Nikiwa nje ya ofisi ya OXFAM SHINYANGA,nikimsubiria dereva aje tayari kwa kuelekea wilaya ya Kishapu.
Nimefika kishapu nikiwa na dada Mwanahamisi(Mishy) toka OXFAM akinisaidia mambo kadhaa hapo,tulianza kwa kuongea na baadhi ya wakazi wa hapo kuhusu tatizo la chakula.
Hakuna mvua kwa mda sasa hivyo hakuna chakula kabisa mlo ni mmoja kwa siku,serikali ilitoa debe 2 kwa kila kaya lakini familia ni kubwa wapo walio 10 wengine 15 hivyo kwa msaada huo bado hautoshi,mifugo inakwisha kwa ukame.
Mzee akiomba watengenezewe mabwawa ya kuhifadhi maji alafu wenyewe watatengeneza mifereji ili ktk kipindi kigumu kama hiki wasiwe wanakosa chakula,
Mzee akijibu swali langu nililomuuliza kwanini wasilime mazao yanayostahimili ukame?akasema hata kama yanastahimili ukame lakini bado yanahitaji maji japo kidogo ili yastawi kitu ambacho hakipo hapo
Umri wa huyu mzee na mwonekano wake ni vitu viwili tofauti,njaa imewakumba,ana familia ya watu 11,asubuhi wanakoroga uji lita 20 hawana sukari wanaweka ubuyu au ukwaju wanakunywa,jioni saa moja ndio wanakula mlo wa mwisho siku imepita.
Huyu mama ana watoto 8 wa kwanza ana miaka 15 yuko darasa la saba wa nane ndio huyo aliyembeba,kutokana na njaa mme wake alimkimbia miaka 2 iliyopita akidai anakwenda kutafuta hadi leo,huyu mama hana kazi yoyote na familia ni kubwa,kuna siku inabidi watoto wasiende shule maana jana yake hawakula chochote mpaka akipata chakula wanakula ndio wanaenda shule hata kwa kuchelewa,shule za huku hakuna mabasi kama mjini ni kutembea sawasawa..
Nikijaribu kuongea nao kwa kisukuma kidogo maana ndio kabila langu....
Nikirekodi video ya mambo ninayoyaona huku,video inayotakiwa kusambazwa duniani kote nikihimiza mfumo wa chakula wenye usawa na haki uwe sawa kwa kila mtu duniani kote.
Ebu tizama ardhi ilivyokauka na huku ndiko waliko wakulima,unafikiri bei ya chakula itakuaje mjini,suala zima kilimo limewekwa nyuma vijana wengi wenye nguvu wanakuja mjini na kuwaacha wazee kijijini wasio na uwezo wa kulima sehemu kubwa,
Popote niendapo duniani watoto ndio huwa mashabiki wangu namba moja nami nawapenda sana maana huwa hawana chuki,majungu,roho ya kwanini,majivuno,matusi,kejeli na dharau huwa kama malaika wanionapo furaha iliyopo moyoni ndio hiyo huionesha usoni bila ya kificho wala kujishtukia nami ucheza nao na kufurai nao hujihisi niko na malaika,ndio maana niliamua kuwa nawatengenezea movie zao ili wajione tuko pamoja mfano THIS IS IT,na UNCLE JJ
10 comments:
thats true steven,watoto wanaweza kukutoa kwenye huzuni na kukufanya usmile hawawezi kukuumiza.it seems udogoni uliteseka some how ee!pole,
we love you so much
thats true steven watoto wanaweza kukutoa kwenye huzuni ukatabasamu hivyo lazima tumake the world a better place for them.Steven,it seems ume experience matatizo sana in your childhood!pole sana
we love you sana
we love you
we love u
Nakupa hongera kaka kwa kujituma kaza buti hivyo ndiyo inavyotakiwa na Mungu akubariki
hi,kwanza kabisa nakpa pongezi saana kaka yangu kanumba huwa nakuombea Mungu sikuzote akuzidishie baraka tele ktk shughuli zako zakila siku zakimaendeleo pia usijali maneno ya watu wasio na busara wala shukrani kila siku wao nikulaumu tuu na hawaoni unayoyatenda ila mwenyenzi Mungu anaona yoote.na anaujua moyo wako kwa dhati so mwanadamu asikukwamishe wala kukutisha,songambele kaka,mimi napenda saana kazi zako na una upendo kwa jamii,ubarikiwe sana ktk jina la yesu pokea baraka zote ziambatane nawepopote uendapo.amen.mimi dada yako niko ugaibhuni huku,
mungu awasaidie!!!! Amin
Ur forcing me to comment on ur blog, i luv watoto a lot, being a star halafu geting a chance kuwa na watoto wa aina hii means a lot 2u na kwao pia, ur adding value kwenye maisha yao hata usipowapa chochote, jst being around them and talking to them means a lot to them, u inspire them! GOD BLESS U DEAR, KEEP ON DOING THESE COMMUNITY WORKS,IT PAYS A LOT, not in monetary form but i tel u, IT ADDS VALUE IN UR LIFE
very very very nice Steven!! Nashukuru kwa kazi unayofanya na naomba Mungu wakazi wa hapo wapate msaada. Ubarikiwe.
hata mm umenifanya nitoe comment katika blog yako....ni vizuri sana mabvyo kwa sasa utakuwa na reality ya maisha ya mwananchi wa kawaida wa kijijini yaani unaishuhudia kwa uhalisi wake...hii ikusaidie pia katika kuandaaa movie ambazo zinalenga kuonyesha maisha ya namna hii na ambzo pia story zake tungependa sana kuziona na kuzisikia pia....maisha kama haya hayaonyeshwi au kama yanaonyeshwa ni kwa kiasi kidogo sana..watengeneza movie wengi wa kitanzania mnaamini kuwa mitengeneza movie yenye kuonyesha mazingira haya haiwezi kupata soko..hii si kweli kabisa tunataka kuona na kusikia pia story za namna hii kwani ndio asilimia zaidi ya 80 ya watanzania ndio wako katika maisha haya...nakupa pogezi kwa kazi yako na keep it going!!!
Post a Comment