Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Jan 14, 2012

NITAKUKUMBUKA DAIMA MZEE KIPARA.

Ni wazi Mzee wetu Mzee Kipara hatunae tena,na hapa ndipo tunapouona ukuu na uwezo wa Mungu ushindao akili za mwanadamu maaana kama wanadamu tungelikuwa na uwezo wa kuzuia KIFO basi tungezuia ili tubaki na Mzee wetu,Kwangu mimi binafsi nitamkumbuka sana Mzee huyu hasa kwa mambo yafuatayo;
1.Kwangu alikuwa kama baba mzazi tena mtoto wa pekee,alinipenda sana nami nilimpenda hii utaiona hata pale alipoumwa nami nikawa nje ya nchi aliuliza mara kwa mara Kanumba hajarudi?Lakini pia kati ya namba za simu alizokuwa amezishika kichwani za wasanii wote wa Kaole nadhani ya kwangu ilikuwa mojawapo hakuitaji kuisave.
2.Mzee Kipara ndiye aliyenipokea wakati najiunga Kaole mwaka 2001 na kuhakikisha napata nafasi ya kuwa kundini humo na kufanyiwa interview,kipindi hiki alinisisitiza sana kuwahi na kufanya mazoezi,alinisihi kuacha mzaha na kujibidiisha kundini humo maana Sanaa alijua itanifikisha mbali.
3.Alinisisitizia sana Shule na kunitetea hasa pale nilipochelewa mazoezini Kaole kwa sababu ya kuchelewa kutoka shuleni nikiwa secondary,wapo viongozi ambao waliniambia soma kwanza sanaa baadae ila yeye alinitengea mda maalumu mbali na ule wa saa nane bali nilifika saa kumi au tisa na kufanya mazoezi ,Hapa alisisitiza kuwa Sanaa yahitaji Elimu hivyo soma mwanangu.
4.Alipenda sana Ukimya na Upole wangu na hapa aliongea kwa ukari kwamba Usijifanye mpole hapa ukishakuwa staa uanze kuwa kimbelembele,kwa hili nimeendelea kumthibitishia hadi pale mauti yalipomfika hakuwai kuona tofauti yangu kitabia tangu niko Kaole sijulikani hadi nilipojulikana.
5.Alinisihi sana kujiepusha na Ugomvi wowote ule,bali hekima na maarifa walinijaza yeye na marehemu Mzee Pwagu,kuna wakati walinitania wakisema weeee Kanumba ebu tizama mimi na mzee mwenzagu Pwagu tangu ujana wetu hadi sasa hatujawai hata kunyoosheana vidole,vipi nyie vijana mpigane ngumi na kurushiana maneno?siku nikikuona unapigana nakutandika na hii bakora yangu...hapa wote tulichekaa,Jambo hili nililimudu tangu Kaole sikuwai kupigana na mtu yoyote iwe kwa ngumi au kutukanana,Wazee wetu hapa walifanikiwa kutuunganisha kama ndugu walio katika kundi moja kwa upendo,Tizama leo hii hawapo TUNATENGANA,TUNAGOMBANA,HATUPENDANI,CHUKI ZA WAZI WAZI,TUNAJIKWEZA NA KUJIINUA HATA PASIPOSTAHILI,Hapa Mwenyezi Mungu atusaidie sana.Nitamkumbuka kwa utani wake alipopenda sana kunitania nami nilimtania pia,nilichukua fimbo yake na kuificha wakati akitafuta anagundua nimeficha basi anafoka kidogo ila lengo linabaki palepale UPENDO.Alinibariki na kunipongeza kwa kila hatua nzuri ya kisanaa niliyopiga,Alinitia moyo pale nilipojikwaa,Alinifariji pale nilipoumia,na akafanyika rafiki wa kweli.Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi..amen.
Hapa ni siku niliyomtembelea kigamboni wakati alipoanza kusumbuliwa na matatizo ya miguu mwaka jana.
Nilimpatia kiasi kadhaa cha fedha kwa ajili ya kupata mahitaji mbalimbali hapo alipokuwa.
Ni kawaida yake alipenda kushukuru,kubariki na kukuombea dua.
Pamoja na kwamba miguu ilikuwa inamsumbua lakini alijitaidi kunisindikiza.
Hapo ni stori mbali mbali za hapa na pale..nikiiba hekima na busara za wazee.
Hapa alivyokuwa akinielezea miguu inavyomuuma na jinsi tatizo lilivyoanza.

18 comments:

Milka Richard said...

R. I .P Mzee kipara,atakumbukwa daima kwa sanaa yake yenye umahili mkubwa.Mumuenz kwa kudumisha yale yote aliyokuwa akiwa asa.Pole sna Kanumba na kwa wasanii wote wa kaole na kwa ndugu jamaa na marafiki.
Bwana ametwaa,jina lake lìhimidiwe milele!hakika ss ni mavumbi,na tutalud mavumbin tulikotoka kwa wakat unaompendeza yy.Amen

Anonymous said...

una kila haki ya kuhuzunika kwani nilikuwa nikisoma habari zaidi ya matoleo 3 tofauti kuwa mzee alikuwa akihitaji msaada na mazingira aliyokuwa akiishi hayakuwa yakuridhisha hata kidogo...!nakupongeza sana sanaa Kanumba na nawalaani wote ambao wamejitokeza baada ya mzee kufariki na kujifanya walimpenda sana MAY GOD CURSE THEM TILL THE DAY THEY WILL DIE..!!May His soul Rest In Peace Mzee Kipara!Amen

Albert said...

"Mungu alitoa na Mungu ametwaa jina la Baba libalikiwe!"
Tulimpenda ila Mungu yeye kampenda zaidi, hatunabudi kuifurahia mipango yake yeye Mungu.
Poleni sana wasanii wenzangu msiba, kwa kuwa mzee wetu ametutoka hata kama tulikua bado tunamuhitaji. Tuzidi kuwa na upendo kati yetu na tusisahau ushauri wa mzeewetu.
Amen!

Anonymous said...

mzee kipare na pwagu hwajawahi gombana hata according to maelezo yako na unadai walikuwa wakikuasa sn juu ya hilo swali we na ray mko okey????? hakuna ugomvi mkubwa twajua ila hamko kiviiiiiile km zamani sijui hapa unamuenzi vp mzee kipara

Anonymous said...

Eti Kipara amekufa! hajafa! Angekuwa amekufa kazi zake na mawazo yake yangepotea lakini kwa kuwa kazi zake mawazo yake na fikra zake zipo ndio maana nasema Kipara yupo.
Waulize watu wa miaka ya sitini hadi sabini watakwambia kipara yupo pamoja na wenzake wote.Ombi kwako Steve kama mwili wa Kipara umeondoka kuna kilichobaki basi kidumisheni.....Kizito!!

Anonymous said...

So nice of you Kanumba. Mungu akuzidishie busara

kighumi said...

Waweja Mwanangosha! nimependa ulivyojitoa kwa mzee wako. Fanya hivyo na kwa wengine wote wasiojiweza pale upatapo nafasi ya kufanya hivyo. kwani siku zote kumbuka kuwa "Aliyekupa wewe ndo kamnyima yule." Be blessed mdogo wangu kwa upendo wako!

Anonymous said...

RIP mzee kipara, huyo ndie aliewatoa woteee si kanumba si ray si johariiii...

Anonymous said...

Maskin very touching.
May his soul rest in Peace Amen

BQ said...

POLE SANA KANUMBA, RIP MZEE KIPARA

Malkia said...

Pole sana kwa msiba mkubwa uliokufika. Kwa kweli nimeguswa sana na maneno yako ya kumbukumbu na jinsi ulivyoonyesha shukrani zako za dhati kwa yale yote uliyofanyiwa Mzee Kipara. Tunamuombea apumzike kwa amani.

Anonymous said...

MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA HUNA BUDI KUMUOMBEA MZEE WAKO KANUMBA NA MUNGU ATAKUJAALIA KATIKA KAZI ZAKO

Anonymous said...

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI

Anonymous said...

kanumba tena umetonesha donda langu, mimi si msanii ila napenda kazi za sanaa sana, kama unakumbuka nimewahi kuku tumia email lakini hujawahi kunijibu hata siku moja, mimi binafsi nashangazwa sana na wasaniii waleo hii, kila kukicha bifu, fulani kamsuta fulani, msanii wa kike kapigana na msanii wa kiume, mara kaninyima scene ndo maana nina bifu nae mara vikaenda mara vikarudi wasaniii wa leo ndo wanaopamba magazeti ya siku hizi kila toleo, wasanii wamo, mara kaa uchi mara kafanya hivi mnatia aibu, hasa hao wasanii dada zako wachafu sana, wanatuaibisha sana sisi wanawake wengine yaani utafikiri hawakuzaliwa na wanawake au hawana wazazi, wanatia kinyaa sana, wengine wanajikweza saaaaaaaaaaana utafikiri wamemaliza ulimwengu mzima, fanya mambo yako ya ustaarabu utashangaa dunia nzima inakujua na kukuheshimu, jiheshimu nawe uheshimiwe sio mtu anakuwa tu kama basi sasa ukiwa masanii ndo jalala la takataka zote, wasichana wenu aibu tupu. natamani sana kuwashauri japo ndo kupatikana kwenu laivu kwa si tusio wasanii ni ngumu. lakini jitahidini sana kuwaheshimu wasanii wakongwe, fateni waliyowafundisha na kuwakanya, kubalini kushauriwa na kusuruhishwa mara mnapohitilafiana. fanyeni kazi kwa bidii acheni mzaha, na kikubwa big up kanumba ongeza bidii zaidi, na mungu atabariki kazi ya mikono yako, kumbuka MITHALI inasema MKUMBUKE MUUMBA WAJO SIKU ZA UJANA WAKO KABLA HAZIJAJA ZILE SIKU...... MALIZIA NA UBARIKIWE NA NAKUTAKIA KILA LILILO JEMA TOKA KWA MUNGU.

makubi.blogspot.com said...

nimepitia your pages kw mara ya kwanza usijali tuko pamoja lakini sisitiza ukweli juu ya tasnia yetu kwa sababu sisi ndio walengwa bila ya kujali nafasi zetu katika wakati tulio nao.
by W.R MAKUBI
- TAFF SECRETARY
- EXC. DIRECTOR TANZANIA DEVELOP
FUND
- EDITOR
- CAMERA MAN
- CO ORDINATOR, TANZANIA FILM
TRAINING CENTER , TFTC
- etc

Gerald Henry said...

Una moyo sana kaka endelea hivyo mungu atakuzidishia.Mzee Kipara R.I.P

Anonymous said...

umepeneza ulivyoshave vizuri coz hupendezi ukibki na nywele na ndevu

Anonymous said...

Kanumba nakukubali sana kaka yangu, uko juu na una uwezo mkubwa sana endelea kuwa hivyohivyo mimi ni ndugu kabisa wa ray ila simkubali kama ninavyokukubali wewe unatumia busara nyingi sana katika mambo yako na hata katika movies zako mimi pia nina kipaji cha kuigiza ila cjui pa kuanzia but if you want to help me out just get me through this contacts 0718030910/sixtusb@gmail.com i hope tukikutana utapenda kipaji changu keep it up big brother na umfundishe na mwenzio ray jinsi maisha yanavyokwenda ila make sure mnapatana cos najua mmegombana....lol