Tumefundishwa katika Biblia kushukuru kwa kila jambo,nami nashukuru kwa hili kwa kuniona na kunitambua,asante dada Asia Idarous Khamsin.
The great mara baada ya kufika maeneo ya chuo hicho ubungo,nikihojiwa na waandishi juu ya chuo hicho cha rafiki yangu Emmanuel Myamba a.k.a pastor myamba,alichokianzisha kwa lengo la kutoa mafunzo kwa watu mbalimbali wanaotaka kuingia katika filamu.Kwa ufupi Myamba ni rafiki yangu tangu tunasoma wote form five na six Jitegemee high school kipindi hicho mimi tayari nilikuwa naigiza kitambo hivyo mara baada ya kumaliza shule nilimtambulisha rasmi katika sanaa hii ya filamu na nikampa staili yake ya UCHUNGAJI,ambayo iliwavutia wengi mpaka leo wengi hujua ni mchungaji wa ukweli,wakati anaanza anza alikata tamaa kidogo lakini nilimsihi unapoona unakata tamaa jua mafanikio yako mlangoni,nikamsihi asonge mbele tizama leo sasa anaamini maneno yangu ambayo Mungu kamsimamia kutokana na yeye aliwezeshwa katika filamu basi nae kafungua chuo kwa ajili ya kuwasaidia elimu wengine,chuo hicho kinaitwa ''TANZANIA FILM TRAINING CENTER''lakini pia leo hii ana kampuni yake iitwayo ''BORN AGAIN FILM COMPANY''inayotengeneza filamu na kusambaza..Hongera sana Myamba Mungu azidi kukusimamia.
Nikisisitiza kuwa kama sisi tulivyoanzia ktk vikundi kujifunza basi na wasanii wengine waje hapa kupata elimu juu ya uigizaji na si kuingia tu ktk film industry wakati hujui lolote.
Waalikwa tukiwa ndani sasa...
Meza kuu,kutoka kushoto ni Baucha,Myamba,mwakilishi wa katibu mkuu Basata,na Makubi ambaye ni mratibu wa chuo hicho.
Ukisomwa ujumbe maalum wa mgeni rasmi toka Basata.
The great kama mmoja wa walezi na mshauri wa chuo hicho nilipewa nafasi ya kusema machache kwa wanafunzi na tasnia kwa ujumla.
Wanafunzi wakiwa na uniform zao safi kabisa lakini pia humu ndio darasa lao,wanasoma katika air condition,
Bosi wa chuo Pastor Myamba akikabithiwa kibali toka Basata kama ishara ya kwamba anatambulika rasmi na mamlaka husika serikalini.
Wosia toka Basata...msipende kukatishana tamaa na kuharibiana,Basata ipo kwa ajili yenu na ndio walezi na washauri wakuu wenu.
Cheti cha usajili..
Kibali...
Maneno yangu The great kwa wanafunzi yalikuwa;
SANAA BILA ELIMU NI SANAA ILIYODUMAA,SANAA YENYE ELIMU NI SANAA ENDELEVU,VIYVO HIVYO KIPAJI PASIPO ELIMU NI GIZA TOTORO,KIPAJI CHENYE ELIMU NI NURU ING'AAYO.NDIO MAANA HATA BIBLIA INASEMA MSHIKENI SANA ELIMU MSIACHE AENDE ZAKE,LAKINI PIA ELIMU PASIPO KIPAJI NI KAZI BURE,BORA USOMEE KITU AMBACHO NI KARAMA YAKO,mfano kama una kipaji cha uchoraji basi somea uchoraji na si uigizaji usijepoteza mda wako bure,ukiviweza vyote hivi basi zingatia nidhamu..wanafunzi walinipigia makofi bila shaka walinielewa.