKE NA ELIZABETH GUPTA

Mshindi wa Big brother revolution mwaka jana KEVIN CHUWANG akiwa na familia yake ametua hapa bongo kwa ajili ya kutoa mahali ya dada yetu Elizabeth tayari kwa maandalizi ya harusi yao itakayofanyika mwezi wa pili mwakani.Katika moja ya vikao vyake hapa Dar Kevin aliniita ili kushauriana mambo kadha wa kadha juu ya harusi yao lakini pia juu ya project zake anazotarajia kufanya Africa mashariki.Binafsi nilianza kujuana na Kevin katika jumba la big brother revolution mwaka jana ambapo mimi nilikuwa humo kama star mwalikwa tu,wakati naondoka katika jumba hilo baadhi ya housemate kama Hannington,Leonel nk waliniomba nguo zangu lakini Kevin yeye aliomba nimpatie jina la The great,nami nilimwita Kevin The great nikimwambia kuwa atakuwa the great wa jumba hilo,hatimae alishinda na kuzidi kuwasiliana nami. The great nikisalimiana na Kevin

Kevin akinikaribisha nikae

Kevin,The great na Eliza

Ndugu baadhi wa Kevin.

Kulikuwa na sahani ya kiti moto kwa kwenda mbele

Nani anakutumia msg hapa na mimi niko hapa??

Story za hapa na pale

Oct 17, 2010

THE GREAT AWATEMBELEA WASHIRIKI WA KILI BONGO STAR SEARCH KATIKA JUMBA LAO.

Leo nilipata mwaliko wa kutembelea jumba la kili bongo star search kuongea na washiriki wa humo ambao walinikaribisha vizuri kwa nyimbo na chakula na kunitembeza sehemu mbalimbali za jumba hilo lililojaa camera kila upande zikirekodi kila kitu na kila wakati ikirusha live mfano wa Big brother house..Nashukuru sana waandaaji wa KILI BONGO STAR SEARCH HOUSE kwa heshima hii nzuri mliyonipatia. Bango la jumba

Kushoto ni producer wa kipindi hicho na kulia ni fundi mitambo wa kipindi hicho MR.Keppy ambaye pia ni mpiga bass guitar wa njenje

Nilipokelewa na Evelyn msimamizi mkuu wa kipindi hicho

Jumba linavyoonekana kwa mbali

Evelyn akinipa maelekezo kabla ya kuingia jumbani nikiwa karibu na mlango wa kuingia tayari kuwa liveeeeeeeeeee

Baada ya kuingia mlangoni nilipokelewa na mother house bi Natasha na kunipeleka kwa washiriki wa BSS

Chumba cha mitambo

The great ninavyoonekana katika monitor za mitamboni mara baada ya kujumuika na washiriki wa kili bss ambao walinikaribisha kwa chakula huku tukipiga stori za hapa na pale

Washiriki wa BSS

Mswali na majibu

Picha ya pamoja na washiriki ndani ya jumba

Mother house akifurahia ujio wangu ndani ya jumba

Evelyn akinirekebishia mic kabla ya kuingia mjengoni ili kila ntakachoongea kisikike vizuri mwishoni kabla ya kutoka niliwatakia washiriki kila kheri na kuwashukuru kwa ukarimu wao.

EUROPEAN FILM FESTIVAL ILIVYOFANA DAR ES SALAAM

Tamasha la film la EFF lililofanyika juzi lilifana vilivyo ambapo watu mbalimbali mashuhuri ndani na nje ya nchi walikuepo...zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio ya siku hiyo. Tayana na mdau akimuuliza mawili matatu

Logo yenyewe ya tamasha ilivyokuwaSlyvia shally na Wastara nao walikuepo

The great na MC.George wa Global publisher tulikuepo

Sajuki,MC George na The great

mmmh The great na Wastara

Slyvia na Sajuki katika picha ya pamoja

RADIO FRANCE INTERNATIONAL YAMTEMBELEA THE GREAT

Radio ya kimataifa iliyopo hapa Dar es salaam na makao makuu yake Ufaransa ilinitembelea kunihoji mambo kadha wa kadha juu ya maisha yangu na sanaa yangu kwa ujumla, The great nikihojiwa na mtangazaji wa radio hiyo MR.EDMOND

Hapo kabla ya kuanza kunihoji alianza mwenyewe utangulizi akisema hii ni radio France internationale ambayo leo imemtembelea Steve Kanumba The great msanii wa filamu.......

Mr.Edmond kabla ya kuanza alinipa utambulisho wake kwa kunipa bussiness card yake ili kunihakikishia kuwa nimetembelewa na mtu makini kabisa aliyetumwa kazi moja tu ya kunihoji maswali ya mashabiki

Akipitia script ya maswali yake kuhakikisha kama kila swali alilopanga kunihoji kaniuliza na hajabakisha.Asante sana Radio France internationale(RFI) karibuni tena na tena