Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Jan 28, 2011

ZIARA YANGU HOLLYWOOD....3(WARNER BROTHER STUDIOS)

Nikiwa bado niko hapa Los Angeles maeneo ya Hollywood nimetembelea pia kampuni ingine ya utengenezaji wa filamu na Tv shows...ambayo ni WARNER BROS.na hapa ni mara yangu ya pili sasa nafika hapa,nimeuliza mengi na kujifunza mengi katika filamu. Hii ni moja ya vazi lililovaliwa na comedian Jeffrey Dean Morgan katika movie ya WATCHMEN(2009) iliyokuwa directed by Zack Snyder,na hili vazi lilibuniwa na Michael Wilkinson chini ya kampuni hii ya warner bros.

Hii ilitumiwa na OZYMANDIAS(MATTHEW GOODE) katika WATCHMEN(2009),NA KUWA DIRECTED BY ZACK SNYDER,VAZI KUBUNIWA NA MICHAEL WILKINSON

nikitazama logo ya kampuni hii

Hii ni mitaa ya kampuni hii iliyotengenezwa kwa ajili ya shooting wakiakisi mji wa Newyork,hivyo huwa hawaendi mbali ni humuhumu tu.

Sound stage 24 ambayo ndani ni location za shooting kama sebule ,jiko,chumba nk,taa,mic na camera zimefungwa kabisa kwa ajili ya kazi.

Harry potter,gari yake na mhusika mwenyewe,katika movie gari inaonekana inapaa lakini wapi ilikuwa hapo hapo tu,hayo mambo ya special effect.

pikipiki ya ajabu na hiyo ndege vilitumiwa na director STEVEN SPIELBERG katika HOVERCOPTER

Kupitia movie ya Harry Potter niliuliza maswali mengi kitu kilichopelekea msimamizi wangu kunionesha kwa vitendo jinsi kile kifimbo kilivyokuwa kinabadilishwa hakika nilipata elimu sawia ambayo nisingeipata pengine zaidi ya hapa.

Akinipatia maelekezo kwa uyakinifu zaidi.

Ndani ya zile SOUND STAGE kwa ndani kuko hivi,

Taa zimefungwa kwa juu na mic ambapo unaweza kushoot wakati kule nje watu hawasikii wala ninyi ndani hamsikii kelele yoyote.

Ikanibidi nipate picha kidogo

Baadhi ya tuzo ambazo kampuni hii imeshanyakua NDANI YA HOLLYWOOD

Nikielekea katika kitengo kingine kujionea ujuzi wa watu hawa.

Mojawapo ya maswali niliyouliza ni:Katika scene za kukiss na romance huwa wanafanya kweli? jibu lake huwa wanafanya kweli isipokuwa scene za kitandani hutegemea director anataka nini,mfano kama anataka waonekane wanafanya mapenzi sana basi kuna angle ambazo huweka camera na kuwaamuru wahusika kuact kama wanafanya tendo ili katika TV ionekane ni kweli..JE ni kweli HOLLYWOOD wanatoa filamu moja kwa mwaka au msanii mmoja kuigiza filamu moja kwa mwaka?..JIBU ni UONGO,kuna makampuni kadha wa kadha kama universal studio,warner bros,disneyland,columbia nk yote yanatengeneza film sasa itawezekanaje hollywood itoe filamu moja?kuhusu msanii kucheza filamu moja au zaidi inategemea na mikata aliyonayo ya kazi kwa mwaka na ratiba yake kwa kila kazi mfano mwanadada GEMA ARTETON kwa mwaka jana kuna filamu zaidi ya 3 kacheza na zote nzuri ikiwemo THE PRINCE OF PERSIA.ila haimzuii kucheza idadi ya anavyoweza.Maswali mengine nitawaandikia wakati mwingine..

17 comments:

Anonymous said...

Uko juu sana Kanumba, nakufagilia sanaaaaaaaaaa. Siku haipiti bila kupita kwa blogu hii.

Anonymous said...

big up kaka kutembea ndio kujifunza.

Anonymous said...

kaka nimekusoma msalimie sana anold mwambie rafiki yake saguda anamsalimia

Do said...

Kila la heri Kanumba Ni vizuri sana kutembelea sehemu kama hizi nawe unajifunza mengi sana ambaye ukirudi nyumbani una mawazo mapya ya kuboresha zaidi kazi zako.

Kanumba mmeact movie moja inatwa Pay back wewe yusufu na monalisa na wengineo kupitia kampuni ya pili pili . Ile movie ni nzuri sana sana kwanza mmeact vizuri mno na walioedit wameipanga vizuri sana halafu inalocation nyingi. Utengenezaji wa vile ni mfano mzuri pia wa kuigwa.

Kanumba nimeona offside mmeact vizuri nzuri sana. pongezi kubwa mnastahiri. movie ambazo mnakutana wenyewe masuper star wa film zinakuwa nzuri sana hakuna hata anaeboa.

Kila la heri likizo njema na Safari njema ukirudi nyumbani.

Anonymous said...

Hi, Kanumba nimefurahi sana ulivyo sema kuhusu kucheza filamu kuwa eti wacheza filamu hucheza mara moja kwa mwaka unajua Kanumba watangazaji wa clouds wanajifanya wanajua mambo kumbe niwashamba kuliko na hasa zamaradi na dina hujifanya wazungu mara eti kucheza filamu na mwanamke huyohuyo watu hawawezi kujua ni filamu gani? hou ni uongo walimtolea mfano Sharukhani na kajori wakati hao watu wanafilamu zaidi ya Tano wakicheza kama mtu na mpenzi wake kazabuti kaka kwani wewe na Ray mko juu M.mungu atazidi kuwajaalia achana nao.

Anonymous said...

Kanumba umepiga jiwe gizani atakae sema yalaaa ujue limempiga nahasa TV clouds muhusika Zamaradi hujifanya anajua movie na kuwachambua sasa lazima ajipanguze. uko juu kaka.

Anonymous said...

zamaradi anafanya kazi yake na wala hakosei chochote, acheni ulimbukeni wa mawazo na kumzidishia ujinga wa mawazo huyo kanumba, asikosolewe yeye nani, hata aende ulaya haitazuia watu kumkosoa, na huo ushamba punguzeni, kwenda America ndio nini, kama anafanya tofauti asiambiwe, acheni ulimbukeni. wabongo bwana.

Anonymous said...

piga picha tena na kinyago halafu ujifanye umepewa tuzo.. tehe tehe tehe... kanumba the great, punguza ushinyanga kidogo kaka.. ni step nzuri ulofikia lakini kwa wanaojua wanajua, bado una ushamba wa mawazo kidogo.. AMKA!!!!!!we ni mkali ila una ulimbukeni ndugu tena ulimbukeni mkubwa sana.

Anonymous said...

Mi nafkiri kwa style hiyo hata mtembee dunia nzima bado ni bure sababu hamtaki kujifunza, hamna exposure especially kama mnaenda ulaya ili kukomoa watu na sio kujifunza, hao watoa point wote sidhani kama wanafkiria mbali, mnamuonea bure huyo zamaradi, hivi mnajua media zinafanyaje kazi huko nje mnakosema mnaenda kujifunza, critisism is just a normal thing ili kumjenga mtu, huyo zamaradi amchukie kanumba wa nini jamani, anakosoa wangapi, kwani ni kanumba peke yake, huyo kanumba asikosolewe yeye nani.. Brother open your eyes na jaribu kuishi dunia ya sasa,huna cha kufanya watu wakuchukie.

Anonymous said...

hata kama zamaradi anafanya kazi yake il kazidi kujifanya anajua katika kazi ambayo hata hajasomea wala hana experience nayo tupeni sehemu ya maoni muone tutakavyomchambua huyo zamaradi na clouds yao

Anonymous said...

palipo na ukweli tuambiana na palipo na makosa tuambiane pia zamaradi anafanya kazi yake ila ana makosa na mapungufu mengi na kanumba kwa hili tumpe hongera zake kwani kuna waigizaji wangapi wanashindwa hata kufika kenya kuona movie industry ila yeye kashaenda nijeria,uingereza,usa ,south africa kwa ajili ya movie hamuoni ili ni la kujivunia kwa wasanii wetu big up kanumba

Anonymous said...

big up the greattttttttt

Anonymous said...

niceeeeeee tour

Anonymous said...

MWENYE ROHO MBAYA NAYEYE HAENDE HUKO TUMUONE TUSIISHIE ETI HATA ATEMBEE DUNIA NZIMA HATOFIKA MBALI UNATAKA AFIKE MBINGUNI?KAOMBE NA WEWE VISA UONE KAMA UTAPATA NDIO UTAJUA SIO KITU KIDOGO ACHA ROHO MBAYA WEWE

Anonymous said...

UMEJITAIDI SANA NDUGU YANGU TOKA ENZI ZILE KAOLE KATIKA DALADALA HADO LEO HOLLYWOOD SAFIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

Anonymous said...

Hongera sana kanumba, kwa kutuhabarisha nasitumejifunza mengi kupitia blog yako, big up!

Anonymous said...

Swali ulitakiw aulize ni howlong does it take before a movie comes out?. Ktk nchi ilozidi kutoa movie kila month tz imezidi, kaeni chini pangeni story, fanyeni movie iwe interesting sio mtu anangalia movie kipengele cha kwanza kashajua inaishia vipi. Kaeni chini mtafakari napia mjue. Napia alokwambia hivo huyo mtu mungo, actor ukiwa umesaniwa kwenye movie flani kma movie zote tatu ziwe zinashutiwa same year basi huwezi unambiwa uchague moja kwani time conflict kwahiyo ulomuliza kakuongopea.