Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Jan 29, 2011

ZIARA YANGU HOLLYWOOD...4 (BEVERLY HILLS)

Mafuvu yaliyomo madame tussaunds yakutengenezwa ambayo pia ndiyo hutumika kwa shooting,mafuvu yanayoonekana katika movie huwa sio halisi,inasemekana yanatengenezwa kwa unga unaotengeneza mishumaa alafu wanayapaka rangi na kuwa hivyo unavyoona.


Kama umeshatazama FRESH PRINCE ya Will Smith au comedy za Eddy Murphy utaona kuna sehemu huwa mnene,basi hutumia mfano wa ma plastic haya ili kuonesha sehemu ya unene.Baada ya hapa nilitembelea sehemu ambapo matajiri na ma celebrity wakiwemo wa movie hupenda kuishi lakini ndiko kuliko na maduka ambayo mara nyingi wao hupenda kufanya shoping zao huku,maduka haya vitu vyake ni bei ghali sana mtu wa kawaida ni aghalabu sana kushop huku maana ni sehemu expensive hata kuishi,panaitwa BEVERLY HILLS,na maduka yamo RODEO DRIVE.


Maduka ambayo hupenda kununua nguo ni haya hapa..










Mwenyeji wangu Mr.Jingo(mzee wa Carlfonia) na mimi katika mitaa ya beverly hills.


Baadhi ya vitu ambavyo inasemekana ma star wa kike hupenda kununua ni kama hivi....














Alama ya eneo lenyewe.


BAADHI YA MASWALI NILIYOULIZA WARNER BROTHER STUDIO&UNIVERSAL STUDIOS:-1.Je hollywood mnachukua mda gani kushoot filamu,JIBU:-miezi 2 mpaka 3.,,editing nayo inategemea na aina ya movie zipo zinazochukua miezi 2,na zingine 6,maana kuna vitu vingi vya kuangalia ikiwemo special effect,sound,nk.


2.Je mnapataje waigizaji hasa wapya?JIBU:-Tuna tangaza na watu wanakuja katika interview lakini pia kuna makampuni yanayohusika na casting wakati mwingine tunawapa hali halisi ya watu tunaowaitaji alafu wao hutafuta na kutuletea.


3.Mtu kama anataka kucheza movie hollywood kampuni yoyote afanyaje?JIBU:-Akisikia matangazo afanye hima kujaribu bahati yake au pia anaweza kujisajili katika hizo kampuni za casting,au anaweza kututumia Head shot(picha zake full na ya karibu) na CV na mawasiliano yake.


4.Mbona mimi mwaka 2007 niliacha hapa headshot,cv na mawasiliano yangu lakini sijawai itwa?JIBU:-Kila mtu ana bahati yake na wanaotuma hivyo vitu ni wengi kulingana na idadi inayoitajika pia sio lazima ukituma hivyo lazima uchukuliwe wewe,yoyote anawezachukuliwa kulingana na director anataka nini,lakini pia sio wote hupitia njia hizi,hollywood kila mtu kaingia kwa njia yake..tizama mtoto wa will smith katika ile movie ya Karate Kid kapata connection kupitia baba yake,kuwa na connection nalo ni muhimu,Samuel Jackson kasota sana kabla ya kuwa hapo alipo ameigiza sana katika stage lakini sasa ni star wa dunia.


5.Movie ikishakamilika inapitia hatua zipi mpaka kuwa katika DVD?JIBU:-Hupelekwa sinema huko ndiko pesa nyingi hutengenezwa,hukaa huko miezi 2 na zaidi kama movie imetokea kupendwa dunia nzima,baada ya hapo hupelekwa katika tv kuoneshwa ambapo hapo station husika hulipia kuonesha movie hiyo hapo napo pesa ingine hutengenezwa,mwisho kabisa ndio huwekwa katika DVD kuuzwa,dvd huwa hatua ya mwisho japo pia PIRATES nao wanaharibu soko maana unaweza kuta movie bado iko theatre lakini nchi fulani zina dvd zake.

NAISHIA HAPA MENGINE YANABAKI KWA FAIDA YANGU.

14 comments:

Anonymous said...

HAYA NDIO MAMBO TUNAYOPENDA KUONA NA KUJIFUNZA ANAYEPONDA NI CHUKI TU HIYO SI UNAWAJUA WABONGO

Anonymous said...

SAFFFFFFFFFFFIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

Anonymous said...

nice my broh....

Anonymous said...

thats why you are the great kanumba

Anonymous said...

mmmmh

Anonymous said...

waoh steve?gud

Anonymous said...

hahahaha!!!!! huyo mtu mbonge mbona kama mna fanana sura au ndiyo weye umejikuza nini, natania nilikuwa nakuchukia sana kwa kubania comment sasa nimeanza kukupenda hongera sana haya ndyo mambo tunataka siyo kila siku wanaigeria

Anonymous said...

hahahaha!!!!! huyo mtu mbonge mbona kama mna fanana sura au ndiyo weye umejikuza nini, natania nilikuwa nakuchukia sana kwa kubania comment sasa nimeanza kukupenda hongera sana haya ndyo mambo tunataka siyo kila siku wanaigeria

Anonymous said...

wewe binafsi umejifunza nini?

Anonymous said...

wewe binafsi (Kanumba) umejifunza nini?

Majoy said...

Safi sana ulipo si pabaya ila ongeza juhudi.

Anonymous said...

upuuzi mtupu

Anonymous said...

safi sana uko juuu kaka

YALAEVA said...

Kaka yangu Kanuba hongera sana kwa juhudi. Ni kijana wa mfano mzuri kabisa kwa vijana wengine....ulikotoka ni mbali sana. Nakuombea baraka tele Mungu akutie nguvu kila jema unalofikiria na kutenda. Je una mpango gani kuhusu kuelimisha vijana wengine? You are a model of youth and development. Sasa mimi nakuambia kuwa huu mwaka ukimbie sana tena kwa speed ya mita mia moja. I real love and appreciate on your work...good job ong'wise! Ukikubaliana na mimi....kuhusu suala la vijana, please anzia Shinyanga. Hali ya vijana ni mbaya sana....tukumbuke nyumbani tafadhari. Hongera sana na Mungu akulinde, Amina.