Juzi maeneo ya magomeni mikumi kulikuwa ni KAOLE DAY wasanii wote wa kaole wa zamani na wa sasa na wote waliowahi kuwa katika kundi hili tulijumuika pamoja kukumbuka mazuri yote ya kikundi chetu kilichotutoa kisanii,tukikienzi na kuhakikisha Kaole inadumu milele.Mastaa wengi wa filamu na tamthilia tumeanzia hapa,ni kundi lililoanza mnamo mwaka 1999,chini ya mkurugenzi na mwasisi Mr.Chrissant Mhengga,Lilipewa jina kaole ikiwa ina maana nenda kaone,Mpaka sasa kaole ina zaidi ya miaka 11 wakati vikundi vingine vimeshakufa lakini Kaole ipo na kimekuwa kama chuo cha mafunzo kwa wasanii wengi,Kina zaidi ya tamthilia 15 ambazo zimeshaonekana katika tv mbalimbali(ITV&TBC) kama HUJAFA HUJAUMBIKA,FUKUTO,JAHAZI,DIRA,TETEMO,TUFANI,SAYARI,BARAGUMU,GHARIKA,TASWIRA,ZIZIMO nk.Baadhi ya wasanii tulioanzia kaole ni,KANUMBA,RAY,MUHOGO MCHUNGU,KIPEMBA,CHENI,MTUNISI,FRANK,NINA,NANA,NORAH,SINTA,KIBAKULI,NYAMA YAO,BI STAR,BI TERRY,MZEE PWAGU,MZEE KIPARA,MAMA HAMBILIKI,MAX,ZEMBWELA,BAMBO,KINGWENDU,KEMMY,BENY,SWEBE,JERRY,CHUZ,MASHAKA,KISSA,AIKA,LIGHT,JOHARI,MAINDA,TEA,MAYA,SAJUKI,DINO,MZEE PEMBE,SENGA,TITO,MBOTO,KEVIN,ZAWADI,BAHATI.BUPE,BI MWENDA,BI KIDIDE,....nk.
Director wetu Chrissant Mhenga na Kemmy kabla ya kuingia katika ukumbi wa mazoezi
Chrissant Mhenga akitoa mawaidha yake ambapo wasanii wengi tulifurai kumuona tena mahali hapa,hakika alitufundisha mengi sana katika sanaa,tulimshukuru sana na tutazidi kufanya hivyo.
Director wetu Chrissant Mhenga na Kemmy kabla ya kuingia katika ukumbi wa mazoezi






























































