Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Jan 29, 2010

Misri yafanya Kufuru, yaikongomeka 4'Oclock Algeria.


Timu ya mafarao wa Misri imemalizia mzunguko wa nusu Fainali kwa Kuibamiza timu yenye upinzani wa jadi ya Algeria kwa jumla ya Mabao yasiyopunfua 4 magoli yaliyowekwa kimiani na Hosni Abd Rabou, Mohamed Zidan, Mohamed Abdelshafi na Gedo.

Hivyo basi timu ya Misri na Ghana zitakutana katika mchezo wa fainali utakaofanyika siku ya jumapili ya tarehe 31 mwezi huu Luanda.

....Fainali zijazo Tanzania lazima tutinge FAINALI, Amini, Usiamini. wadhungu wanasema, "From zero to Hero".

Jan 28, 2010

Kombe la Mataifa ya Africa... Nigeria Kinbonde kwa Ghana
Timu ya Taifa ya Ghana imefanikiwa kuifunga timu ya taifa y a Nigeria katika hatua ya Nusu Fainali kwa jumla ya Bao moja kwa bila na kutinga fainali.
Kama ni mpira aiseee, nigeria wamejitahidi kwa kadri ya Uwezo wao lakini Peter Odemwingie alionekana kupoteza nafasi nyingi za wazi pamoja na mwenzie Obafeni Martins

Hata hivyo baada ya mpambano kuisha Kocha wa Ghana Milovan Rajevic alijitambia kwa kuwaambia wachezaji wake awali kwamba, "Leo hatuendi kucheza kandanda la kuvutia, bali tunaenda kucheza kwa ajili ya matokeo". na kweli wamepata matokeo mazuri ya kuingia Fainali.

Jan 27, 2010

Behind the scene (Point of No Return)


Lameck katika pozi la kichawi

Hii ni katika family Tears


Wachawi wakijiandaa kwenda kuroga

Jan 23, 2010

Swahiba wangu TINO aja na Movie mpya (WILLY WOODS)


Swahiba hapa akiwa mkao wa kula


Jamani huyu Sio yule wa Marekani (Tiger Woods)


...Nadhani mtakuwa mshamtambua. Hapa akiwa katika moja ya Scene katika Viwanja vya Golf
..muendelezo wa scene katika filamu ya Willy Woods

...hapa akiwa kwa hawara. oooooooh hoooo sio kiukwelikweli ni kimovie-movie.

Swahiba anaanda movie yake hiyo mpya, mpaka hivi sasa scene karibia zote zimeshamalizika na sasa nadhani kazi itakuwa imebaki kwa watu wa studio katika kuchanganya picha.... kwako mdau, Mnamuona swahiba?
Jan 22, 2010

Behind the Scene (VILLAGE PASTOR)


Njaa inauma jamani,...... Samahanini nilisahau,..
karibuni tule.... no ... tusonge Ugali.

Jamani kushoot si  mchezo.


Hata wazungu nao wanakula kumbe mihogo...!!!


Huyu mbuzi hafundishiki hajui hata ACTION!!


Msinisemeeeeh, msinisemeee..... msiniseme kama napenda kula..
Scene ya kula jamani, Director alijuta kwanini alinipa hii Scene.


Hawa mbuzi walimtesa sana huyu mzungu mpaka akasema, "Siji tena kuigiza na mbuzi wa Kiswahili kama hawa"..ha ha ha hah haaaa!


Hapa nilikuwa na njaa hatari, na mbuzi hawasikii action wala Cut toka kwa Director, walinitesa haoo!!Jan 21, 2010

Jamani Mshika Dau mwenzetu nae kafungua Blog yake...


Dada vaileth Mhinga ambaye ana saluni yake maeneo ya Gongo la Mboto amefungua Blog yake ambayo itakuwa inaelezea masuala ya urembo na maisha mbalimbali ya akina dada katika masuala ya urembo. Tushirikiane katika kuangalia mambo yahusuyo urembo hasa akina dada... Kazi kwenu!
tunaweza kumpata kupitia anwani ifuatayo:

http://beautytouchdar.blogspot.com

Jan 19, 2010

Some of the Behind the Scene (Family Tears)


Briton and Charles


Asteria and Charles


Asteria and Briton in one of the Scene

Siku Designer wangu wa ukweli Masoud Bitebo alipouaga ukapela na kujichukulia jiko Bi. Zabibu. The Great nakupa pongezi nyingi sana ipo siku na mimi "NITAKUJIBU" haaa ha ha ha...
Mr & Mrs Masoud BiteboMasoud Bitebo akiwa amelikumbatia jiko lake
Msosi, msosi, msosiiiiiiii!

Abdalah bitebo, Kaka yake Masoud Bitebo akisalimia waalikwa.

Huyu jamaa ni Mdau Mkubwa wa Man UTD, hivyo hata Keki yake ilikua ni nembo Man UTD. Wapenzi wa Manchester Mpo hapo!!!Hapa mi Chichemi....


Wazazi wa Masoud bitebo wakiwa wanafuatilia matukio kwa umakini zaidi.

Waaaana mere meta!! wanameremetaaaaaa!! Kulia kabisa mwa picha namuona Mdau mkubwa wa Koffi Olomide Mr. Shamiri a.k.a JJ "FULAMAMBO"

Jan 16, 2010

Vijana wa JK, Siku tulipotua Zanzibar kwa ajili ya kushoot O'prah 2008


(Kutoka kushoto: Irene Uwoya, The Great, Mayasa Mrisho"katikati", Swahiba na Aunt Ezekiel)Genevieve Nnaji mpinzani wa Omotola Jalade NOLLYWOOD.


Genevieve katika pozi ni mmoja wa waigizaji mashuhuri Nigeria mwenye tuzo kadhaa za uigizaji na ambaye ameshafanya kazi nyingi za filamu ndani na nje ya Nigeria Mfano. Uingereza, South africa, Ghana  n.k. Ameshacheza Filamu zaidi ya 300 na ndiye mpinzani mkuu wa Omotola Jalade katika Filamu nchini NIgeria. Genevieve ana Mtoto 1 anayeitwa Julieth. Haya dada zetu Nyumbani..........

---------kuna hata mmoja ambaye ameshafikisha hata Filamu 50 wakati Genevieve ana zaidi ya 300!!??

Irene Uwoya, Aunt ezekiel Mpo hapo?

Hii ni moja ya filamu aliyowahi kuact na ikazua maneno mengi sana Nigeria hata katika vyombo mbalimbali vya habari kama ilivyokua hapa kwetu mara mimi,swahiba na Irene Uwoya tulipotoa filam ya OPRAH.Omotola ameolewa na MR.EKEHINDE na ana watoto wanne.

Hii ndio cover ya albam yake ya nyimbo....

mapoooozi

Omotola au ukipenda muite OMOSEXY kama alivyoandika katika gari lake.