Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Dec 6, 2011

THE GREAT NDANI YA MWANZA NA STARTIMES....

Kila zawadi niliyoitoa ilinibidi nisaini


ilifika wakati wa kila shabiki wangu kupiga picha na mimi


Wakala maarufu wa startimes Mwanza nilimpa zawadi ya picha tuliyopiga pamoja Dar-Movenpink siku niliyosimikwa rasmi ubalozi.

Huyu mama toka matangazo yakitangaza kuwa Kanumba atakuepo viwanja hivyo toka asubuhi alikaa akinisubiri hata pale watu walipojaa na kumziba asinione pamoja ni mlemavu alipaza sauti akisema mwanangu kanumba naomba nikushike mkono nakuonaga katika tv,na hapo ilikuwa ni saa tisa maskini hajala ili anione tu,nami nilikatisha onesho hili na kuamuru aje mbele kufika kumbe ni mama mlemavu kaletwa na mwanae akimsukuma hakika huruma ilinijaa sana,mama aliongea akilia kuonesha upendo wake kwangu,nilimpatia zawadi toka Startimes lakini pia nilitoa pesa yangu na kumpa mama akale na mwanae,Nilimuuliza Mungu moyoni tizama mama huyu mwenye upendo wa dhati lakini ni mlemavu na asiye na uwezo mzuri kimaisha,vipi vijana wenzetu wenye afya nzuri lakini hawana upendo wala uzalendo kama huu,bali chuki,ugomvi,matusi na kupondana,Dunia hii kwa sasa inahitaji upendo na uzalendo kama huu wa huyu mama...ni maono yangu tu.


Mama akilia baada ya kupokea zawadi huku mwanae akimsukuma ktk baiskeli ya walemavu mara baada ya kuongea na mimi.


Dada huyu akipokea zawadi mara baada ya kuweza kuigiza kicheko changu na watu kumshangilia,sikujua kama mashabiki hufatilia hata jinsi mtu unavyocheka.4 comments:

Anonymous said...

pole kaka kanumba maneno yako uliyeyasema juu mama mlemavu yamenigusa sana wewe kanumba endelea na kazi yako na utaendelee kubarikiwa maana roho yako ni nzuri na unasaidia wasio jiweza usiwajali wenye roho za kwa nini kwani aliyepewa kapewa tu hata wafanyaje wenye chuki hazitasaidia kitu big up kanumba nakupenda sana

ngaizaskids said...

ni kweli mpendwa, kwa nini hatupendani binadamu? ukiuliza msanii gani unampenda utaambiwa willy smith na wengine wa marekani kwa nini hatuwakubali wakwetu? tupendane wapendwa.

Anonymous said...

kwa kweli nilipo muona huyomama namaneno uliyosema kwa kweli nimelia mungu atakubariki .

fan said...

Big up bro. Uendelee na moyo huo wa upendo. Mungu akubariki, nategemea wasanii wenzako watafuata mueleko wako.Hope to c u again California...