Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Jul 21, 2011

NAOMBA TUCHANGIE WADAU JE? POMBE NI DHAMBI?

Niliamua kumtembelea rafiki yangu baba PAROKO Maganga wa kanisa la SINZA kufafanuliwa kuhusu pombe,niliamua kufanya hivyo kutokana kuwa na kauli tofauti toka kwa watu kuhusu pombe,wapo wanaosema pombe ni dhambi,wapo wanaosema unywaji wa pombe kupindukia ni dhambi,wapo waosema pombe ni haramu,lakini yapo madhehebu ya dini ambayo yanaruhusu unywaji wa pombe na yapo yanayokemea kabisa hata kugusa,na wote hao hutoa mistari toka katika Biblia takatifu kama kidhibitisho,Hii haimanishi mimi ni mnywaji wa pombe lakini ebu tujadili hili toka katika maisha yetu ya kila siku,toka katika maandiko ya vitabu vya dini lakini pia toka kwa wanafalsafa mbalimbali duniani na viongozi wetu.Katika utafiti wa kwanza niliofanya toka kwa Paroko yeye alisema....''''Pombe ni kama kisu,ukikichukua kisu kukatia nyanya na vitunguu kisha ukapika chakula watu wakala hapo kisu ni kizuri,....ILA ..ukichukua kisu hicho hicho na kwenda kumchoma mtu na kumjeruhi hapo kisu ni kibaya,hivyo basi hata pombe ukinywa na kwenda kufanya yasiyofaa hapo ni mbaya kwako lakini ukinywa na bila kufanya mabaya hapo si mbaya hivyo inategemea na unavyoitumia yenyewe haina ubaya.'''''Jamani wanywaji na msiowanywaji ebu tuchangie hapa............... Nikiwa ofisini kwake akinielekeza mambo mengi kuhusu Dunia


Mimi huwa napenda sana kudadisi kwa kuuliza maswali hapo nikiuliza swali?


Akinifafanulia jambo kwa umakini zaidi


Ukiwa katika ofisi za watumishi wa Mungu mda wote unajihisi kutakasika...


Baada ya maongezi alinisindikiza na tukapata picha ya pamoja


Hakika nilijifunza mengi sana hivyo nikawa nimeongeza vitu kichwani ila kwa leo tu naomba tujadili kuhusu POMBE...

39 comments:

Msimbe said...

KAKA HUKUENDA KUDADISI NATIA SHAKA ULIENDA KUUNGAMANA NI ILE SINEMA YA SHETANI INAANZA KUKUPA MALUELUE NINI

Anonymous said...

KWA UJUMLA KTK MAANDIKO HAKUNA MSTARI AU SEHEMU ILIYORUHUSU POMBE SIZANI KWAMBA BIBLIA INARUHUSU POMBE NI SISI WANADAMU TU NDIO TUNATAKA KUFANYA POMBE NI HALALI LAKINI MIMI NINAVYOJUA POMBE NI POMBE HAKUNA CHA KUSEMA UKINYWA KIDOGO NZURI SIO DHAMBI NI UONGO HAKUNA DHAMBI NDOGO NA KUBWA KATIKA BIBLIA HAKUNA MAHALI ILIYOANDIKWA KURUHUSU POMBE HIYO TUSIDANGANYANE

Anonymous said...

mimi nnavyojuwa katika quran tukufu inasema kwamba pombe aramu tena sana tena sana ifanyie kabisa ata kugusa chupa yake ata kufanya kazi katika kiwada ni dhabi kubwa sana kwa mungu walai

Anonymous said...

kiukweli pombe ni haramu na haifai kabisa kutumia hakuna andiko lolote si katika BIBLIA ama QURAN linaloonesha juu ya uhalali wa kutumia pombe hivyo ni haramu na ni dhambi kubwa. tusijihalalishie kitu kwa matakwa ya nafsi zetu. itoshe kua mungu ameikataza. na ALLAH anasema tusiziue nafsi kwa mikono yetu.

Hebu jiulize ewe ndugu yangu ni kiasi gani cha fedha unatumia kwa ajili ya pombe kwa wiki?

Ni faida gani unaipata kwa unywaji wa pombe?

Hivi ni madhara mangapi tunayapata kwa ajili ya matumizi ya pombe?

Kwanini usitumie fedha kuwapatia mayatima, maskini, au wagonjwa wasiojiweza?

Anonymous said...

Wewe unayesema kwenye Biblia hakuna mstari au sehemu inayoruhusu pombe, ni Biblia gani hiyo unayosoma? Kwani pale harusi ya Kana Yesu alipobadilisha Maji kuwa divai...ilikuwa nini hile?

Biblia inakuambia fanya kila kitu kwa kiasi, kula kwa kiasi, kunywa kwa kiasi etc.

Anonymous said...

me navyojua brother pombe ni mbaya hata km unywe kidogo hta nyingi,familia nyingi zimevunjika kwa unywaji wa pombe.baadhi ya watu hasa wanaume wakinywa pombe wanaishia kufanya uovu km kupiga watu,kubaka,kufanya ngono zembe,wengine hawaachi hela home wanaenda kunywa pombe so pombe kwangu ni mbaya ingawa nimesahau mstari kwenye biblia ila pombe ni dhambi

Anonymous said...

Ashindwe na mifano yake ya uongo hakuna kitabu kinaruhusu unywaji wa pombe amenishangaza huyo kiongozi wa dini tujuavyo pombe ni KHARAM

Anonymous said...

pombe ni haram kabisaaa,

Anonymous said...

jamani mimi kwa mtazamo wangu binafsi na c kwenye msahafu au biblia imeandikwaje kama ni dhambi au la.

Pombe is the best coz dah mshikaji ukipata 2beer twako 2wili au na zaidi kdg unajifeel raha na unapata ujacri na unakuwa huna uzushi zushi wa kijinga

Anonymous said...

hahhahah, sio kuwa ulienda kuandikisha ndoa kaka??? hahahahha.
Mimi nipo pamoja na padre kabisa, pombe si dhambi ila inakuwa dhambi pale wewe mnywaji utakapofanya kinyume baada ya kuinywa, haijalishi ni bia moja au 10, father is right.
Hakuna swala la haramu hapa kwasababu hata nguruwe mnasema haramu kisha eti ukiwa ktk janga hakuna chakula unaruhusiwa sasa si upimbi huo? utawezaje kunywa sumu kwa sababu eti hakuna kitu kingine cha kula? kama ni haramu na iwe haramu maisha sio kwenye raha tu.

Anonymous said...

soma luka21;34, habakuki2:15 na efeso 5:18 yote hii inakemea pombe kwa hiyo pombe ni dhambi ndugu yangu
ubarikiwe sana

jane said...

KWELI DUNIA IMEISHA YAANI NILITEGEMEA WATUMISHI WA MUNGU NDO WAWE MSTARI WA MBELE KUKEMEA POMBE NDO KWANZA HAWANA HABARI,HIVI KATIKA AKILI YA KAWAIDA KUNA MTU ANAYEKUNYWA POMBE HALAFU ABAKI NA AKILI ZAKE TIMAMU? KWA UFUPI 95% YA NDOA ZINAZOVUNJIKA NA WATOTO WA MITAANI USABABISHWA NA POMBE.WATUMISHI WA MUNGU NAOMBA MSIIPOTOSHE JAMII NYIE NDO NGUZO YETU JAMANI.MBONA NACHOKA MIE.

Anonymous said...

pombe ni dhambi mpendwa, kwanza kabisa biblia inasema mwili wako ni hekalu la Mungu halipaswi kuchafuliwa na kilevi ch aina yeyote wala dhambi ya aina yoyote iwayo ile. huko ulikoenda kuomba ushauri ndio walewale wanaosemaga kunywa kidogo tu si dhambi, ole wao kwa kuwa watakuja kutolea hesabu mafundisho yao siku moja. hata kibinadamu tu huwezi kunywa eti kidogo kwa kucontrol ni kiasi gani basi kinatakiwa maana kidogo ni kipi? Wawafundishe watu injili ya Mungu iliyokweli ili iwaweke watu huru kwenye vifungo vyao, Injili itakayowapelekea watu Kumwona Mungu, injili ambayo hata ukifa sasa hivi ukamwone Mungu. na sio kuleana tu kwa kutenda dhambi kwa kisingizio cha udogo, NEVER, MUNGU AMEKATAZA POMBE TENA AMESEMA OLE WAO WATUMIAO KILEO Bila kusema ni kwa wingi au kidogo, mwenye masikio na asikie.............

Anonymous said...

Hi Bw KANUMBA..Mungu azidi kukupa moyo wa kuzidi kutafakari juu ya kuielimisha jamii,kuikumbusha,kuihamasisha na hata kuikosoa kwa kupitia Mtandao wako huu....Nimeshaanza kulifanyia kazi suala hili la POMBE au "ULEVI" nikawakilisha maoni yangu mda sio mrefu....

KWA SASA NAOMBA TU NIMJIBU PAROKO WAKO...."asijibu kwa mtazamo wako bali afuate sana maandiko" kwa mfano alioutoa sikubaliani nae hata kidogo....

HAKUNA DHAMBI KUBWA AU NDOGO, katika mfano wake ni sawa na kusema ANAYEIBA PESA KIDOGO NA ANAYEIBA NYINGI WANA TOFAUTI KI-DHAMBI...au ALIYELEWA SAAAANA LAKINI ASIFANYE LOLOTE BAYA SIO DHAMBI, LAKINI ALIELEWA HATA KIDOGO ATAFANYA MACHAFU nI DHAMBI...Nadhani Paroko alikujibu kwa haraka sana bila kutafakari kwa kina!...Hili ni jibu kwa Paroko....Nitakuja tena na Mfafanuo zaidi wa maandishi!

ADVISER

Anonymous said...

Hamna tatizo kunywa pombe ili mradi unajua ngapi zinakulewesha. Usizidishe viwango. Hakikisha umekula mlo wa nguvu kabla ya kunywa. Watu huko nyumbani hufakamia bongo za bure wakati wana njaa. Biblia na Koran ziliandikwa wakati dunia haijaendelea ilikuwa haijulikani kiasi cha alcohol kwenye pombe. sasa hivi unajua pombe ipi kali ipi sio. Gongo si kwamba ni pombe kali kuliko zote, wazungu wanatengeneza poombe kali kuliko gongo, lakini gongo haina viwango vya kisayansi. Miaka kumi mie hunywa, sijawahi tukana mtu wala gombana. Hizo Biblia na Koran, wazungu wametuachia, halafu wao wanaendelea bila kufata dini
Mdau USA

Anonymous said...

OOH..Please Kanumba Rudi ntena kwa PAROKO na ukamuulize...

Je anaposema "WATU WAMERUHUSIWA WANYWE POMBE KIDOGO LAKINI WASIFANYE MABAYA ameyatoa wapi? Na kama Biblia imeruhusu hivyo "JE PAROKO ALISHAWAHI KUWAHUBIRIRIA WATU KUWA WANYWE POMBE LAKINI WASIFANYE MAOVU ??? mmmh Mi Nadhani Kama ULIWEZA KUANZIA NA PAROKO ..Usisahau kwa "MASKHEIK na WAALIM WA KIISLAM kwa kuwa mtandao wako ni wa watu wote na hauna udini....kama nimekosea NIREKEBISHENI...

JKT

Anonymous said...

jamani tucdanganyane hata kidogooo,pombe ni dhambi,kwa mtu aliyeshika imani yake asichafue hekalu la MUNGU kwa pombe sawa mbarikiwe.

Anonymous said...

jamani tucdanganyane hata kidogooo,pombe ni dhambi,kwa mtu aliyeshika imani yake asichafue hekalu la MUNGU kwa pombe sawa mbarikiwe.

Anonymous said...

jamani tucdanganyane hata kidogooo,pombe ni dhambi,kwa mtu aliyeshika imani yake asichafue hekalu la MUNGU kwa pombe sawa mbarikiwe.

Milka Richard said...

Acording 2 mm nanavyofaham pombe ni dhambi japokuwa ckumbuki vifungu kwenye biblia takatifu,lakin tunakatazwa kuitumia.Na pia asilimia kubwa ya maovu yanasababishwa na pombe,ndoa nying huvunjika,wa2 hugombana na wapenz wao,zinaa kuzid,wengine hufukuzwa mpaka makazini,wengine hudilik hata kuua sababu ya pombe.so binafs ckushaur kuitumia,kama hujaanza itumia acha kabisa ucguse.na kama unai2mia ni vizur ukaacha taratibu utazoea,na itakuongezea ufanis mzur zaid ktk kazi zako.Mungu akuongoze,akulinde na kukutunza.

Anonymous said...

Hapo ndipo utakapojua dini ya haki ni ipi.Uislm unaweka kila kitu bayana hata kama wanaadam hawkipendi, zinaa haram, pombe haram tena qurani inasema wazi faida yake ni ndogo kuliko hasara yake. Tofauti na dini nyengine zinacompromize kila uchafu ili kuwfurahisha wanaadam. haya huyo kiongozi wa dini anajibu swala zito kma hilo bila ushahidi wa mandiko. Tutafika kweli?

Anonymous said...

Kanumba ingelikuwa wewe ni muislam wakuamini unasoma Qurani na kuifuata,basi hili swali usingeuliza,kwa sababu wewe ni mkristo unamini biblia ndio mana lina kutatiza,nakushauri usisubutu hata kuigusa wala hata idondoke nguoni,mana hata tonya la pombe likigusa nguo yako haupaswi kuiabudiya nguo hiyo,kwa mana hiyo pombe ni kharam kabisa,kila la kheri Kanumba mungu akusaidie uwe muumin kweli yani muislam,inawezekana hakuna kisicowezekana Allah akipenda.

Anonymous said...

Naomba MJIULIZE..KWA NINI KANUMBA AMEWEKA MJADALA WA POMBE ???

...JIBU: Kanumba ni mkristo kama wakiristo wengine,Ingelikuwa Biblia imefafanua wazi kuhusu swala la POMBE ..basi naamini Bwana Kanumba angeliisoma Biblia na kupata jibu bila shaka yoyote. Lakini kwa kuwa Biblia yenyewe inajichanganya kutokana maandiko tofauti-tofauti ndani ya kitabu hicho kitukufu...

KAMA BIBLIA IKO WAZI..JE KWA NINI HATA WAKRISTO WENYEWE WANATOFAUTIANA KUHUSU SUALA HILI LA POMBE...Kwa nini tunajadili kitu ambacho kimeharamishwa...na ndio chanzo cha matatizo mengi sana duniani??

SWALI LA NYONGEZA:
Kwanini tumeziacha haramu nyingi zote,na kuizungumzia Pombe tu?...Nahisi kama vile kuna hisia za kujaribu kuitetea kwa kuwa "TUNAIPENDA"....Ni wapi katika Biblia imendika " TUNYWE LAKINI KIDODO NA TUSIFANYE MOVU"??? Je kama kweli tunamfuata yesu...JE YESU ALIKUWA MNYWAJI WA POMBE?? ...Kama Paroko wa Kanumba anadai sio vibaya kunywa kidogo bora tusifanye mabaya..JE TUKIMPA HUYO PAROKO NUSU GLASI TU YA "KILI" atainywa ???

Tutumie maandishi matakatifu na sio fikra na mtazamo wetu..

Anonymous said...

NENO LA MUNGU HALICHANGIWI HOYA AU MAWAZO YA WATU....NENO
NI NENO na Kama kweli halibadiliki inakuwaje leo linageuzwa na kujadiliwa...

UKIONA NENO LA MUNGU LINAFIKIWA KUYADILIWA AU KUTOELEWEKA na KULETA MJADALA...BASI UJUE KUNA "MASHAKA MAKUBWA"

masuka said...

pombe ni dhambi! hlo halipingiki, unapokunywa pombe unakuwa katka hali ambayo inaweza kuksababsha utende dhambi, na akili inakuwa umeivuruga na pengne inkulekea kufanya maamuz yasyo sahii, wee research utagundua fujo nyingi zinaletwa na wanywaji pombe, aisee! POMBE NI DHAMBI

Anonymous said...

FGG

Anonymous said...

Sasa kwenye mjadala huu mbona Waislamu mnachangia kusema hata kwenye Biblia hakuna sehemu inayoruhusu pombe.

Katika harusi pale Kana, Je Yesu alikunywa maji au pombe? kwa wakristo, Je divai ni pombe au maji?

Wakati wa Yesu ilikuwa kawaida kwa Wayahudi kunywa divai kabla ya chakula na wakati wa sherehe.

Kwenye harusi katika mji wa Kana, Yesu alienda na mama yake na wanafunzi wake. Wakati wa sherehe divai iliisha...in short...Yesu aliwaambia wanafunzi wake wajaze maji mitungi 12 na akabadilisha yale maji kuwa divai, watu wakanywa kama Enjili inavyosema kuwa wengine wakauliza hii ni kali sana kuliko hile ya kwanza. Je hayo yalikuwa maji?

Mdau,

PhD Student in Biblical Studies

Anonymous said...

pombe zamani ilikuwa ni halali kabisa,lakini Mungu baada yakuona watu wanashindwa kumuabu kwakuendekeza pombe yani na manisha waislam,ndipo apo Mungu akafika anaiharamisha,ilikuwa ngumu kidogo kwao kuzoea lakini iliwabidi waacane nayo kabisa mana ni kharam kweli kweli,nakusihi Kanumba usitumiye pombe ni kharam.

Anonymous said...

POMBE NI DHAMBI KAMA DHAMBI NYINGINE TU

Anonymous said...

HABARI YA YESU KUGEUZA MAJI YAKAGEUKA KUWA DIVAI...ni kweli ipo...lakini kinachotatanisha ni kuwa zipo sehemu nyingine nyingi katita kitabu hichohicho zinazokataza POMBE,..."kwa nini kitabu hiki kitakatifu kimefafanua habari hii ya pombe Tofauti-Tofauti ?? WHY ??

Swali kwa Mdau mwenye PHD "student in biblical studies:

Umesoma habari hiyo tu ya Yesu kugeuza maji kuwa Divai??...Hujawahi kusoma ndani ya Hiyi hiyo biblia yako kuhusu kukatazwa kwa POMBE ???

labda kwa kuwa wewe bado ni Student wa Biblical studies, UKIMALIZA MASOMO UTAELEWA ZAIDI JUU YA SUALA HILI LA POMBE...Ubarikiwe !!!

Anonymous said...

kwenye Harusi ya kana..Ni kweli yesu aligeuza maji katika yale mapipa sita, ambayo Wayahudi walikuwa wakiyatumia kuwekea maji ya kutawadhia (kama wafanyavyo waislam)..yesu akaagiza yatiwe maji, na kisha akayegeuza kuwa DIVAI..

SWALI: kwa nini alifanya hivyo?
JIBU: kabla hata yesu hajafika kwenye hiyo karamu ya harusi, tayari kulikuwepo na divai..baada ya Yesu kufika (Na mama yake Yesu pia alikuwepo) divai ilipokwisha..Mama wa Yesu (MARIA) akamwambia yesu "Divai imewaishia" yesu akajibu: "Bado saa yangu haiyaffika"
Maria akawaambia wenye harusi "Mfanye kila atakachowaambia" Yesu akawaambia wajaze maji kwenye ile mitungi sita na akayageuza kuwa DIVAI...Maandishi yakaendelea kuwa .."Kwa kitendo hicho WAKAMUAMINI" Yesu akaondoka,akaenda zake.....Je YESU ALIBADILISHA MAJI KUWA DIVAI..AKANYWA? AU ALIBADILISHA TU ILI WATU WAMUAMINI KUWA ANA UWEZO HUO?...Tafakari na utafute ni wapi YESU ALIONJA POMBE?

Anonymous said...

POMBE NI HARAMU....

SOMA kwa MAKINI mistari ifuatayo...
1. (HOSEA 4:11)
2. (WAKORINTHO 6:9-10)

Someni hizi kwanza, kama hamtozielewa au mtazipinga "Tutajadiana zaidi"

HATA NGURUWE NI HARAMU HATA KWA WAKIRISTO...SOMA:(WALAWI 11:7-8) maandiko yamesema "Nguruwe msimle,ana kwato zilizogawanyika lakini hacheuwi,kwenu huyo ni najisi,kwa sababu wanyama hao ni NAJISI msile nyama zao wala MSIGUSE mizoga yao"

ADVISER

Anonymous said...

Jamani mbona tunapotosha watu,Yesu alikunywa divai ambayo haijachachuliwa,hata na mkate ambao haujachachuliwa.
tusipindishe mambo kisa mnataka kuweka uhalali wa kiDevel hata.
angali Luka 21:34Basi angalieni mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi na ulevi wa masumbufu wa maisha haya.

Anonymous said...

Nimewaambia kuwa Hata Wakiristo wenyewe Wanatoa maandiko tofauti-tofauti...Kama wao hawakosei kutoa kauli hizo tofauti,ina maana BIBLIA INATOA KAULI TOFAUTI-TOFAUTI ????

Jamaa uliyesema wewe ni "STUDENT IN BIBLICAL STUDIES-PHD" ...Umeandika kuhusu habari ya yesu kugeuza maji na kuwa DIVAI...Ukasema waliweka maji kwenye mitungi 12 igageuka kuwa Divai....

UMEKOSEA au UMEGANGANYA ???
JIBU: Kulikuwa na MIYUNGI 6 NA SIO 12.

MUHIMU: Elewa kuwa kitendo hicho cha kugeuza Maji kuwa Divai kilikuwa ni Moja ya MIUJIZA ya mwanzo ya YESU ili AKUBALIKE, na sio kwa lengo la Kuwaruhusu watu wanye POMBE!! Vipo vitendo vingi vilivyofanywa na Bwana YESU lakini haina maana nasi pia tuzifanye..

KWA MFANO:
1.Yesu hakuona - lakini sisi tumeamrishwa kuoa,na tunamfata yesu.
2.Soma (WALAWI 19:27) neno linasema "msikate pande yote ya nywele zenu ya vichwa,wala msikate pande ya ndevu zenu" Lakini wanaofuata maandiko haya wengi wao ni WAISLAM. Kufuga ndevu kumeelezwa hata ndani ya Biblia na YESU mwenyewe alifuga ndevu kama walivyofanya mitume au Manabii wengine...

3. Soma (EZRA 9:03) kuhusu suala la ndevu kwa Manabii...

ADVISER.

Anonymous said...

JE TUMESOMA MANENO HAYA YA BIBLIA ??

(WAKORINTHO 6:9-10) inasema hivi..
JE,WAMESAHAU KWAMBA WATU WABAYA HAWATAURITHI UTAWALA WA MUNGU ?..
MSIDANGANYIKE! WATU WANAOISHI MAISHA YA UASHARATI,WANAOABUDU SANAMU, WAZINZI AU WALAWITI,WEVI,WACHOYO,WALEVI,WASENGENYAJI,WANYANG'ANYI,HAO WOTE HAWATASHIRIKI UTAWALA WA MUNGU...."

Je KUNA AWEZAE KUYAPINGA MANENO HAYA???????.......

ADVISER

Anonymous said...

nyie mnaosema eti ktka Biblia hakuna mahala panapo-support comment ya Baba Paroko mwasoma Bibliazipi ?! Au ndo ule mtindowa kukaririshwa na hao wachungaji wenu? Toeni unafikiwenu hapa. kwani katika arusi ya Kana, Yesu alifanya nini? Tena ile aliyotengeneza yeye ilikuwa kali kuliko ile ya mwanzo (kwa mujibu wa maandiko).
Na nyie mnaodai kuwa Biblia inajichanganya eti kwa sababu ya wakristo kutofautiana katika mada hii naona mnaropoka pasipo kujitathmini wenyewe kwanza. Mnataka kusema nyie hamtofautiani? inakuwaje basi wengine wenu mwavaa vijisuruali vifupi na hata kufunga mwezi wa ramadhan mnatofautiana kuanza na siku ya kufungua hivyo hivyo? Hii ni mifano michache tu, ipo mingi.

Anonymous said...

Nimependa sana debate hii. Nilipotoa mfano wa harusi ya Kana watu wamechangia na kila mtu kaja na hoja yake. Kwangu mimi nafarijika sana kujifunza toka kwa wengine.

Ni Yesu alikuwa mlevi au?Luke 7:33. Soma mstari huu wa Luka...kwa kifupi tu ni pale waliposema kuwa Yesu alikuwa mlafi na mlevi...literally translation....

Nichopenda kusema kuwa pombe ni mbaya inapelekea kufanya tendo la dhambi. Lakini Yesu ametufundisha kufanya kila kitu kwa kiasi.

Matthew 26:27, Mark 14:23, na Luke 22:17 Enjili zote hizi zinaongelea kuwa Yesu alichukua kikombe, na of course kwenye kikombe kulikuwa na divai, hii ilikuwa ni kawaida kwa Wayahudi kunywa divai...Je kama ingekuwa dhambi, kwa nini Yesu asingechukua maji ya machungwa badala ya divai?

Colossians 2:16 Usilete mtu yeyote akuhukumu una kula nini au una kunywa nini...

Ni kweli kuna sehemu nyingi sana kwenye Biblia wanasema ubaya wa pombe, kwa ujumla kama nilivyosema kuwa pombe ni mbaya,ikizidi itakufanya utende dhambi.

Lakini tumeshapalia sana hili la pombe, Biblia inakataza uzinzi Exodus 20...Je uzinzi siyo dhambi? Katika Biblia napenda sana sehemu ile ya mwanamke alivyokamatwa ana zini. Ilikuwa sheria kuwa ni lazima apigwe mawe hadi kufa. Walipomleta kwa Yesu, aliwapa jibu moja, "asiye na dhambi miongoni mwenu, na awe wa kwanza kumtupia jiwe".

Nachosema kwa nini ni mhukumu mtu kuwa mlevi na anatenda dhambi wakati mimi nafanya uzinzi kila siku, nasema uongo na kusimanga wengine. Sitoi msaada kwa maskini etc.

Ni mimi Mdau,

PhD Student in Biblical Studies.
Israel.

Anonymous said...

ASANTE uliyejiita ADVISER...ninayakubali Maoni yako baada ya kuipitia tena Biblia...Yesu alifanya MIUJIZA mengi kwa ajili watu Wamkubali..na ni kweli AKAKUBALIKA !! na ni kweli hata kama alibadilisha Maji yakageuka na kuwa Divai..na hata kama Yesu mwenyewe alikuwa ni mnywaji wa Divai...Zipo sehemu nyingi ndani ya biblia zimekataza kabiiisaaaaaaaaaa POMBE!! na hata kama Yesu alikunywa Divai HAINA MAANA NDIO AMETUAMRISHA NASI TUNYWE...."Tunatakiwa Kumfata Yesu Kwa yale Yote Tuliyoamrishwa na sio ALIYOYAFANYA YESU...

RPC - Mbago

Anonymous said...

Inategemea aia ya Imani yako. Kama Ukristo wako ni wa Mashakamashaka! basi Pombe ni dhambi. Lakini kama Ukristo wako umekua! Pombe sio dhambi.
Vivyo hivyo kwa Uisilamu Kama uisilamu wako ni wa mashakamashaka ! basi Pombe ni Kharamu, Lau kama Uisilamu wako ni alhamdulhah! unaelewa basi pombe ni suna.........Kizito!!