Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Dec 6, 2011

THE GREAT NDANI YA MWANZA NA STARTIMES....

Kila zawadi niliyoitoa ilinibidi nisaini


ilifika wakati wa kila shabiki wangu kupiga picha na mimi


Wakala maarufu wa startimes Mwanza nilimpa zawadi ya picha tuliyopiga pamoja Dar-Movenpink siku niliyosimikwa rasmi ubalozi.





Huyu mama toka matangazo yakitangaza kuwa Kanumba atakuepo viwanja hivyo toka asubuhi alikaa akinisubiri hata pale watu walipojaa na kumziba asinione pamoja ni mlemavu alipaza sauti akisema mwanangu kanumba naomba nikushike mkono nakuonaga katika tv,na hapo ilikuwa ni saa tisa maskini hajala ili anione tu,nami nilikatisha onesho hili na kuamuru aje mbele kufika kumbe ni mama mlemavu kaletwa na mwanae akimsukuma hakika huruma ilinijaa sana,mama aliongea akilia kuonesha upendo wake kwangu,nilimpatia zawadi toka Startimes lakini pia nilitoa pesa yangu na kumpa mama akale na mwanae,Nilimuuliza Mungu moyoni tizama mama huyu mwenye upendo wa dhati lakini ni mlemavu na asiye na uwezo mzuri kimaisha,vipi vijana wenzetu wenye afya nzuri lakini hawana upendo wala uzalendo kama huu,bali chuki,ugomvi,matusi na kupondana,Dunia hii kwa sasa inahitaji upendo na uzalendo kama huu wa huyu mama...ni maono yangu tu.


Mama akilia baada ya kupokea zawadi huku mwanae akimsukuma ktk baiskeli ya walemavu mara baada ya kuongea na mimi.


Dada huyu akipokea zawadi mara baada ya kuweza kuigiza kicheko changu na watu kumshangilia,sikujua kama mashabiki hufatilia hata jinsi mtu unavyocheka.



NIKATOKA MBEYA NA KUELEKEA DAR ALAFU DAR TO MWANZA.

Nyuma akiwa msaidizi wangu Sethy Bosco.


Angani nikiwa mbele na dereva.


kwa juu


Mawinguni....

Dec 4, 2011

THE GREAT NDANI YA MBEYA MJINI NA STARTIMES KWA AJILI YA X-MASS

ENJOY PICHA....ZAWADI KIBAO NILITOA HAPO...























Nov 29, 2011

CHINEDU IKEDIEZE(AKI) AFUNGA NDOA....

Msanii maarufu mfupi toka Nollywood,anayeigiza sana comedy Chenedu wa AKI na Ukwa,,jumamosi iliyopita tarehe 26 mwezi huu amefunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Nneoma Nwajah katika kanisa la St.Theresa-Imo state.The great kupitia mtandao wa BBM nilimtumia ujumbe wa kumpongeza nae akashukuru sana.


oooh Chalee congratulation my broda.....

TWANGA PEPETA WAFANYA KUFURU LONDON...KAMA KAWAIDA YAO....

UMATI WA MASHABIKI WA TWANGA LONDON ULIVYOFURIKA KUSUGUA KISIGINO....


KIBOSHO KAMA KAWAIDA KTK DRUMS





Nov 9, 2011

MUONEKANO WANGU WA SASA HIVIIIIII.....

NIENDELEE AU NIISHIE HAPO???











NILIAMUA KUFANYA HIVI BAADA YA MASHABIKI WANGU WA KWELI WENYE MAPENZI YA DHATI NA MIMI KUNISHAURI KUWA NILINENEPA SANA HIVYO MWILI KUKOSA MVUTO KAMA WA AWALI WALIOUZOEA KATIKA FILAMU ZANGU LAKINI PIA HOFU YAO IKAWA KATIKA UNENE WANGU ULIOELEKEA HATA KUNILETEA KITAMBI KWA MBALI HIVYO KUHISI BAADHI YA SCENE SITOZICHEZA TENA,NDIPO KWA DHATI KABISA NIKAANZA KUFANYIA KAZI MAONI YENU KWA KUPUNGUZA KULA(DIET) MAANA HII ILIKUWA NI UGONJWA WANGU NA HAIKUWA RAHISI,LAKINI PIA NIKAANZA MAZOEZI KWA KASI JAPO NA HII NAYO HAIKUWA RAHISI MAANA UBUSY MWINGI MARA SHOOTING MARA SAFARI ILA NIKAWEKA NIA,NA LEO HAPO NDIPO NIMEFIKIA SASA JE NIISHIE HAPO?AU NIENDELEE TENA?AU NIRUDI KULE KTK UNENE??

MARA TU BAADA YA KUANZA DIET NA MAZOEZI KWA NGUVU MUONEKANO WANGU UKAWA HIVI.....

HAPA NIKISHOOT ''BECAUSE OF YOU''ILIYOTOKA HIVI KARIBUNI......








MWANZONI MWA MWAKA HUU KABLA SIJAANZA DIET NA MAZOEZI KWA NGUVU..MUONEKANO WANGU ULIKUWA HIVI....

WAKATI WA THE SHOCK...


WAKATI WA DEVIL KINGDOM....

Nov 7, 2011

BAADA YA KUTUA TU BONGO THE GREAT NA STARA THOMAS WAUNGANA NA MAMA SALMA KIKWETE KATIKA CHARITY WALK-SAIDIA WATOTO WENYE KANSA.

Matembezi yalianzia mnazi mmoja mpaka Movenpick.na kiasi cha pesa zaidi ya milioni 40 zilichangwa kusaidia watoto.The great kama balozi wa OXFAM GROW nilichangia milioni mbili na Stara milioni moja.


Nikisalimiana na mheshimiwa Zhakia Megghi


Nikisalimiana na maafande





Ilituongoza.....





Mama Salma Kikwete akifungua matembezi rasmi..





Watoto toka shule mbalimbali walikuepo.....

THE GREAT ALIVYOTEMBELEA SOKO LA FILAMU GHANA...

Nilipata muda wa kutembelea soko la filamu Ghana na kuweza kununua baadhi ya movie kwa ajili ya kutizama ila pia kuongea na mtayarishaji na msambazaji mkubwa wa filamu Ghana na mkurugenzi wa VENUS FILMS PRODUCTION,ndugu Abdul Salam.ndiye mmoja wa waasisi wa Ghallywood(Ghana movie industry).moja ya maongezi yetu ni ushirikiano wa filamu za bongo na Ghana lakini pia kutanua soko letu la filamu n.k.maongezi yalikwenda vizuri sana. The great nikichagua filamu


The great na Prince Richard Nwaobi


Kibao kinachoonesha ofisi yake.


The great,Monalisa na Abdul Salam from VENUS FILMS PRODUCTION mara baada ya kumaliza maongezi.


Monalisa nae alinisaidia kuchagua filamu....


Katika ndege nikirudi bongo


Masaa 6 angani yanachoooooshaaaaaaaaa



Staa anayependwa sana kwa sasa Ghana John Dumelo,Mona,Prince Richard,kabla ya kufika Ghana nilijua anayewatingisha huku ni Van Vicker kumbe kwa sasa ni huyo kaka na Michel Majid yaani wanapendwa sana,Van Vicker hayuko sana katika movie zao na kama vile amebaki kucheza movie za Nigeria na za kwake ambazo hazifanyi vizuri sokoni Ghana.kwa tetezi nilizosikia ni kuwa alianza kuwa msumbufu hivyo maproducer na directors wakaamua kuacha kumpa kazi jambo ambalo linazidi kumshusha.