Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Jan 29, 2011

MWISHO NIMEMALIZIA ZIARA YANGU KWA HAPA LOS ANGELES MAENEO YA UKUMBI WA STAPLES CENTER.

Kwa kumalizia ziara yangu ya kutembelea hollywood nimetembelea ule ukumbi maarufu wa michezo mbalimbali hasahasa basket ball kutizama mchezo wa HOCKY unaopendwa sana hapa USA,Kikubwa kilichonifanya nije hapa si kwa kupenda huu mchezo wa HOCKY ila ni umaarufu wa huu uwanja,kwa kifupi uwanja huu ndio alikuwa akifanyia mazoezi MICHAEL JACKSON kwa ajili ya show yake ya THIS IS IT,lakini pia humu ndipo mwili wake ulipoagwa mara baada ya kifo chake,Pia ukumbi huu ndio timu kubwa kama Lakers na LA KINGS hucheza mechi zake..nami nikaona ni vyema nije niione jinsi ulivyo unaitwa STAPLES CENTER. Nikiingia

Pengine unaweza shangaa kwanini napiga picha na sanamu hili la mcheza basket ball maarufu na mkongwe mwenye heshima kubwa katika mchezo huu,pengine katika maisha yangu naweza nisije onana nae na kupiga nae picha ila alininivutia kwa umahiri wake katika mchezo huo,lakini zaidi ni pale alipojigundua kuwa ni muathirika wa ugonjwa wa UKIMWI akiwa ni star mkubwa duniani aliamua kujitangaza hadharani jamii imjue kama kaathirika,ujasiri huu ndio unaonifanya nipige picha katika sanamu lake hili kama mtu yoyote yule anavyoweza kufanya,mara baada ya kujitangaza jamii ilishtuka kwa taarifa hizi lakini makampuni mengi yalijitokeza kumpa misaada na akastaafu mchezo huu akiwa kaweka rekodi hii,hadi leo bado anadunda akiwa na afya njema,aliwai pia kushiriki katika video mojawapo ya Michael Jackson,,huyu ni MAGIC JOHNSON.

Uwanjani

Monitor ya juu katikati ya kiwanja

Huu ndio uwanja wa Staples center

Mr.Jingo na mimi uwanjani

kwa juu waonekana hivi

Burudani mbalimbali

wasichana hao kazi yao ni kusafisha uwanja kwa kuondoa barafu zilizoyeyuka uwanjani maana mchezo huu unachezwa katika kiwanja chenye barafu huku wachezaji wakitumia viatu vya matairi kukimbia.

Tizama uwanja ulivyo hakika kodi za wananchi zinafanya kazi

Nikifatilia mchezo huo

Huu ndio mchezo wenyewe wa Hocky

Watu wakitazama monitor ya juu pale inaporudia goli lililofungwa....

8 comments:

Anonymous said...

kaka hongera sana.....

Anonymous said...

HAKIKA UNAONESHA NJIA KAKA MUNGU AKUSAIDIE NI VIZURI KUJIFUNZA

Anonymous said...

Am proud of u steven huwa unakutana na mitihani katika jitihada zako lakini masikini huwa hukatai tamaa hongera darling

Anonymous said...

WE LOVE U KANUMBAAAAAAAAAAAAAAA

Anonymous said...

Tunakuombea bro kaza buti, Mungu si mwanadamu hata aseme uongo, atabariki kazi ya mikono yako, na ndivyo ilivyo.

Anonymous said...

yaani kanumba huwa unashangaa ukienda nje ya tz kama hujawahi safiri kila sehemu unataka upige picha ngoja nikuletee na zangu uziweke uwone bonge la mipicha ya kufa m2mingine nipo na viongozi nani watu kibao utaweka wewe

Anonymous said...

Am proud of you! keep it up my dear, we love u!

Anonymous said...

Am proud of you! keep it up my dear, we love u!