Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Feb 14, 2010

FC Lupopo yatuadhiri watanzania

Mrisho Ngassa wa Dar Young African (Yanga) akichuana na mchezaji wa St. Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika mchezo uliopigwa katika uwanja Mkuu wa Taifa jana. Lupopo waliondoka na kitita cha magori 3-2 dhidi ya Yanga, ambapo katika mchezo mwingine watarudiana katika mji wa lubumbashi wiki mbili zijazo.

Katika mchezo wa jana Yanga ilicheza kandanda safi sana labda pengine kama sio umakini wa washambuliaji wa Yanga wangeweza kutoka na jumla ya magori zaidi ya 5.

Napenda pia kuwaasa watanzania wenzangu hebu tuacheni usimba na uyanga katika mashindano ya kimataifa kwa manufaa ya soka la nchi yetu kwani kila siku tutakuwa tunatia aibu katika mashindano haya ya kimataifa. mi nadhani kama sio support ya baadhi ya mashabiki wanaoaminika kuwa wa simba wale jamaa sidhani kama hata wangekuwa na nguvu ya kushinda hata hayo magori matatu kwa jinsi walivyokuwa wameshikwa. Jamani tuipende NCHI yetu!!

1 comment:

Anonymous said...

YANGA sio WATANZANIA ACHA UFALA!