Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Dec 28, 2009

Hongereni YANGA


Hatimaye yale mashindano yanayoandaliwa na Bia ya Tusker (Tusker Cup) yamemalizika jana kwa wanajangwani Dar Young African (YANGA) kuchukua ubingwa huo kwa mara ya pili kwa kumkandamiza Sofapaka ya Kenya mabao 2 - 1. Yanga ambayo ilionekana kutawala zaidi mpira katika vipindi vyote viwili ilipata pigo la gori la kwanza kwa mpira wa adhabu uliopigwa moja kwa moja na kujaa wavuni katika kipindi cha kwanza. Yanga iliendelea kulisakama lango la sofapaka bila ya Mafanikio hadi wanakwenda kupumzika ikiwa nyuma kwa bao moja. kipindi cha pili yanga ilionesha uhai zaidi kwa kuendeleza mashambulizi yake lakini hayakuzaa matunda mpaka Papic (Kocha wa Yanga) alipoamua kumtoa Nsajigwa na Kumuingiza Fred Mbuna, na Jerryson Tegete kumpisha Boniface Ambani ambao kwa kushirikiana na Mrisho ngassa, Athumani Idd (Chuji) na wengineo katika safu ya Ushambuliaji wakaandika bao la kusawazisha mnamo dakika ya 86 kupitia kwa boniface Ambani. Muda sio mrefu mnamo dakika ya 90 yanga iliandika bao la Kuongoza kupitia kwa Mrisho Ngassa.

kutokana na hayo tunaipongeza Yanga kwa kuonesha mchezo mzuri na hata Kuchukua Ubingwa huo.

No comments: