Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Nov 30, 2010

FILAMU YA UNCLE JJ YAINGIA MTAANI KWA KISHINDO YAVUNJA REKODI YA THIS IS IT

Wadau ile filamu yenu mlioisubiri kwa hamu ya UNCLE JJ niliyocheza na wanangu(watoto)iko madukani kote sasa,na mpaka sasa imevunja rekodi ya ile ya mwanzo ya THIS IS IT,Pata nakala yako original ktk dvd,vcd na vhs. Poster la UNCLE JJ

Nilitembelea duka moja kariakoo ambapo wamachinga walifurai kuniona na kuomba picha na mimi.

UNCLE JJ dukani

Hili ni duka mojawapo ambalo wamenihakikishia movie hii imevunja rekodi ya filamu bongo ikiwemo This is it maana duka hili tu copy 4000 za dvd na vcv 200 zimekwisha siku hii tu ya kwanza.Nawashukuruni sana mashabiki wangu bila ninyi hakuna Steve kanumba,nami ntazidi kuwakonga nyoyo maana nina kipaji toka moyoni.

3 comments:

Albert said...

Yaani hii ndo nilikua nasubiriya kwa hamu kaka, kila siku nilikua niko hewani nikisubiria kuona posta la Uncle JJ.
Hongera sana Bro mengi zaidi tutaongea kwenye simu.
Hongera sana...
Albert
Australia.

Anonymous said...

Kwani Uncle JJ ilikuwa haijatoka mbona mimi nimeiona siku nyingi au imekuwaje wajameni????????????????

Anonymous said...

Je, sisi wa huku ughaibuni tutaipata vipi hiyo movie jamani? Wiki iliyopita niliiagiza bongo nikaambiwa bado haijatoka, kumbe ndo imetoka sasa. Tufanyieni mpango na sisi wa huku ughaibuni tuwe tunazipata hizo movies kwani tunapenda kuziangalia pia.