Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Aug 19, 2011

MASTAA WA MOVIE GHANA NA NIGERIA WENYE FAMILIA ZAO(MKE\MUME NA WATOTO)

SWAHIBA WANGU RAMSEY NOUAH(NIGERIA) Ameoa na ana watoto watatu ila mtoto wake wa kwanza alizaa kabla ya kuoa anaishi Marekani,Mkewe anaitwa Emily na amezaa nae watoto wawili yaani Quency na Camili kama unavyoona katika picha hapo juu.


VAN VICKER(GHANA) Ameoa,jina la mkewe ni Adjoa,wamezaa watoto watatu ambao ni J'dyl,J-ian, na Vj kama unavyowaona katika picha hapa juu.


DESMOND ELLIOT(NIGERIA) Ameoa na mkewe anaitwa Victoria na mwaka jana walibahatika kupata watoto mapacha...kama unavyowaona hapo juu katika picha.


GENEVIEVE NNAJI(NIGERIA) Hajaolewa japo ana miaka 32 kwa sasa,ila ana mtoto wake wa kike anayeitwa Jullieth aliyemzaa akiwa na miaka 17 alipopachikwa mimba utotoni,mpaka sasa Jullieth ana miaka 15.watizame hapo katika picha.


MAJID MICHEL(GHANA) Ameoa tangu mwaka 2004 nchini kwao Ghana na mpaka sasa ana watoto wawili,picha hapo juu ni yeye na mkewe na mtoto wao wa pili.


OMOTOLA JALADE(NIGERIA) Ameolewa tangu ana miaka 18 na mmewe Mr.Mathew Ekehinde,walianza mahusiano yao tangu Omotola akiwa na umri wa miaka 16 kabla hata hajaanza kuigiza,mpaka sasa wana watoto wanne kama wanavyoonekana katika picha.

21 comments:

Anonymous said...

BADO WEWE

Anonymous said...

wewe unasubiri nini umri unaenda kaka

Anonymous said...

haya sasa na wewe UOE..sio kutoka na masista duu tu wanaouza Sura kwenye Kideo..kua Mfano wa kuigwa, na kwani lazima uwe na msichana maarufu?ona wenzako ...tafuta mdada mwenye heshima na mwenye kazi yake anaejua nini maaana ya kua na msaidizi wake katika maisha na si kukutamani wewe kama msanii..TAFAKARI CHUKUA HATUA.

Rachel

Anonymous said...

oa na wewe umri umeenda

BQ said...

SAFI SANA KANUMBA HABARI NZURI UMELETA KEEP UP KAKA ILA WAKO WENGI SANA HUJAMALIZA FIND MORE, WE LOVE UUUUUUUUUUUUUUU

ON FIRE link. said...

vipi kuhusu mastaa wa bongo walio oa na wana watoto wangapi ,ukiwemo wewe igeni mfano wa wenzenu .

Anonymous said...

woow familia zinavutia sanaaa, wabarikiwe zaidi,,, sasa mr kanumba tafuta mwanamke aliyetulia hana umaarufu wowote oa bwana heshima itaongezeka, inapendeza kuzaa ukiwa bado kijana , ili ukifikisha miaka 35, mtoto wako atakua atleast ana miaka 6 kuendelea

Anonymous said...

Unaweka ndoa za wenzio ya kwako iko wapi???

Anonymous said...

Muoe wema hata move mlizocheza nae ukifananisha na wasichana wengine ulioshiriki nao wema ukiwa nae mnatengeneza couple nzuri sana.

please mtoe kwa diamond anafujika lile ni ua linalokupendeza. kwanza hata kuigiza anajua kuuva uhusika kuliko msichana yoyote wa game ya move bongo.(no wapo wakina riyama na wastara) wengine wanaonyesha mapaja tu. Please naomba ucheze nae move nyingine then mmalize tofaiti zenu. kwani wagombanao ndio wapatanao.

Anonymous said...

Angalia move mlizocheza na WEma halafu fikiria mara mbili. anastahili kuwa ua lako. Good couple mtatengeneza. kuwa nae please halafu uone.

Anonymous said...

Nimetoka kuangalia picha moja ya Va Vicker na Mercy si mchezo. Huyu van Vicker nadhani atakuwa ni half cast wa ki dutch. Napenda movie zake sana naona anamfukuza Swahiba wako lover boy kwa karibu sana. He is also very handsome. Am happy kama ameoa na kutulia maana na uzuri alonao kutanga tanga kungempeleka pabaya.

Na nyie igeni mfano Kuoa dili bwana. Una kuwa na heshima na ni vizuri kuwa untaegemewa sio kula rahah tu!

Anonymous said...

hi kanumba wasikushinikize umrudie huyo malaya wema hakufai kamwe tafuta mwanamke waheshima kaka yangu nakupenda sitaki yakupate yaliokufanyia huyo wema tena ni yeye mwenyewe aloandika hizocomment anajipendekeza tuu hana lolote abaki na huyo bwanamdgo diamond kama mtu na mwanae loh mwl mkuubwa wema pale anaonekana kama jimama atajiju kanumba hakutaki tena jamani siumwache kaka yangu mbona kinganganiz ataamua yeye amuoe nani halaaaa mnaniudhi wu wengine

Anonymous said...

Safi sana kaka Steve tuwekee na wabongo

Architect said...

Mkuu Kanumba!
mbona hujibu maoni ya wadau?wadau tumetoa vilio vyetu vilivyoambatana na ushauri.Tunahitaji kusikia na comment kutoka kwako.Huo ni upendo kwako kaka!

Anonymous said...

nimegundua wa ghana/nigeria walio half cast hawa mind kuoa mtu mweusi.ingekuwa bongo,wanaume half cast wangetafuta weupe wenzao.mfano mkubwa hao waarabu,wanapenda kuoa waarabu wenzao.genevieve alisema huyo sio mtoto wake ni fan alipiga nae picha,ingawa wamefanana.mtoto wake hamuonyeshi kabisa kwenye media.harusi vya omotola ilifanyika kwenye ndege,simuwezi.na desmond ana watoto 4 sio 2.wote ni twins.mara ya kwanza alipata twins na mara ya 2 alipata twins

Anonymous said...

KANUMBA TUNAKUOMBE UMUOE WEMA,LABDA ATATULIYA KWASABABU WEWE UNAHIKIMA SAAAANA PLS FANYA HIVO KAKA.

Anonymous said...

ni kweli Genevive hamuoneshi mwanae wala hamtambulishi jina lake wala la babake, mahalf cast wa Ghana hawana uchaguuzi cjui longolongo tena ndo ma spa zaid ya staa cyo wabongo mfan ww mwenyewe unaona huwezi kutoka na demu asiejulikana.

Anonymous said...

Mdogo'gu kwa Wema wala sikushauri kabsa kurudi tena! Si lazima kuoa star au mdada maarufu nakwambia itakusumbua sana,ona wenzenu wake zao sidhani kama ni ma-star na wanaonekana ni wadada wenye shughuli zao za maana na wanaelewa maana ya ndoa. Pia nawe uoe umri unakwenda, kuna leo na kesho bwana maisha ni safari ndefu better kuwa na familia yako na wewe ili uheshimike. Mtangulize MUNGU ktk kuchagua mke mwema.

Anonymous said...

Mbona wewe kimya umri unaenda kijana tafuta jiko sasa

Anonymous said...

very nice kuona kuwa vijana wa kinigeria na ghana (movie stars ) wote wana permanent responsibilities in life! excellent stuffs! kanumba igeni huu mfano jamani

Anonymous said...

you need to think b4 you decide kanumba ndoa siyo lelemama, but ni vizur ukaoa mwanmke analiyekua kiakili mwenyehekima na aliyelelew kwenye familia yenye maadil aijalish ni star or not and you too you need grow up lazima utambue umuhim wa ndoa na wote muwe tayar kulinda ndoa yenu