Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Jan 24, 2012

BEST ACTOR ZIFF AWARDS (2011/2012) NI STEVEN KANUMBA.,NA BEST FILM IN SOUND NI MOVIE YANGU DEVIL KINGDOM.

Nikipokea tuzo yangu ya Best actor kutoka kwa Mr.Danny wa ZIFF,Shukrani zangu za dhati kwa majaji,shukrani kwa waandaaji,shukrani kwa mashabiki wangu wa roho na kweli,shukrani kwa walionipigia kura na kunipendekeza,zaidi ya yote sifa na utukufu nitaendelea kumrudishia mfalme wa maisha yangu YESU KRISTO na MUNGU BABA maana yeye ndiye aliyeniahidi ktk Biblia yake takatifu kuwa nikimtumaini yeye atanifanya kuwa kinara na si mkia tena atanifananisha na mlima Sayuni sitoteteleka milele,waigizaji wazuri tupo wengi ila imempendeza Mungu nichukue mimi tuzo hii kuwasilisha uzuri wa wengi tulionao.
Kaka yangu JB alichukua tuzo ya filamu bora(Senior bachelor)hongera sana kaka yangu nakumbuka baada ya kutizama filamu hii nilikupigia simu kukupongeza hasa kwa stori na uchezaji wako,mwandishi Vincent Van Goh anasema...appreciate people so that one day u ll be appreciated,if u don,t do that no one will appreciate you,,
Hiyo ilikuwa ni tuzo ya msanii bora chipukizi.....
Kambarage akipokea tuzo ya Steps Entertainment co Ltd kama kampuni bora ya usambazaji wa movie.
The great nikipokea tuzo ingine ya BEST FILM IN SOUND(DEVIL KINGDOM)hii ni ile niliyocheza na swahiba Ramsey toka Nigeria,Filamu zenye ubora huu wa sauti zipo nyingi ila imempendeza Mungu Filamu yangu kuchukua tuzo hii kuwakilisha ubora wa sauti katika filamu zetu tulizonazo.
Issa Musa(Cloud)akichukua tuzo ya BEST DIRECTOR,Hongera sana kaka yangu kumbuka Chanda chema siku zote huvikwa pete.
Picha ya pamoja ya washindi wote wa tuzo waliokuepo jana maisha club......
Interview ya Cloud mara baada ya tuzo nae kama kawa alilia na bodi ya filamu.....
Kwa niaba ya Ray ambaye hakuepo ukumbini nilimchukulia tuzo yake ya THE MOST INFLUENTIAL ICON.
Maneno yangu ya mwisho mara baada ya tuzo yalikuwa ''Hata tukiwa na uwezo wa kuhamisha milima kama hatupendani ktk tasnia ni kazi bure,kile kilicho moyoni ndio kioneshe usoni na sivinginevyo kama wanichukia moyoni basi onesha usoni na kama wanipenda moyoni basi onesha usoni na si vinginevyo,Isiwe moyoni wanichukia alafu usoni wanichekea,Hii sanaa ni karama tuliyobarikiwa na Mungu tuitumie vyema kwa ajili ya utukufu wake maana ipo siku atatuuliza na kutudai,kama katupa bure basi anao uwezo wa kutuny'ang'anya pia''soma Wakorintho uone jinsi Mungu alivyogawa karama hizi na ni kwanini katugawia.,

19 comments:

Anonymous said...

kweliiiiiiiiiiiiiiiii wambie wanafki wote message delivered

Dorry said...

Great, Great words Kanumba me love u sana

Anonymous said...

woow kanumba! i love u even more after reading ur words,Mungu abariki kazi ya mikono yako

Anonymous said...

werawera imefika hiyo vifuu tundu..

Anonymous said...

U are Great brother, nimependa maneno na hiyo picha uliyochukua tuzo kwa niaba ya Ray naomba sana huo uwe mwanzo wa kumaliza bifu lenu, live ur words brother mabifu hayajengi.

Anonymous said...

Hongera kanumba,you deserve it.

Anonymous said...

Be blessed Kanumba..I appriciate your wisdom

Anonymous said...

Kanumbaaa, wewe ni mkali katika tasnia ya filamu. Na ukitegemea mlima Sayuni hakika hutotikisika kamwe.

Milka Richard said...

Hongera sna Kanumba u deserve it bro!uko juu,zidi kuwa creative zaid.Ulichopanda ndo unachovuna ss,Mungu anazid kuonekana ktk maisha yako,sanaa yako na mafanikio yako kwa ujumla.Fans wako wa ukwel tunakuombea ufike mbali zaid ya hapo,na hakuna kinachoshindikana kwa kum2maini yy.Umefanya vizur kumchukulia ray,i like dat.Stay blessed!
Milcah.

Milka Richard said...

Hongera sna Kanumba u deserve it bro!uko juu,zidi kuwa creative zaid.Ulichopanda ndo unachovuna ss,Mungu anazid kuonekana ktk maisha yako,sanaa yako na mafanikio yako kwa ujumla.Fans wako wa ukwel tunakuombea ufike mbali zaid ya hapo,na hakuna kinachoshindikana kwa kum2maini yy.Umefanya vizur kumchukulia ray,i like dat.Stay blessed!
Milcah.

Anonymous said...

Kanumba sikuji wala unijui, lakini nakuomba kama mtanzania mwenzio, mwanaume mwenzio, kijana mwenzio,fanya hima hili muyamalize na swaiba wako, sisi ni binaadam kila mmoja ufanya sivyo sometimes, so haina haja watu mkakaa msizungumze, nakuomba chukua muda na kaa chini ufikiri imekuwaje mpaka umekosana na swaiba wako utaona mambo yenyewe ni ya kipuuzi sana, kiukweli mnamkasirisha Mungu sana,siyo vizuri kabisa ndugu yangu, hata sisi tusio mastaa ukosana pia, lakini tukishaambiwa na watu urudisha mioyo nyuma na kumaliza tofauti zetu, embe fanya kwa ajili ya Mungu, Mwenyezi Mungu apendi kabisa nawe unajuwa hilo, maneno haya ninayokuandikia nimeandika kwa Ray pia, tafadhali rudisheni mioyo yenu nyuma mkae kwa amani. na Inshallah Mwenyezi Mungu atawajalia zaidi!

Anonymous said...

upo juu kaka

Aminaclara kiparis said...

hongera bro an mungu aendelee kukupigania mpnz

Anonymous said...

kanumba uko juu mm naikubali kabisa kwa moyo mmoja kufanyiwa hivyo ni haki yako kabisa yani hakuna malalamiko wala nini unastahili mtu wangu kip it up

BQ said...

HONGERA SANA KANUMBA U ARE REAL THE GREATTTTTTTTTTTTTTTT NAKUPA BIG UP SANA YAANI MIE NAKUPENDA BUREEEEE KABISA MWENZIO AI WEWE XOXO

esther kanda ya ziwa. said...

Hongera sana kaka yangu,Mungu ataendelea kukupigania na kukuongoza,simama imara.

Sevelyner said...

Keep it up bro,god z everthng

Anonymous said...

hello brother...congrats 4the awards ulizopata...mi love the way u act,ur movies and directin...natamani ningekuwa hero kama wewe coz i like acting and writting storyz...though am still studying...be gud as u are,hardworkin is the key to success,may god help u achiev higher and higher...yan ur movie deserves kuwa best katk sound...just a big up to u brother...be blessed!!!!!!!!!!!!
ma email..mohamedlattie@yahoo.com

Anonymous said...

Hongera sana Kanumba, i like your work!May our Lord God,strenghthen and bless you always!Remember,Amtumainiae Mungu anafanya kitu chema!Just keep on cooperating with your fellow actors and specifically the Junior ones!SEBA OSHIGONGO AKUSUNGOLELE LUBANGO!