Juzi maeneo ya magomeni mikumi kulikuwa ni KAOLE DAY wasanii wote wa kaole wa zamani na wa sasa na wote waliowahi kuwa katika kundi hili tulijumuika pamoja kukumbuka mazuri yote ya kikundi chetu kilichotutoa kisanii,tukikienzi na kuhakikisha Kaole inadumu milele.Mastaa wengi wa filamu na tamthilia tumeanzia hapa,ni kundi lililoanza mnamo mwaka 1999,chini ya mkurugenzi na mwasisi Mr.Chrissant Mhengga,Lilipewa jina kaole ikiwa ina maana nenda kaone,Mpaka sasa kaole ina zaidi ya miaka 11 wakati vikundi vingine vimeshakufa lakini Kaole ipo na kimekuwa kama chuo cha mafunzo kwa wasanii wengi,Kina zaidi ya tamthilia 15 ambazo zimeshaonekana katika tv mbalimbali(ITV&TBC) kama HUJAFA HUJAUMBIKA,FUKUTO,JAHAZI,DIRA,TETEMO,TUFANI,SAYARI,BARAGUMU,GHARIKA,TASWIRA,ZIZIMO nk.Baadhi ya wasanii tulioanzia kaole ni,KANUMBA,RAY,MUHOGO MCHUNGU,KIPEMBA,CHENI,MTUNISI,FRANK,NINA,NANA,NORAH,SINTA,KIBAKULI,NYAMA YAO,BI STAR,BI TERRY,MZEE PWAGU,MZEE KIPARA,MAMA HAMBILIKI,MAX,ZEMBWELA,BAMBO,KINGWENDU,KEMMY,BENY,SWEBE,JERRY,CHUZ,MASHAKA,KISSA,AIKA,LIGHT,JOHARI,MAINDA,TEA,MAYA,SAJUKI,DINO,MZEE PEMBE,SENGA,TITO,MBOTO,KEVIN,ZAWADI,BAHATI.BUPE,BI MWENDA,BI KIDIDE,....nk. Director wetu Chrissant Mhenga na Kemmy kabla ya kuingia katika ukumbi wa mazoezi
Chrissant Mhenga akitoa mawaidha yake ambapo wasanii wengi tulifurai kumuona tena mahali hapa,hakika alitufundisha mengi sana katika sanaa,tulimshukuru sana na tutazidi kufanya hivyo.
13 comments:
kazi nzuri sana kanumba ubarikiwe mimi niko nje ya nchi kwa sas nilikuwanaomba jinsi yakupata cd movie yakaole ya zamani wakati mnaigiza hawa woote uliowaorodhesha naomba nipate cd yao yazamani pls
Nimeipenda Kaole day! Mzee Chrissant
hayupo tena kaole? je vipi ule mgogoro wa kaole uliosababisha baadhi yao kujitoa umeisha?
My take: nyie mlio nje ya kaole kwa sasa mkifanya issue zenu binafsi muwasaport waliobaki waweze kufanya kama mlivyofannya ninyi b4 coz now kunddi linapoteza mvuto kwa sasa ingawa ni kongwe iko siku litaanguka kama extra powerr toka kwenu wadau haitawekwa
jamani ni imani yangu kua huyo crissant japo amefaidika, kimaisha maana kawainua weeengi, fanyeni mambo mumuinue na yeye kifedha.
JAMAN MMENISISIMUA SANA WANA WA KAOLE MPAKA MACHOZI YAMENITOKA MMEANZA MBALI. KUMBE WASANII WENGI HIVYO MNAOFANYA VIZURI WENGI MMETOKA KAOLE, MDUMU MILELE JAMANI NA KAOLE IDUMU MIAKA 1000. MSIACHE KUFANYA KILA MWAKA NA WASANII MLIOTOKA KIMAISHA MSAIDIE KIKUNDI CHENU HICHO MANA KIMEWATOA MBALI.
Hongereni sana Nina siku hizi anafanya nini? Ameacha kuigiza. Kwa kweli ukuangalia zile picha zenu za zamani zilikuwa zinavutia sana. Yaani mliigiza Kitanzania. Mbona sijamuona Muhogo mchungu? Yaani Muhogo Mchungu anafaa kuwa Muigizaji bora Hivi siku hizi ameacha naye kuigiza?
Kwa kweli nimefurahi sana kuwaona wasanii wa zamani wa kaole ambao walikonga nyoyo na kufanya mapinduzi katika fani ya sanaa ya maigizo Tanzania. Nime wa miss sana akina Nora, Sinta, Kibakuli, Bi Terry, Nyama yao, Mashaka, Kissa, Aika, Light n.k.Kundi lilikuwa lina mvuto sana wakati vipindi vyenu vinarushwa ITV lkn sasa tangu muhamie TBC limepoteza mvuto na linaendea kufa, sijui tatizo ni nini au labda wasanii wengi wamehamia kwenye filamu. Mmetoka mbali sana, hapa mlipofika si haba, mshukuruni Mungu na kutumia vizuri kile mnachopata huku mkiwanyanyua wenzenu walio chini. Nawatakia kila la kheri!
yaani kanumba unanifurahisha sana hicho mlichofanya ni kizuripia kakayangu unajichanganyan kwenye shughuli na wenzako inafurahisha sana Mungu akutangulie kwa kila jambo
yaani kanumba unanifurahisha sana hicho mlichofanya ni kizuripia kakayangu unajichanganyan kwenye shughuli na wenzako inafurahisha sana Mungu akutangulie kwa kila jambo
yaani kanumba unanifurahisha sana hicho mlichofanya ni kizuripia kakayangu unajichanganyan kwenye shughuli na wenzako inafurahisha sana Mungu akutangulie kwa kila jambo
Reyuu nimefurahi kumuona,aisha mbona hakuwepo jaman? kaka Dino kwema hapo kwa Reyuu mmmmh.
hakika ni kitu kizuri sana pia kwakweli hili ndilo lilikua kundi mama maishani kuliona na nilipenda sana michezo yake kipindi kile hasa michezo km ujafa ujaumbika,jahazi nk ilikua ni mirefu na ilikua inaelimisha kweli jamii mimi mchezo hule wa kisa na mashaka na dr chezi nilikubali dada yangu aolewe na mlemavu ingawa mwanzo nilikataa katakata hila mpakaleo uwa namambia dada yangu kua unajua mimi kisa ndio alinifanya nimkubali shem so ni kitu kizuri sana hila kwa jinsi sasa mulivyo litendea hilo kundi baada ya kila mtu kuanza kutoa filamu yake na mpaka leo mumeshindwa kutengeneza hata sehemu ya kuigizia please jamani musiwe wa binafsi ki hivyo na pia mr chiki fanya kazi yako hili kundi hili lirudi kama zamani
Nimefurahi sana kuwaona Rayuu, Kemmy, Swebe Bi hindu na wengne safi sana nilikua napenda sana kuangalia Kaole sanaa Group sina uhakika km hlo jina bado lipo hvyo, vp Vicent KIGOSI hakuwepo ama nimechapia maana namkumbuka kwenye filamu zenu km vile Johari, dah big up wakuu kisima cha burudani na maelimisho....
ilikuwa raha sana nahisi mliienjoy sana maana natumaini wengine hamkuonana mda kidogo lol
meggie impostra
Post a Comment