Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Feb 14, 2012

EMMANUEL MYAMBA AZINDUA RASMI CHUO CHAKE CHA FILAMU(TANZANIA FILM TRAINING CENTER,,TFTC)

The great mara baada ya kufika maeneo ya chuo hicho ubungo,nikihojiwa na waandishi juu ya chuo hicho cha rafiki yangu Emmanuel Myamba a.k.a pastor myamba,alichokianzisha kwa lengo la kutoa mafunzo kwa watu mbalimbali wanaotaka kuingia katika filamu.Kwa ufupi Myamba ni rafiki yangu tangu tunasoma wote form five na six Jitegemee high school kipindi hicho mimi tayari nilikuwa naigiza kitambo hivyo mara baada ya kumaliza shule nilimtambulisha rasmi katika sanaa hii ya filamu na nikampa staili yake ya UCHUNGAJI,ambayo iliwavutia wengi mpaka leo wengi hujua ni mchungaji wa ukweli,wakati anaanza anza alikata tamaa kidogo lakini nilimsihi unapoona unakata tamaa jua mafanikio yako mlangoni,nikamsihi asonge mbele tizama leo sasa anaamini maneno yangu ambayo Mungu kamsimamia kutokana na yeye aliwezeshwa katika filamu basi nae kafungua chuo kwa ajili ya kuwasaidia elimu wengine,chuo hicho kinaitwa ''TANZANIA FILM TRAINING CENTER''lakini pia leo hii ana kampuni yake iitwayo ''BORN AGAIN FILM COMPANY''inayotengeneza filamu na kusambaza..Hongera sana Myamba Mungu azidi kukusimamia.
Nikisisitiza kuwa kama sisi tulivyoanzia ktk vikundi kujifunza basi na wasanii wengine waje hapa kupata elimu juu ya uigizaji na si kuingia tu ktk film industry wakati hujui lolote.
Waalikwa tukiwa ndani sasa...
Meza kuu,kutoka kushoto ni Baucha,Myamba,mwakilishi wa katibu mkuu Basata,na Makubi ambaye ni mratibu wa chuo hicho.
Ukisomwa ujumbe maalum wa mgeni rasmi toka Basata.
The great kama mmoja wa walezi na mshauri wa chuo hicho nilipewa nafasi ya kusema machache kwa wanafunzi na tasnia kwa ujumla.
Wanafunzi wakiwa na uniform zao safi kabisa lakini pia humu ndio darasa lao,wanasoma katika air condition,
Bosi wa chuo Pastor Myamba akikabithiwa kibali toka Basata kama ishara ya kwamba anatambulika rasmi na mamlaka husika serikalini.
Wosia toka Basata...msipende kukatishana tamaa na kuharibiana,Basata ipo kwa ajili yenu na ndio walezi na washauri wakuu wenu.
Cheti cha usajili..
Kibali...
Maneno yangu The great kwa wanafunzi yalikuwa;SANAA BILA ELIMU NI SANAA ILIYODUMAA,SANAA YENYE ELIMU NI SANAA ENDELEVU,VIYVO HIVYO KIPAJI PASIPO ELIMU NI GIZA TOTORO,KIPAJI CHENYE ELIMU NI NURU ING'AAYO.NDIO MAANA HATA BIBLIA INASEMA MSHIKENI SANA ELIMU MSIACHE AENDE ZAKE,LAKINI PIA ELIMU PASIPO KIPAJI NI KAZI BURE,BORA USOMEE KITU AMBACHO NI KARAMA YAKO,mfano kama una kipaji cha uchoraji basi somea uchoraji na si uigizaji usijepoteza mda wako bure,ukiviweza vyote hivi basi zingatia nidhamu..wanafunzi walinipigia makofi bila shaka walinielewa.

11 comments:

Anonymous said...

HONGERA SANA JAMANI NYIE NI VIJANA WADOGO SANA LAKINI MNAFANYA MAKUBWA MUNGU AWABARIKI SANA NA MPENDANE ZAIDI CYO NJE TU MIDOMONI BALI MPENDANE NA NDANI YA MIOYO YENU.UNAFIKI CYO KITU KIZURI JAMANI KAMA MTU KAFANYA JAMBO JEMA MPENI HONGERA ZAKE HAKIKA MTAONA MKONO WA BWANA UKIWA JUU YENU KUNA BINADAMU WANAFIKI SANA WANAWEZA KUKUCHEKEA UKIWA NAO MUNGU HAPENDI BORA MTU KAMA HAKUPENDI AKUONYESHE NA CYO UNAKUWA MNAFIKI BILA SABABU KILA LA KHERI MIYAMBA NA BRO KANUMBA MUNGU AWATANGULIE MANA NAAMINI MAFANIKIO HAYAJAJA TU MMEJITUMA NDO MANA MPO HAPO MMLIPO LEO HII.MIMI PENDA NYIE SANA JAMNAI

getrude said...

HONGERA SANA JAMANI NYIE NI VIJANA WADOGO SANA LAKINI MNAFANYA MAKUBWA MUNGU AWABARIKI SANA NA MPENDANE ZAIDI

getrude said...

HONGERA SANA JAMANI NYIE NI VIJANA WADOGO SANA LAKINI MNAFANYA MAKUBWA MUNGU AWABARIKI SANA NA MPENDANE ZAIDI

Anonymous said...

nimesoma hii habari imenivutia sijui niende ni kasomee? lakini nina aibu sana pia siwezi ni kaongea saana maneno yote yana nitoka kabisa! alafu mie sio muongeaji, nahisi nita chemka kwenye mambo ya kuigiza! ila napenda!ebu nishauri kanumba?

Milka Richard said...

Hongereni sna,Myamba ni creative sna.Hiyo idea ya kuanzisha chuo na kuwa msambazaji wa kaz zenu ni nzuri sna.Utatoka tu Myamba,na huo ni mwanzo mzuri.Hakika Mungu amutupi mja wake,na hizi ndo mbegu njema mnazovuna ss mlizopanda kwenye mashamba yenu.Mbarikiwe sna Kanumba,zaid mdumishe upendo,na kupongezana wasanii kwa wasanii.unapoona mwenzio kafanya jambo jema,mpe hongera.na co kumpiga vijembe.chuk na fitina hazifai.Zinabomoa na kuludisha nyuma tasinia yenu ya filam.

Anonymous said...

Ongera sana. Mungu awe pamoja na nyie

Anonymous said...

Kanumba naomba kujua ni muda gani, nina kipaji mwanamke mie ila najua mtanipiga chini wabongo but msiwe naofu ntawafata tena nikishafanikiwa. nilishakuomba nafasi ukadengua na email hujibu nisawa tu ila nambie ni muda gani nipange kwenye likizo yangu nijiwahi. nilimsikia clouds fm ila miaka au miezi haielezewi.Kila la kheri Emanuel

Patience Paty said...

Hongera!!! mashari mwa kongo ya Kidemocratia, tuna wapenda sana waigizaji wa Filamu wa Tanzania, zaidi sana Steven Kanumba, Pastor Myamba ambaye amekuwa akionesha ukakalavu wake.

Patience Paty said...

Hongera sana. Tunawapenda waigizaji wa Filamu wa Tanzania. Mjini Butembo pa Congo ya Kidemocratia 95% ya wakaaji wanatamani kuliona kundi lenu likifika Butembo

Patience Paty said...

Hongera sana. Tunawapenda waigizaji wa Filamu wa Tanzania. Mjini Butembo pa Congo ya Kidemocratia 95% ya wakaaji wanatamani kuliona kundi lenu likifika Butembo

Patience Paty said...

Alakini kwa nini unapana anwani za internet sizizo za kweli? mara ninapotaka andika ujumbe huwa ujumbe unarudi kwangu kwamba una fail. kwa nini hivyo? jamani!!! ama siyo anwani yako, ama hutaki maujumbe zatu?? Aksanti, lakini inatuma sana!!!
Samahani kama ujumbe huu unakwaza moyo wako