Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Mar 16, 2011

WATOTO WA UNCLE JJ WAMTEMBELEA UNCLE JJ...

Katika pitapita wanangu waliocheza katika THIS IS IT,UNCLE JJ na DECEPTION waliamua kupita nyumbani kwangu kunitembelea kidogo,lakini pia kujua kwa mwaka huu nimewaandalia movie gani?... Umeme ukikatika basi ndani hakukaliki,kushoto ni msaidizi wangu(PA)Seth,mtoto LAUREN JOHNSON aliyecheza katika DECEPTION,anayefuata alikuja na Jenifer nayeye akiomba nafasi awe kama wenzake...nyuma yao ni Patrick..anyepiga picha mbele yao ni Jenifer.

Ikabidi Patrick aje kupiga picha ili Jenifer nae awepo kama unavyomuona katikati yao

Lauren akiwa katika pozi katika movie atakayoshoot ni mpambano kati yake na Jennifer ambapo movie itaitwa IRENE and AUNTY,Lauren ataigiza kama Aunty na baba yake ataitwa Ezeckiel,wakati JENIFER ataigiza kama IRENE na baba yake ataitwa Uwoya,katika movie hiyo wote wana ndoto za kuja kuwa waigizaji wakubwa nchini,PATRICK yeye ataigiza kama RAY KIGOSI mwenye ndoto za kuja kuwa director wa filamu nchini...

Patrick akifanya mazoezi ya sauti kama Ray.

Jenifer katika pozi,yeye ataigiza kama Irene na baba yake ataitwa Uwoya wakiwa watoto.

Baada ya kutambiana nani atamfunika mwenzake Jenifer(Irene)au Lauren(Aunty) au director Patrick(Ray)...wakapata picha ya pamoja,,,nami nikawaahidi pindi kila kitu kikiwa tayari nitawaita na kuanza mazoezi kisha kushoot ila wakati wa likizo zao bila kuadhiri masomo yao.

14 comments:

Anonymous said...

Me naona hako katoto keusi cha kike katafunika sana kazuri mno halafu kanaonekana kajanja sana.
Safi sana ila shule wasome sana na wala wasiige tabia za akina AUNT EZEKIEL NA IRENE UWOYA si mifano ya kuigwa kwenye jamii.......Tabia zao chafu.
Wasome sana

lucy said...

hongera kwa kukuza vipaji vya watoto, but naomba uwe unawakumbusha na kusoma pia wasijisahau si unajua tena umaarufu ukishakuwa mkubwa kakaaaaaaaaaa.

Anonymous said...

safi

Anonymous said...

HONGERA KANUMBA KWAKUINUA VIPAJI VYA WATOTO UBARIKIWE SANA NA MIMI NAONGEZEA WAHIMIZE WASOME SANA WASIBWETEKE KANUMBA NYUMBA YAKO NZURI JAPO UMEIONYESHA KIDOGO HII NI OMBI LANGU BINAFSI NAOMBA BASI UTUONYESHE NYUMBA YAKO KWA UJUMLA NA KILA CHUMBA KWA NDANI IKIWEZEKANA KWANI SISI WASHABIKI WAKO TULIOKO NJE YA NCHI TUNATAKA KUONA MAHALI MASTAR WETU WANAPOISHI KWANI HATA HUKU MAREKANI TUNAONYESHWA NYUMBA YA MASTARKUANZIA ANAPOLALA KILA MAHALI TAFADHALI NAOMBA OMBI LANGU ULIFANYIE KAZI NAJUA UNAISHI MAHALI PAZURI NI HAYO TU OTHERWISE UNAFANYA VIZURI SANA

Anonymous said...

Kanumba mzima ww!
Ni hivi kuna mvulana mmoja anakaa mwanza anaitwa stephan kama sijakosea jina kama siyo hilo mnisamehe......
Ametoka wiki iliyopita kwenye kipindi cha clouds ''TAKE ONE'' alimuhoji ZAMARADI anadai wewe ni kaka yake?
Ni kweli au alituzuga?
Na kama ni kweli unamsaidiaje maana anasema anapenda kuigiza
Halafu hata simuelewi alisema hamjaonana mna miaka mitano...inawezekana kweli?
Me sijui lakini ni mshabiki wako nataka kujua tuu......
Unafanya kazi nzuri napenda filamu zako.

mimi said...

maskini wajitahidi na masomo pia, pia uwakumbushe wawe na tabia njema na wawaheshimu wazazi na kumuomba mungu wasije wakaharibika kama lulu. nakuaminia the great

Albert said...

Hawa watoto si vibaya hata kidogo kuwashirikisha kwenye movies ila ni vizuri pia kuwaandaa kwenye maisha yao ya baadae. Wasije wakajikuta wameharibu future yao kwa kuacha kusoma au kwa kushawishika na mafataki. Si unajua ukisha kuwa star? Hawa watoto msiwaache, la sivyo wataharibika, umri wao bado ni mdogo sana wanahitaji malezi.
Uncle JJ uwe makini sana!
Albert
Australia.

Anonymous said...

nina wapenda wope nawatatoka boba sana naisubili dukani

Anonymous said...

nina wapenda wope nawatatoka boba sana naisubili dukani

sophia mkumbo said...

kaka una jitahidi mi huyo mtoto jannipher ananitishia sana yaani namuamini ila asilewe sifa ila anaweza na naisubili kwa hamu hiyo filamu nione uwezo wa watoto big up mkubwa unatisha

Anonymous said...

msiiigi tabis za Lulu wanangu msiige kabisa aliaza km nyinyi lakini sasa hivi amekuwa na tabia mbaya zisizo semekana na ameshindikana hata na mama yake mzazi nawapendeni sana nawatakia mafanikio mema kanumba wachunge sana hao watoto.

Anonymous said...

hi kanumba mm ni mshabiki wako nakupenda sana ,napenda kazi yako uko juu sana kaka napenda sana unavyo inua watoto kama wakina jenifer,,nitapenda tuwasiliane zaidi,,nitakutafuta ,,wako mdau kutoka Holland

Anonymous said...

Mi si mshabiki sana wa movie za kibongo ila THIS IS IT ilikuwa ni funika na hao watoto nimewakubali kabisa. Wana vipaji vya ukweli

Anonymous said...

kawaida ya watoto wanachokifanya sana ktk muvi ndo kinachowaathiri watazamaji bila ya kuangalia mwisho wa film.mi naona maudhui ya muvi ya hao watoto ingehusu suala zima la elimu.maybe tufanye kwamba jenipher ana lengo la kusoma na kuwa daktari tokea utotoni au lawyer,kwa hivyo anashajihisha watoto wenzake juu ya kuweka mazingira safi ili kujikinga na maradhi ya kuambukizwa kwa malaria,uharo na mengineyo,yani nnachokusudia maudhui isiwe kuwa muvi star tu kwani tz tunahitaji madaktari,malawyer na viongozi wengine hapo baadae,so kupitia watoto hao tunaweza kuwaelimisha watoto ktk jamii kwa ujumla..............