Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Feb 22, 2011

THE GREAT NDANI YA JUKWAA LA SANAA(BASATA)

Jana nilipata mwaliko wa kuhudhuria jukwaa la sanaa ambalo hufanyika kila jumatatu hapo Baraza la sanaa taifa,nilipata nafasi ya kuzungumza mengi na uongozi wa BASATA lakini pia waandishi,wanachuo na wadau mbalimbali wa sanaa hii ya filamu,mada ilikuwa ni jinsi gani twaweza ifikisha tasnia ya filamu kimataifa zaidi. The great nikiwa meza kuu na uongozi wa juu wa BASATA.kushoto ni katibu mkuu wa basata.

Nikiifafanua mada hiyo kwa uyakinifu



Umati wa watu mbalimbali wakiuliza maswali ambayo niliyajibu vizuri na kwa ufasaha

Niki note kidogo baadhi ya point zilizoongelewa hapo

Swali hilo kwanini majina ya filamu zetu ni kiingereza wakati ndani ni kiswahili?...nilijibu swali hili lakini pia niliweka angalizo kuwa si filamu tu pekee hata radio,tv,vyama vya siasa,shule n.k majina yao ni kiingereza ila ndani wanaongea kiswahili hapa bongo hivyo.

Ilibidi nisimame ili watu wote wanione

Hapa nikielezea jinsi utandawazi nao jinsi unavyoharibu maadili.

Katibu wa basata nae akichangia machache juu ya mada yetu.....

3 comments:

Anonymous said...

Kanumba, unapofanya kitu usifanye kwa sababu fulani kafanya hapana u r wrong, fanya kitu na utoe sababu kwanini umekifanya maana wewe ni wewe na hufananishwi na tv, radio wala wanasiasa. kujibu kwa ufasaha ungesema (kwa mfano) unaweka majina ya kingereza kwa sababu ya utandawazi kwani filamu zenu kwa sasa zinavuka nje ya nchi nyiingi zinazoongea kingereza na ndo maana mnaweka hata subtitle za kingereza ndani lakini lugha inabaki kuwa kiswahili. Hili ni katika kuweza kutambulika zaidi kimataifa na kwasababu kingereza ni lugha kubwa kuliko zote duniani na si kwasababu kila mtu anafanya hivyo HAPANA nimekataa kwani yawezekana hao tv, radio na wanasiasa wakawa na maana yao nyingine tofauti na ya kwako, jifunze kujitofautisha, kujiamini kwa kila unachofanya na si kuangalia nani anafanya nini.

Anonymous said...

Kwasawala la maadili nakubaliana na wewe mia kwa mia kwamba filamu zetu hazichangii. hii sayansi na teknolojia ndo ilaumiwe na pia wajue si tanzania tu ni dunia nzima yale maadili ya kipindi icho hayapo tena si kwa wachina,wahindi,wala waarabu tunaishi kutokana na sayansi ilokuwepo sio zamani walifanayje hpn.
Haya mfn kipindi cha nyuma uchekeshaji wa kina majuto ,small na bi chau ulitamba sn sasa ivi sizani km wanamarkrt km enzi izo na ndo mana wachekeshaji hawana kipato kikubwa km waigizaji wa filamu mana ndizo zinazopendwa zaidi kwa sasa
Wachekeshaji km ze comedy wanafanya REALITY mambo ya bunge,afya,burudani yani kitakachojiri ndani ya wiki chenye maana lazima wakitoe sio vibweka bora vibweka ambavo kwa sasa havina soko kutokana na sayansi na teknolojia na si kupotea kwa maadili
Haya mapenzi na mavazi tunayoyaona kwenye filamu hata wasnii wa mziki ndiyo wanayoimba video zao wenyewe nyingine balaa lakini hazisemwi ni fiamu tuu kwanini???? haya filamu ya shoga imezuiwa eti inachunguzwa mbn hawaeleweki hawa watu???
Siku izi ni km fashio ktk wanaume 10utakaopishana nao 3 au 4 ni mashoga tena hata hofu hawana wanajiweka hazarani na ndomana ikatengenezwa filamu mana wamekuwa wengi hapo napo utasema ni filamu zinaharibu?? yani filamu inamfanya m2 awe shoga?????Wahusika wa sanaa wasikurupuke wanatuulia raha sie watazamaji

Anonymous said...

duuh kweli wewe the great, sikuwahi kufikiri kwa nini radio ziwe na majina ya kizungu na wanaongea kiswahili na nyie filamu zenu kuweka majina ya kizungu kwenye kava iwe inshu mbona radio hawazisemi... safi sana inaelekea uliwapa kigugumizi. all the best brother.