Ugeni kutoka benki ya Dunia ulitembelea kata ya keko Wilayani Temeke Mkoa wa Dar es salaam kuiangalia jinsi ilivyo kabla ya kuiboresha kimiundombinu kwa kuyapitia maeneo yatakayoboreshwa ikiwa ni pamoja na Barabara za lami, Barabara za Changarawe, Barabara za kwenda kwa miguu, mifereji ya maji ya Mvua, Vyoo vya Umma (Public Toilets) Taa za Barabarani na vituo vya kukusanyia taka ngumu (Solid Waste Collection Points)
Picha ya pamoja ikimuonesha Senior Vice President wa Benki ya Dunia (Mdada Mwenye Blauzi ya Pink, wa nne toka kulia Mstari wa mbele) na Mwenyeji wake Diwani wa Kata ya Keko Mh. Francis Mtawa (Wa pili toka kulia mbele) pamoja na Mstahiki meya wa Manispaa ya Temeke Jerome Bwanausi (Mwenye tai).
Wakiwa pamoja na Baadhi ya wajumbe wakazi wa keko wenye fulana nyeupe
Wakitembelea moja ya Barabara zitakazoboreshwa (Njia inayounganisha Keko Mwanga na Keko Magurumbasi)
Diwani wa Kata ya Keko Mh. Francis Mtawa (Kulia) Pamoja na Mh. Ally Kinyaka, mwenyekiti wa kamati ya mipango miji manispaa ya Temeke
Barabara ndo iko hivi? Kweli inahitaji kuboreshwa.
Hapa wakielekea kupanda magari baada ya kutembelea maeneo husika