Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Nov 1, 2010

WADAU WENGI WATABIRI SAWIA....HII NI MIMI NA SWAHIBA

Hivi juzi niliandika GUESS WHAT?nikatoa na picha za mimi na swahiba tukiwa na Irene Uwoya nikiitaji wadau mtabiri,na wengi wamepatia ni kweli kwa mda wa karibia miaka 2 mimi na swahiba hatujakutana katika filamu yoyote mpaka hii ya sasa ambayo ni moto wa kuotea mbali saaaaaaaaana ni KANUMBA VS RAY.Wadau tumeingia ulingoni hasa hasa kutokana na maoni ya mashabiki wetu wengi ambao kila mara wamekuwa wakiomba tukutane kama zamani nasi tumeamua kuweka mkakati wa kila baada ya mwaka mmoja tutakuwa tunakutana na swahiba katika filamu moja tu kama hii ya sasa,filamu yetu ya mwisho ilikuwa ni OPRAH ambayo tulimshirikisha Irene uwoya mwaka 2008 na ya sasa ni hivyo hivyo.hapa ni kampuni mbili za production zinazoshirikiana yaani RJ COMPANY NA KANUMBA THE GREAT FILMS.Jina la filamu nitawatajia siku ingine wadau.. The great na swahiba tukiwa tayari kwa kushoot

Katika movie hii tunae pia JB ambae kaongeza utamu katika movie

The great na JB on set,Toka nianze kuact sijawai kukutana na kaka yangu JB movie hii ndio ya kwanza kukutana mimi na yeye.Ni msanii ninayemkubari sana.

Swahiba na JB kazini

Swahiba akipitia script kwa uyakinifu

The big two kazini....hapo ni makamuzi ya hatari

mmmmh?

Katikati ya scene

The great kazini

Ebu fikiria hii scene itakuwa vipi hapa The great pale swahiba pale JB...hatariiii

19 comments:

Albert said...

Hapo sasa mtatuua wadau! Siwezi nikatabiri mzigo huu utakua vipi, ninachokijua tu ni kwamba utakua moto wa kuotea mbali. Aaah, JB, Kanumba, Ray, Irene, for the first time, kwenye mzigo mmoja??!?!??... Hii itavunja record Kaka!
Haya, tunaisubiriakwa hamu...
Albert
Western Australia.

Anonymous said...

INAONEKANA KANUMBA KACHEZA KA MSELA FULANI IVII ALAFU RAY NA JB WASHUA............TUNAINGOJEA KITAA

sheilla said...

jamani mnajitahidi hongereni saaaaaaaana!! sheilla

Anonymous said...

inaelekea itakuwa nzuri sana,hongereni kwa kazi zenu nzuri nawakubali.

Anonymous said...

ray mbona una endelea ku nenepa?

Anonymous said...

Ahahahahaaaa inaonyesha utakua bonge la tozi kwa baadhi ya picha nilizoziona.....am waitin huo utamu jamani....Kanumba haubahatishi and u know that

Zuu...

Anonymous said...

kwa muonekano wa hii picha,ume act kama bad boy

naima said...

iyo naona itakuwa kali ile mbaya,mtafunikaa we na swahiba wako ray.kila lakheri. from-Finland.

emu-three said...

Safi sana, hiyo itawavuta washabiki wote wa pande mbili na matoke ni mazuri!
Big up!

Anonymous said...

I c my brothers and i belive the movie is going to be hot.coz u two swahibas and uwoya in da house nocing is going to be disappointed am always put my trust in all of u guys.Aiso i do like pastor emma where is he?My big up to your uncle JJ movie every now & zen wen am watching za movie am ending lughing and appriciate your job you real the great in the industry.I do admire u with your job.

Anonymous said...

mhmm kwa kweli siipatii picha hii movie maana nahisi itakuwa gumzo zaidi ya zingine maana hao masuper star wanaoiigiza humu mhmmm balaa tupu na JB ninavyompenda jmn ananogeshaga sana filamu huyo kaka home wakiiona filamu ya JB yumo ndani hakuliki wala hakulaliki mpk iishe kwa vituko vyake tuaisubilia tu kwa hamu kaka angu.

marimar

Anonymous said...

i cant wait to watch this movie bt aunt ezekiel is missing.jb is too good namkubali sanaa.keep going.luv u all.

Anonymous said...

Nyie vijana sasa oeni maana muda unazidi kuondoka na nyie hatuwasikii mkitangaza nia vibaya namna hiyo visura mbona wengi..........Kizito!!

Anonymous said...

lakini huyu JB si aliseema kufanya kazi nje ya kampuni yake ni marufuku sasa hapa inakuaje?au kampuni yake ndio waandaji wa hio movie?au njaaa tu?

Mdau -Hollywood CA said...

Ila kitu kimoja bado ,kwenye bongo films ,sehemu nyingi ni za maongezi na ndani ya nyumba kwenye masofa..vile vile bado hamjaweza kuhusisha watu wengi .. sinema zima waigizaji wanaweza kuwa watatu tu ...vile vile its too much high class life ..sidhani kama ukiwa ndani ya nyumba umepumzika especially on sunday uwe umevaa suti kama koffi olmide on stage.

Anonymous said...

hello, naona mambo ni bam-bam,big up.

Anonymous said...

Ebwana mie nataka kuhuliza kwa rafiki yangu Ray!!ebwana mshikaji kila mala unakuwa na mashati ya kung'aa mchana usiku,au ndo design mpya make inawezekana mie ndo mshamba.

MARMO said...

Hongerini kwa ushirikiano wenu, kwani naamini mtatoa filamu nzuri ambayo itaonyesha uwezo wenu na naamini itakua imefanyiwa kazi nzuri, kuanzia maandalizi hadi kutoka kwake. Ushauri wangu kwa wasanii wote wa filamu ukiwa na wewe mwenyewe, kumekua na utitiri wa filamu kila mara na nyingi zake hazipati maandalizi ya kutosha kwa hiyo zinaingia sokoni na zinachuja mara moja.. sio movie ambayo inakua na maisha marefu kwenye soko la filamu, na hii inatokana na mapungufu mengi yanayokua kwenye filamu hizo. Ni bora ukatoa filamu moja kwa mwaka mmoja au baada ya miaka miwili au mitatu kuliko kutoa filamu mbili ambazo hazijafanyiwa maandalizi ya kutosha. Kinachotokea ni kwamba, msipokua mnatoa filamu zenye ubora soko lenu litakufa na hasa ukilinganisha na nchi nyingine ambazo zimepiga hatua. Swala sio tuu kuuza Tanzania ni kuuza nje ya Tanzania, na kukaba hilo soko pia. Ni wakati wa kutoa filamu bora na sio bora filamu. Na pia wazo la kushirikisha wadau mbali mbali kabla ya kutoa filamu ni swala la msingi, na wadau hao ni experts wa filamu, na bila kusahau wateja unaowategemea kununua filamu yako. Sio mbaya ukaingia gharama kubwa kutengeneza movie bora, italipa kwani haitatamba mwezi au miezi miwili bali itabaki kua ya muda mrefu, hata vizazi vyetu vitaikumbuka...nyie wote ni mashaidi kuna filamu za zamani kutoka kwa wenzentu za miaka ya 70, 80 na 90 ila bado zinapendwa, na hii inatokana na kuandaliwa kimakini na kwa ubora unaofaa.

Anonymous said...

uroho umetuzidi fanyeni mzigo huyu inaonekana ni moooto.