Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

May 22, 2011

THE GREAT ZIARANI SHINYANGA NA OXFAM...

Mara baada ya kuchaguliwa kuwa balozi wa OXFAM the great nimeanza kazi rasmi ya kuzunguka maeneo kadhaa hasa ya vijijini ambako kuna watu wanaishi maisha ya shida na tatizo la chakula ni kubwa sana,toka juzi nilianzia mkoa niliozaliwa(SHINYANGA) nikaenda ktk wilaya ya kahama kata ya MONDO na kijiji cha MONDO.....hali iko hivi.... Hili ni shamba la mpunga lililopo kijijini ambalo kutokana na ukame mazao yamekauka kabisa na hakuna chakula ukizingatia huu ndio msimu wa mavuno lakini hakuna cha kuvuna.

The great nikiwa na viongozi wangu toka OXFAM tukiongea na wanakijiji juu hali ngumu hapo

Ukisikia story za akina mama hawa utalia,,mvua hakuna hivyo mazao hayastawi,inabidi wafanye kazi za vibarua ili kupata japo kilo moja ya unga wale na watoto wao.

Wakati sisi mjini tunakula milo mitatu au zaidi wenzetu ni mlo mmoja tu na hawashibi.

Pia niliombwa kusalimia shule hii nami nikafanya hivyo lakini pia kuwatia moyo katika kilimo kwani siku hizi vijana wote wanakimbilia mjini hivyo walimaji wanakosekana.

The great na walimu wa shule hiyo

Hapo ni saa mbili asubuhi wakati mjini watoto wetu wanapata kifungua kinywa kizuri hawa asubuhi hii wanakula machungwa mabichi kabisa baada ya hapo chakula ni saa kumi jioni.

Tizama mwenyewe,unadhani hata akiwa darasani yataingia??je unategemea atashika namba ngapi darasani?

Jamani kila mtu ashike nafasiyake na tusaidiane tuache chuki....mfumo wa chakula wenye usawa na haki kwa Tanzania unawezekana......

11 comments:

Anonymous said...

Hakika inasikitisha sana!! na ukweli hili ndio tatizo kuu la kwe2 na unashngaa kuona viongozi wanapoteza muda kwa malumbano yasonamana na wanaacha wajibu wao wa msingi hakika inasikitisha na kukatisha tamaa na ukweli uwezo wa kujumuika pamoja kama watanzania na kuhakikisha familia zisizo na uwezo zinawezeshwa angalau kwa mlo inawezekana basi tungeweka kuwa hii ndio ajenda ye2 kubwa kuliko ajenda yeyote ile.Mbona mambo yaso nalazima tunaweza kuyafanya mpaka wa2 wa duniani wakashangaa na uwezo we2. kwann tushindwe na hili. Udhati nakupongeza kwa kukubali kuwa balozi mana nahisi roho yako inaendana na kazi ulopewa yaani mtumishi wa watu kwa ajili ya wa2 lakini pia ni fursa itayokupatia ujuzi utakaokusaidia kwenye shughuli zako za kila siku za utengenezaji wa filamu na kuelimisha. Mungu awape nguvu za kusaidia utatuzi wa matatizo ya jamii inaowazunguka. "PANAPO NIA PANA NJIA"

Anonymous said...

kazi nzuri kanumba mungu akubariki endelea kuwasaidi hawa watu wa vijijini na mungu atakuongezea na kukubariki asnte

Anonymous said...

i believe all are possible ila serikali yetu jamani inatia aibu sana.mashangingi wanayo endesha gharama zake zingeweza kusaidia vijijini.tatizo watanzania tumekuwa wabinafsi sana.hao watoto hawawezi kufanya vizuri darasani sababu wanakosa lishe bora.hayo ndio maisha bora kwa kila mtanzania kwa kukosa mlo kwa siku.sijui kama tutafika.

gosbety said...

kaka, Mungu akutie nguvu ktk hizi harakati maana bila mkono wake hakuna litakalofanyika. usikate tamaa, endelea kuwa na moyo huo wa kuwa sauti ya wanyonge na maskini. kila la kheri

Anonymous said...

Hongera sana kaka kwa moyo wako, hakika Mungu akutie nguvu katika kuyatenda hayo jamani, ukiwa mjini huwezi kujua ni jinsi gani watu nwanateseka huko vijijini kwa kweli, yani umetufurahisha sana wewe kama msanii una uwezo mkubwa wa kufanya hata movie ambayo itaihamasisha serikali katika kuchangia njaa hii jamani.Mungu akubariki sana na akutie nguvu siku zote.Hakika Ubalozi unakufaa kaka wewe, na unafana na kazi yako, fanya kila njia kuielimisha jamii na hata serikali katika hili.Tutakusupport kabisa.

X-tina J said...

dah! kiukweli hizi picha zimenitoa machozi.hayo maisha nayajua vizuri nimeyapitia na 99% ya ndg zangu ndo hali zao hizo.eeh Mungu muumba wa mbingu na nchi nusuri waja wako na pia tupe viongozi wenye utu na busara

Anonymous said...

kwa kweli inasikitisha sana hongereni sana kwa kutembelea maeneo hayo na kutujunza maisha ya watanzania wenzetu,asante

Anonymous said...

ndio hapo uone tanzania baadhi ya mikoa watu wanapata shida sn ya chakula alafu mafisadi wanaachiwa tu na serikali kuchekezea kwa mambo mengine yasiyo ya msingi baada ya kuwasaidia watu kama kawaa kwa kweli inaumaa sanaa acha tu

meggie impostra