Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Nov 1, 2011

IN ACCRA-GHANA.......................

Monalisa kazini akiwa na CHRISS ATTOH,
Huyo dada ndiye main character uigizaji wake naufananisha na Leleti Khumalo(Sarafina) yaani anakamua ni balaa.
Kwa taarifa niliyopewa hapa huyu ndiye aliyechukua tuzo ya best cinematograph katika American cinematograph awards mwaka jana anaitwa CHASE BOWMAN mlioko huko Marekani mnaweza kunisaidia hapo.
Picha ya pamoja katika kuwaaga CHRISS na OMARY ambao wamemaliza scene zao na hapo hapo wanaelekea airport kwenda Nigeria kuanza kushoot series ya Tinsel session two.Watu wako busy na kazi hawana mda wa majungu,chuki,roho mbaya,roho ya kwanini,kupondana na kutukanana mda wote wanawaza mafanikio tu, I wish hii hali ingekuwa kwetu bongo maana hali iliyopo siku hizi imegeuka kuwa ndio utamaduni wetu.
Monalisa kazini......

Monitor...
Pusher kazini.....


MONA NA CHRISS MARA BAADA YA SCENE KUISHA.

12 comments:

Happy Ole Ngambi. said...

Ni balaa jamani!cha msini na wewe ujifunze mambo mazuri hapo sasa hapo angekuwepo uwoya oh ni balaa!GOD BLESS YOU KILA MARA MSHUKURU MUNGU KWA HAYO YOTE AKUTENDEAYO KILA SIKU.

Anonymous said...

Kanumba hacha hizo; umeenda mahali siku mbili tu unasema hawana majungu. Are you sur?. Mi navojua waafirka woote ndo tulivyo.

Hata wadhungu wana majungu ya staili yao.

Binadamu ni wagumu kaka yangu si Tz tu.

Anonymous said...

Mbona sijaona big names kwenye hiyo shooting?? Where is John Dumelo? Where is Van Vicker, Where is NAdia and the rest.

dogojohnson said...

kaka hongera sana nakukubali kwa sna yaani kila nikianga wakati unatoka na na filam ya johari na sikitiko langu naona umepiga hatua kubwa sna kuelekea mafanikio ya kina will smith kaka, big up kwa hilo wanaoponda waache waponde mafanikio ni yako na tanzania hili coz wewe ni mmoja wa wawekezaji wakubwa kwani umeweza kutoa ajira kwa wasanii wachanga. Its Me Johnson Matembo Mtanzania Mzalendo.

Anonymous said...

Steve, Unajua bongo si wote wanakuponda, wengine wanajaribu kukushauri ila wewe unatafsiri tofauti yaani chuki! Hakuna akuchukiaye ila watu wanataka ufike mbali, maigizo yako yafanane na ukweli, wenzako huko Ghana na Nigeria wako mbali sana katika uigizaji, iga mfano wao!!! Wewe inaonekana hautaki kujifunza kupitia watu, hamna ajuaye kila kitu, haiwezekani wewe huyo huyo ndio main character huyo huyo Director, waachie wenye fani hiyo wafanye kazi yao, mfano mzuri ni mnapoigiza movie za kibongo mavazi yenu hayafanani na mazingira unayoigizia, unaigiza uko ofisini umevaa mavazi yenu yale ya kung'aa kama wacongoman wa muziki!! Badilikeni sisi tupo nyuma yenu, unaigiza uko serious ofisini unamiliki biashara kubwa na contacts kubwa tu halafu sikioni hereni!! Hizo ni movie za America sio bongo!!! Umevaa suti unaenda kazini suti yenyewe za wanamuziki maua kibaooooooo, angalieni wenzenu hata Kenya muone tofauti.

Nimeandika haya kwa ushauri tu kwakuwa napenda mfike mbali katika tasnia ya filamu.

Ni hayo tu kaka.

Anonymous said...

Waliopa US wakusaidie nini?ukitaka information unaingiz kwenye internet una google hilo jina
Acha ushamba ,unatakiwa kuwa mjanja bwana

Esther kanda ya ziwa. said...

Hongera broo tunakuombea wewe na Mona muwakilishe vizuri.

Anonymous said...

shummepiga hatua sana kaka ila wewe ni kiburi siku zote haujibu msm za watu humu blogini,nimetoka kuangalia muvie yako because of u ni nzuri mmejitahidi ila vimakosa vidogo vidogo,kweli scene fupi fupi nimependa sana hata devil kingdom nayo mmefanya vizuri ila tatizo lako hamtaki kukubali kukosolewa ili upone na uendelee na kazi nzuri kubali yote hauna maadui ila unahisi wanaokukosoa ni maadui zako ni Hapana wanapenda maendeleo yako ndiyo maana wankuambia,all in all mnafanya vizuri kwenye fani big up

Anonymous said...

yeees dis is what i was dreaming abt
keep it up u shining stars of tz!!!!

Anonymous said...

vipi mambo ya umeme huko kama bongo au ni bata tu full time?

Anonymous said...

hongera kanumba. endelea kuwa positive. mad love

Anonymous said...

nadhani kaka umepewa maoni mazuri sana na yakitolewa kama hivi ni vizuri uka-acknowledge hata kama hutayafanyia kazi. mtu anafurahi kuona kwamba kanumba ame-acknowledge comment yake. wenzetu wanakuwa na publicity managers wakuweza kuangalia kuna nini kwenye habari,kwenye blog nk sasa kama hatujafika hapo basi kaka jitahidi kuangalia na kufanyia kazi comments ulizopewa. tunakupenda ndo maana tunatumia muda wetu kutoa maoni. asante