Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Jul 27, 2010

Nimekifyatua jamani..

Sasa Filamu ya YOUNG BILLIONAIRE ipo mtaani
Pata nakala yako katika DVD, VCD na VHS mahala popote pale penye maduka ya kuuzia kanda zetu hapa Nchini. Akhsanteni kwa ushirikiano.

PILIPILI ENTERTAINMENT WAISHEHEREKEA TUZO YAO YA ZIFF

FURAHA WALIYOIPATA KAMPUNI HII KWA MOVIE YAO YA NANI?KUCHUKUA TUZO YA FILAMU BORA YA BONGO NA MSANII MONALISA KUWA MUIGIZAJI BORA TOKA KATIKA MOVIE YAO YA BLACK SUNDAY,KAMPUNI HII ILIFANYA SHEREHE AMBAYO MASTAA MBALIMBALI WA MOVIE WALIALIKWA NIKIWEMO MIMI.KAMA UNAVYOONA CHINI HAPA


Jul 23, 2010

HAKIKA UKIONA MOVIE HII HUTOAMINI KAMA NI MIMI NIMECHEZA..... NI CRAZY LOVE

Movie hii hata mimi mwenyewe japo nimecheza lakini naipenda sana na naisubiria kwa hamu,ni moja kati ya movie ngumu nilizowai kucheza na nikamudu sawia,itakuwa mtaani mwezi ujao (wa nane)Movie hii ilinifanya kwa mda wa mwezi mzima kusoma vitabu mbalimbali vya wasomi na watu mashuhuri duniani kama PLATO,KARL MAX,ALEXANDER THE GREAT,SAMUEL TAYLOR nk,Ilinibidi kuwa karibu sana na waalimu wakubwa wa vyuo vikuu ili kujua tabia zao.TAFADHALI SI YA KUKOSA,PATA NAKALA YAKO ORIGINAL,,MOVIE HII IKITOKA NAOMBA MNIAMBIE KWA KUNITUMIA E MAIL MBALI NA MIMI HAPA BONGO NI MSANII GANI WA FILAMU HAPA AMBAYE ANGEWEZA KUCHEZA UHUSIKA HUO?NINA UHAKIKA MAJIBU YATAKUWA HAKUNA....AHAHAHAH SWAHIBA UPO?
Hapa kila mtu alisema ama kweli The great ni zaidi ya msanii

Sina utani kabisa niko kazini

The great na Hemedy ndani ya CRAZY LOVE

HII NDIO HALI HALISI YA BOMU LILILOLIPUKA KAMPALA-UGANDA HIVI JUZI.

TUZIDI KUMUOMBA SANA MUNGU.WAPO WALIOPOTEZA MAISHA YAO BILA SABABU...MWENZAKO AKINYOLEWA ZAKO TIA MAJI JAMANI TUITUNZE AMANI YETU CHUKI ZA NINI?

Jul 19, 2010

TUZO ZA ZIFF MONALISA NDIYE MUIGIZAJI BORA.

Kupitia movie ya BLACK SUNDAY toka Pilipili entertainment co. ltd Dada yetu na mkongwe wa sanaa ya filamu nchini Yvonn Cherry(MONALISA) amepata tuzo ya muigizaji bora katika filamu za kiswahili hapa nyumbani.Movie hii ambayo tumecheza wote na Monalisa bado haijaingia sokoni ila ni filamu nzuri na Monalisa kacheza vizuri sana.The great na blog hii twakupa hongera sana hakika ni haki yako upate,Monalisa ameidedicate tuzo hiyo kwa watoto wake wawili na mama yake mzazi bi.Suzan Lewis(NATASHA) huku akiongea kwa furaha ''nawapenda sana'' Akionesha tuzo yake juu mara tu baada ya kukabithiwa

Kidumu,The great,Slyvia na Swahiba tulikuwa tumekaa tukishuhudia msanii mwenzetu akipokea tuzo yake

Akiwa na tuzo yake toka ZIFF

The great nilimfata kumpa hongera maana nae huwa mstari wa mbele kunipa moyo na pongezi pindi ninapofanya jambo la heri

Swahiba nae alimpa pongezi kwa hatua hii.

TAMASHA LA ZIFF LAISHA,MSANII KIDUMU AVUNJA REKODI

Kama tulivyopewa nafasi ya kipekee kuongea machache wakati wa ufunguzi wa tamasha hili la kimataifa ndivyo tumepata fursa ya pekee kuongea machache wakati wa kufunga tamasha hili la ZIFF,Wasanii tuliitwa mbele na kusema machache jinsi tulivyofurahishwa na tamasha la mwaka huu maana limetukumbuka wasanii wa nyumbani tofauti na matamasha ya nyuma,lakini pia kuweka siku maalum kwa ajili ya filamu za nyumbani na kuzipa tuzo

Toka tamasha lianze The great nilikuepo hadi mwisho wake nimeshuhudia wasanii mbalimbali wa mziki wakitumbuiza vizuri ila kwa msanii KIDUMU toka Kenya kavunja rekodi kwa burudani hakika alikonga nyoyo zetu.

Msanii Ray wa zanzibar na mkewe walikuepo

KIDUMU akipiga drum na kuimba hakika jamaa anaweza hasa kwa live..hatari

Hapa aliacha drum akaja mbele na vijiti vya drum akipiga huku akiimba wimbo wa SITOPENDA TENA

Joyce kiria na Monalisa wakicheza mziki uliokuwa ukipigwa na KIDUMU,Wakisaidiwa na mashabiki wengine.

Picha ya pamoja mimi,mzee chilo,swahiba na mdau

Hata mimi nilishindwa kujizuia ikabidi nicheze tu jamani..

Hii ni suruali yangu niliyovaa siku hii na naipenda sana.

WASANII WA FILAMU WALIVYOONGEA NA JOPO LA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU ZIFF.

WASANII KANUMBA,RAY,BABA HAJI,NA MONALISA WAONGEA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU KUSHIRIKI KWAO ZIFF NA SIKU YA SWAHILI FILM DAY AMBAPO JANA FILAM ZA KISWAHILI ZILIKUWA ZIKIONESHWA,ZANZIBAR KATIKA HOUSE OF WONDER NA MALAIKA HOUSE. KUTOKA KUSHOTO NI RAY,KANUMBA,BABA HAJI,MONALISA NA PROGRAM MANAGER WA ZIFF NDG DANNY.HAPO KILA MSANII ALIONGEA JUU YA FURAHA YAKE KUWEPO KWA SIKU MAALUM YA SIKU YA FILAMU ZA KISWAHILI KATIKA ZIFF.

WAANDISHI WAKIZIDI KUONGEA NA MOVIE STAR WA BONGO

MKURUGENZI WA PILIPILI ENTERTAINMENT MR.SAMEER SRIVASTA NAE ALIONGEA NA WAANDISHI MAANA NAE KUPITIA KAMPUNI YAKE WALIWAKILISHA FILAMU 6 ZA KISWAHILI AMBAPO MOJAWAPO IITWAYO (NANI)IMECHUKUA TUZO YA FILAMU BORA YA NYUMBANI.

Jul 14, 2010

STEVE KANUMBA NA RAY WAKUTANA NA MHESHIMIWA MAMA SHADIA KARUME(FIRST LADY)

Mimi na swahiba tumepata nafasi ya kukutana na kuongea machache na mke wa raisi wa Zanzibar mama Shadia Karume hapahapa Zanzibar. Akitupongeza kwa kazi zetu na jitihada zetu katika tasnia hii ya filamu.

Hakika nimefurai kuwaona..

Pia tuliendelea kuwaona na kusalimiana na waheshimiwa wengine.

Wakati wa kutoka sikutaka kuwabania mashabiki wangu hivyo niliwapa nafasi ya kupiga picha na mimi kama kumbukumbu yao

STEVE KANUMBA NA RAY TWATEMBELEA SHULE YA SECONDARY YA JANG'OMBE ZANZIBAR

Tumepata wakati mwingine wa kutembelea shule hii tukiwa tumeambatana na mwalimu wa sanaa ya film toka UK(jina kapuni) aliyewai kuwafundisha wanafunzi hawa sanaa ya uigizaji kabla hajaondokana kurudi tena leo kwa ajili ya kuwapa zawadi zao wana funzi hao waliofuzu vizuri. Kutoka kushoto ni Joyce Kiria,Gervas kassiga,Kanumba,Ray,Headmaster wa shule hii na mgeni wetu toka UK.

Wanafunzi waliopata mafunzo hayo

Mwanafunzi kiongozi akipokea zawadi kwa niaba ya darasa

Zawadi mbalimbali vikiwemo na vitabu vya shule

The great nilipata nafasi ya kuongea machache kwa wanafunzi na kuwapa moyo kwani hata sisi tulianza hivyo hivyo mpaka ndoto zetu zilipotimia

Picha ya pamoja na wanafunziWasanii na head master....kutoka kushoto ray,joyce,headmaster,monalisa,cloud na mimi.

THE GREAT KATIKA KAZI ZA KIJAMII ZANZIBAR.

Jina la shule nimesahau kidogo ila hii ni moja ya shule tuliyoitembelea na kuongea na wanafunzi ambao walikuwa wanatusubiri kwa hamu ili kuongea na sisi lakini pia walikuwa na maswali yao ambayo tuliwajibu kwa ufasaha. wakitusikiliza

Tukiwa mbele yao wakihoji maswali na kuelezea furaha yao kuonana nasisi live

The great nikijibu maswali yao ambayo mengi yalikuwa yakihusu film yangu ya THIS IS IT...unce jj na Jenifa.

Picha ya pamoja na wanafunzi

Monalisa akisaini autograph..

The great pioneer nikisaini Autograph ya mwanafunzi huyu aliyeniomba nifanye hivyo