Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Jan 29, 2011

THE GREAT NDANI YA VOICE OF AMERICA(VOA)WASHINGTON DC.

Nimepata mwaliko wa kutembelea voice of America na kufanya interview tatu tofauti yaani ya redio,ya TV kwa lugha ya kiswahili na ingine kwa lugha ile yetu ya Kiingereza chini ya mtangazaji mahiri kabisa MR.SUNDAY SHOMARI,Baada ya interview nilipewa zawadi nzuri ambayo nami nachukua nafasi kushukuru sana kwa zawadi na kupewa heshima hii ya kukaribishwa VOA sehemu kubwa ya kimataifa na yenye heshima. Nikivarishwa mic tayari kwa interview
Sunday,the great na dada sharifa
Bosi DR.Mwamoyo Hamza,the great na dada sharifa

Sunday Shomari akijiandaa kuanza kipindi
The great nikirekodi tangazo la VOA yaani mimi steve kanumba na unatizama Swahili VOA
Kibao kikielekeza unakostahili kwenda
Sunday Shomari na Steven Kanumba katika logo ya VOA
Interview ikiendelea
Kwa raha zangu nikijibu maswali kwa uyakinifu
Taa za production zikifanya kazi yake kwa juu
Camera zikiwa sawia kabisa kwa kazi
Hii ndio VOICE OF AMERICA
The great na Father Bandawe alikuja kuniona ninavyofanya interview
The great na producer Duane Collins
Nikipokea zawadi yangu toka kwa DR.Mwamoyo Hamza ambaye ndiye mkuu wa kitengo cha kiswahili VOA.Nikashukuru sana kwa hili.
SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KABISA ZIWAENDEE:-Dada Sharifa Kalala(WORLD BANK),DR.Mwamoyo Hamza(VOICE OF AMERICA),Sunday Shomari(VOICE OF AMERICA)Mungu azidi kuwabariki.

SNOW TENA WASHINGTON DC....

Baada ya kumaliza ka ziara kangu Hollywood nimerudi DC na kukuta snow imemwagika kwelikweli,kwa wengine yaweza kuwa kitu cha kawaida ila kwangu mimi niliyetoka bongo kwenye joto ni ADVENTURE.... Dada Sharifa Kalala akiisikilizia jinsi inavyomwagika

Dada Sharifa na The great

EEEEEHH mwanawaneeeeeeeeeh

Hali halisi ilivyo huku..

MWISHO NIMEMALIZIA ZIARA YANGU KWA HAPA LOS ANGELES MAENEO YA UKUMBI WA STAPLES CENTER.

Kwa kumalizia ziara yangu ya kutembelea hollywood nimetembelea ule ukumbi maarufu wa michezo mbalimbali hasahasa basket ball kutizama mchezo wa HOCKY unaopendwa sana hapa USA,Kikubwa kilichonifanya nije hapa si kwa kupenda huu mchezo wa HOCKY ila ni umaarufu wa huu uwanja,kwa kifupi uwanja huu ndio alikuwa akifanyia mazoezi MICHAEL JACKSON kwa ajili ya show yake ya THIS IS IT,lakini pia humu ndipo mwili wake ulipoagwa mara baada ya kifo chake,Pia ukumbi huu ndio timu kubwa kama Lakers na LA KINGS hucheza mechi zake..nami nikaona ni vyema nije niione jinsi ulivyo unaitwa STAPLES CENTER. Nikiingia

Pengine unaweza shangaa kwanini napiga picha na sanamu hili la mcheza basket ball maarufu na mkongwe mwenye heshima kubwa katika mchezo huu,pengine katika maisha yangu naweza nisije onana nae na kupiga nae picha ila alininivutia kwa umahiri wake katika mchezo huo,lakini zaidi ni pale alipojigundua kuwa ni muathirika wa ugonjwa wa UKIMWI akiwa ni star mkubwa duniani aliamua kujitangaza hadharani jamii imjue kama kaathirika,ujasiri huu ndio unaonifanya nipige picha katika sanamu lake hili kama mtu yoyote yule anavyoweza kufanya,mara baada ya kujitangaza jamii ilishtuka kwa taarifa hizi lakini makampuni mengi yalijitokeza kumpa misaada na akastaafu mchezo huu akiwa kaweka rekodi hii,hadi leo bado anadunda akiwa na afya njema,aliwai pia kushiriki katika video mojawapo ya Michael Jackson,,huyu ni MAGIC JOHNSON.

Uwanjani

Monitor ya juu katikati ya kiwanja

Huu ndio uwanja wa Staples center

Mr.Jingo na mimi uwanjani

kwa juu waonekana hivi

Burudani mbalimbali

wasichana hao kazi yao ni kusafisha uwanja kwa kuondoa barafu zilizoyeyuka uwanjani maana mchezo huu unachezwa katika kiwanja chenye barafu huku wachezaji wakitumia viatu vya matairi kukimbia.

Tizama uwanja ulivyo hakika kodi za wananchi zinafanya kazi

Nikifatilia mchezo huo

Huu ndio mchezo wenyewe wa Hocky

Watu wakitazama monitor ya juu pale inaporudia goli lililofungwa....

ZIARA YANGU HOLLYWOOD...4 (BEVERLY HILLS)

Mafuvu yaliyomo madame tussaunds yakutengenezwa ambayo pia ndiyo hutumika kwa shooting,mafuvu yanayoonekana katika movie huwa sio halisi,inasemekana yanatengenezwa kwa unga unaotengeneza mishumaa alafu wanayapaka rangi na kuwa hivyo unavyoona.


Kama umeshatazama FRESH PRINCE ya Will Smith au comedy za Eddy Murphy utaona kuna sehemu huwa mnene,basi hutumia mfano wa ma plastic haya ili kuonesha sehemu ya unene.Baada ya hapa nilitembelea sehemu ambapo matajiri na ma celebrity wakiwemo wa movie hupenda kuishi lakini ndiko kuliko na maduka ambayo mara nyingi wao hupenda kufanya shoping zao huku,maduka haya vitu vyake ni bei ghali sana mtu wa kawaida ni aghalabu sana kushop huku maana ni sehemu expensive hata kuishi,panaitwa BEVERLY HILLS,na maduka yamo RODEO DRIVE.


Maduka ambayo hupenda kununua nguo ni haya hapa..










Mwenyeji wangu Mr.Jingo(mzee wa Carlfonia) na mimi katika mitaa ya beverly hills.


Baadhi ya vitu ambavyo inasemekana ma star wa kike hupenda kununua ni kama hivi....














Alama ya eneo lenyewe.


BAADHI YA MASWALI NILIYOULIZA WARNER BROTHER STUDIO&UNIVERSAL STUDIOS:-1.Je hollywood mnachukua mda gani kushoot filamu,JIBU:-miezi 2 mpaka 3.,,editing nayo inategemea na aina ya movie zipo zinazochukua miezi 2,na zingine 6,maana kuna vitu vingi vya kuangalia ikiwemo special effect,sound,nk.


2.Je mnapataje waigizaji hasa wapya?JIBU:-Tuna tangaza na watu wanakuja katika interview lakini pia kuna makampuni yanayohusika na casting wakati mwingine tunawapa hali halisi ya watu tunaowaitaji alafu wao hutafuta na kutuletea.


3.Mtu kama anataka kucheza movie hollywood kampuni yoyote afanyaje?JIBU:-Akisikia matangazo afanye hima kujaribu bahati yake au pia anaweza kujisajili katika hizo kampuni za casting,au anaweza kututumia Head shot(picha zake full na ya karibu) na CV na mawasiliano yake.


4.Mbona mimi mwaka 2007 niliacha hapa headshot,cv na mawasiliano yangu lakini sijawai itwa?JIBU:-Kila mtu ana bahati yake na wanaotuma hivyo vitu ni wengi kulingana na idadi inayoitajika pia sio lazima ukituma hivyo lazima uchukuliwe wewe,yoyote anawezachukuliwa kulingana na director anataka nini,lakini pia sio wote hupitia njia hizi,hollywood kila mtu kaingia kwa njia yake..tizama mtoto wa will smith katika ile movie ya Karate Kid kapata connection kupitia baba yake,kuwa na connection nalo ni muhimu,Samuel Jackson kasota sana kabla ya kuwa hapo alipo ameigiza sana katika stage lakini sasa ni star wa dunia.


5.Movie ikishakamilika inapitia hatua zipi mpaka kuwa katika DVD?JIBU:-Hupelekwa sinema huko ndiko pesa nyingi hutengenezwa,hukaa huko miezi 2 na zaidi kama movie imetokea kupendwa dunia nzima,baada ya hapo hupelekwa katika tv kuoneshwa ambapo hapo station husika hulipia kuonesha movie hiyo hapo napo pesa ingine hutengenezwa,mwisho kabisa ndio huwekwa katika DVD kuuzwa,dvd huwa hatua ya mwisho japo pia PIRATES nao wanaharibu soko maana unaweza kuta movie bado iko theatre lakini nchi fulani zina dvd zake.

NAISHIA HAPA MENGINE YANABAKI KWA FAIDA YANGU.

Jan 28, 2011

ZIARA YANGU HOLLYWOOD....3(WARNER BROTHER STUDIOS)

Nikiwa bado niko hapa Los Angeles maeneo ya Hollywood nimetembelea pia kampuni ingine ya utengenezaji wa filamu na Tv shows...ambayo ni WARNER BROS.na hapa ni mara yangu ya pili sasa nafika hapa,nimeuliza mengi na kujifunza mengi katika filamu. Hii ni moja ya vazi lililovaliwa na comedian Jeffrey Dean Morgan katika movie ya WATCHMEN(2009) iliyokuwa directed by Zack Snyder,na hili vazi lilibuniwa na Michael Wilkinson chini ya kampuni hii ya warner bros.

Hii ilitumiwa na OZYMANDIAS(MATTHEW GOODE) katika WATCHMEN(2009),NA KUWA DIRECTED BY ZACK SNYDER,VAZI KUBUNIWA NA MICHAEL WILKINSON

nikitazama logo ya kampuni hii

Hii ni mitaa ya kampuni hii iliyotengenezwa kwa ajili ya shooting wakiakisi mji wa Newyork,hivyo huwa hawaendi mbali ni humuhumu tu.

Sound stage 24 ambayo ndani ni location za shooting kama sebule ,jiko,chumba nk,taa,mic na camera zimefungwa kabisa kwa ajili ya kazi.

Harry potter,gari yake na mhusika mwenyewe,katika movie gari inaonekana inapaa lakini wapi ilikuwa hapo hapo tu,hayo mambo ya special effect.

pikipiki ya ajabu na hiyo ndege vilitumiwa na director STEVEN SPIELBERG katika HOVERCOPTER

Kupitia movie ya Harry Potter niliuliza maswali mengi kitu kilichopelekea msimamizi wangu kunionesha kwa vitendo jinsi kile kifimbo kilivyokuwa kinabadilishwa hakika nilipata elimu sawia ambayo nisingeipata pengine zaidi ya hapa.

Akinipatia maelekezo kwa uyakinifu zaidi.

Ndani ya zile SOUND STAGE kwa ndani kuko hivi,

Taa zimefungwa kwa juu na mic ambapo unaweza kushoot wakati kule nje watu hawasikii wala ninyi ndani hamsikii kelele yoyote.

Ikanibidi nipate picha kidogo

Baadhi ya tuzo ambazo kampuni hii imeshanyakua NDANI YA HOLLYWOOD

Nikielekea katika kitengo kingine kujionea ujuzi wa watu hawa.

Mojawapo ya maswali niliyouliza ni:Katika scene za kukiss na romance huwa wanafanya kweli? jibu lake huwa wanafanya kweli isipokuwa scene za kitandani hutegemea director anataka nini,mfano kama anataka waonekane wanafanya mapenzi sana basi kuna angle ambazo huweka camera na kuwaamuru wahusika kuact kama wanafanya tendo ili katika TV ionekane ni kweli..JE ni kweli HOLLYWOOD wanatoa filamu moja kwa mwaka au msanii mmoja kuigiza filamu moja kwa mwaka?..JIBU ni UONGO,kuna makampuni kadha wa kadha kama universal studio,warner bros,disneyland,columbia nk yote yanatengeneza film sasa itawezekanaje hollywood itoe filamu moja?kuhusu msanii kucheza filamu moja au zaidi inategemea na mikata aliyonayo ya kazi kwa mwaka na ratiba yake kwa kila kazi mfano mwanadada GEMA ARTETON kwa mwaka jana kuna filamu zaidi ya 3 kacheza na zote nzuri ikiwemo THE PRINCE OF PERSIA.ila haimzuii kucheza idadi ya anavyoweza.Maswali mengine nitawaandikia wakati mwingine..