Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Jul 6, 2011

BONGO MOVIE ILIPOMTEMBELEA JACQUE WOLPER NYUMBANI KWAKE KUMPA POLE KWA KUMUUGUZA MAMA YAKE...

Wasanii wa club ya bongo movie tulimtembelea msanii mwenzetu Jacque Wolper nyumbani kwake Urafiki kumpa pole kwa kuuguliwa na mama yake mzazi ambaye mpaka sasa anaendelea vizuri kiafya,pole sana dada yetu Jacque Wolper... Mwenyekiti wa mipango wa Bongo Movie Steve Nyerere akitoa machache


Mdau wetu Ino Bachard akiwa na Cloud...


Steve,Odama,na Maya


Steve Nyerere akiombea chakula..


Jacque alipika chakula balaaaaa


The great na sahani yangu...kwa wale tunafahamiana katika kipengele hiki cha msosi bado rekodi inashikiliwa na mimi,swahiba Ray,JB,Cloud na Masanja,ukitualika jiandae...


mmmmh 112 Cloud anatafuna,Steve Nyerere sio mlaji kiviiiiile anaharibu tu chakula








Manywaji yalikuepo kwa wingi





Jacque Wolper akitoa shukrani kwa kuja kumuona na kuishukuru BONGO MOVIE CLUB kwa umoja huu kuwa haujawai tokea hivyo watu wayapuuze baadhi ya maneno yanayoenezwa na watu katika vyombo vya habari ambayo yanaipaka matope club hii ili ionekana ni mbaya.Zamani wakati hatuko wamoja walitusema na kutushangaa leo tumeungana na kuwa wamoja eti wanatukashifu..jamani binadamu??

10 comments:

Anonymous said...

Endeleni hivyo hivyo binadamu hawakosi lakusema. Safi sana

Anonymous said...

Wasanii wa bongo movie muendelee na moyo huo huo hata kwa wanabongo movie wanaiibukia(chipukiz) mfanye hivyo ivyo c mnafanya kwa wale maarufu na wa hali ya juu tu. ivyo mtakuwa kweli kioo cha jamii.

Anonymous said...

Yaani steve anaombea chakula wewe unapiga picha mweee.. Halafu mlienda kusalimie mgonjwa au mlienda kwa ukaribisho maalum, manake kusalimia mgonjwa kisha ma whisky wapi na wapi jamani

Anonymous said...

Hongereni sana, sema jamani unapomtembeleya mtu kwa kumpa pole msile sana, maana inakuwa siyo pole bali mnamzidishia majukumu hata kidogo alichonacho anakitowa kwenu tena! but safi sana. Ni mwongozo mzuri kwa jamii!

Anonymous said...

songa mbele achana nao

Anonymous said...

Hakuna lolote mmeenda kula tu,kwa kula vya watu tu hamjamboo.
Jesca

Kanumba said...

Ushirikiano ni mzuri na umoja ni nguvu. but nyie mnaojiita mastar wa bongo movie mtakufa kama bongo flava au movie za kihindi au za kinigeria . Uo umoja ungekua na kukanusha skendo za magazetini ingekua bora kaeni mjipange. Ustar ni kama maji ya bahari kuna kupwa na kujaa. Pia punguzeni madenda kwenye filamu uwezi kukaa unaangalia na mzazi wako.jiita mastar wa bongo movie mtakufa kama bongo flava au movie za kihindi au za kinigeria . Uo umoja ungekua na kukanusha skendo za magazetini ingekua bora kaeni mjipange. Ustar ni kama maji ya bahari kuna kupwa na kujaa. Pia punguzeni madenda kwenye filamu uwezi kukaa unaangalia na mzazi wako.

Mey said...

Ushirikiano ni mzuri na umoja ni nguvu. but nyie mnaojiita mastar wa bongo movie mtakufa kama bongo flava au movie za kihindi au za kinigeria . Uo umoja ungekua na kukanusha skendo za magazetini ingekua bora kaeni mjipange. Ustar ni kama maji ya bahari kuna kupwa na kujaa. Pia punguzeni madenda kwenye filamu uwezi kukaa unaangalia na mzazi wako.

Mey said...

Umoja ni nguvu ila kaeni mfanye mambo ya msingi. Nyie mnao jiita mastar wa bongo movie msipo kua makini mtakufa kama bongo flava au movie za kihindi au ningeria .ustar ni kama maji ya bahari kuna kupwa na kujaa. pungunzeni skendo za magazetini . Pia madenda kwenye filamu ss waafrika hiyo si utamaduni kiss inatosha mwisho mtataka mfanye live yani imekua uwezikukaa na mzazi wako unaangalia filamu. Na maliza mjipange pia kukanusha skendo zisizo za ukweli .nawatakia mafanikio mema

Anonymous said...

@ jesca we kilaza kweli, mbona misibani wayu wanakula jamani..kwa nini kumsalimia mgonjwa wasile? roho inakuuma wenzio wanavyo jinafasi roho mbaya yako utakoma