Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Mar 18, 2010

KANUMBA THE GREAT FILM kazi ndio imepamba moto vijana tuko msituni tukipika mambo.

Aunty na The great katika moja ya scene za kifamilia zaidi,katika movie hii Aunty kaonesha mabadiliko makubwa sana tofauti na mwanzo,kiwango ni kikubwa zaidi ya mwanzo maana nimeshafanya nae kazi nyingi kama Fake smile,Village paster,Unfortunate love n.k.

Sio kweli jamani ni shooting tu...Aunty kaamua kuua.


Hapa ilikua ni baada ya kumaliza kusali kama ilivyo kawaida ya KANUMBA THE GREAT FILM Aunty akishauri ni vizuri sana kwa kila jambo tunalotaka kufanya kumuhusisha Mungu alisema kwakweli kila baada ya maombi huwa anajiskia kama Mungu ameweka uwezo wa ziada kwake hivyo kumfanya aigize zaidi ya kiwango cha kawaida.

The great nikiongoza sala nikiwa nimezama kiroho nikimkabithi Mungu sanaa yangu na kazi zangu nikiomba kibali kutoka katika kiti cha enzi cha Mungu baba.

Lusubiro Mwanguku ndie cameraman wangu nimeridhika na kiwango chake cha kazi baada ya kuona bidii yake alipokuwa SOPHIA RECORDS lakini pia nimewai kufanya nae kazi kadhaa GAME 1ST QUALITY na sasa ananishootia KANUMBA THE GREAT FILM.


Mara nyingi tunapomaliza kushoot scene iliyokua na vyakula(props)na vikabaki baada ya shooting huwa halali yetu kama unavyoona hapo mimi na Aunty tukishambulia.Kama director inabidi niangalie monitor vizuri kama inanipa quality ya picha ninayoitaka na setting za taa kama ziko sawa.

katikati ya scene tukiendelea
Aunty hataki utani mara kadhaa kabla ya kuanza kushoot huangalia upya script yake na kukagua kama maneno yake yako sawa na kama ana ushauri pia hutoa kwa vigezo hivi ndio hupatikana muigizaji bora.

Nice chande nae ni mmoja wa washiriki wa movie hii hivyo yuko location akichek kazi inavyokwenda hapa akijipoza kwa juice.

katika scene huu ndio muonekano wangukazi imepamba moto


Kama director lazima nihakikishe kabla ya kuanza wasanii wangu wanafanya rehasal na niridhike na kiwango ninachokitaka wacheze kwa mujibu wa story.

Mzee magari na Mama mjata wakionesha kiwango

Pamoja na kuwa muongozaji na producer lakini huwa natoa nafasi kwa wasanii wangu kuchangia maoni kama wanayo kama unavyomuona mama mjata akishauri kitu hali hii husaidia movie kuwa nzuri zaidi.

Mungu kwetu ni kimbilio la kweli na la nguvu kama mnavyoona nikiongoza maombi na wote wamefumba macho kwa unyenyekevu ili Mungu abariki na kututangulia kwa kila jambo tufanyalo hapo maana maadui ni wengi wengine twawajua wengine hatuwajui lakini katika ulimwengu wa roho twaweza kuwaona,kama unavyoona wengine tupo kazini ila wengine wako busy kukutengenezea scandal wakiamini kuwa eti shangwe za harusi zinaweza kubadili maji ya mchele kuwa maziwa.

Muonekano wangu location.

17 comments:

Anonymous said...

Aunt kamua kamua dada halafu paisha. Napenda sana ukijituma kama hivi. Mungu atakujalia tu.


disminder.

Anonymous said...

Aunt ezekiel bomba na hizo fake lashes mmh. mungu atamsaidia na yeye atafungua campuni yake,wanawake na wao wawe juu.

Suzie said...

Inaonekana ni itakuwa nzuri ila Kanumba kama unafanya movi Tz nafikiri ungeifanya mambo mengi KiTz maana kama hapo naona kama unavuta Cigar sasa hapa bongo tuna visport, embasi na kazalka huoni kama vitu kama hivyo ndio vinavyoonyesha movi zako nyingi ni za kuiga, try kuleta vitu vilivyozoeleka hapa bongo ili nikimuonyesha bibi yangu asianze kuuliza na hiyo fimbo mkononi anaipeleka mdomoni kwa nini

Ester Ulaya said...

Kila la heri katika hilo

Anonymous said...

kanumba ur the best...trust me and kitu nachokupendea ni kwamba hauchuji...i love that kiukweli,also god is fighting for u ndomana hata baraka zinakushukia kwa wingi...BUT am sorry kma ntakua naingilia mambo yako bt epuka skandals,find a girl alietulia na mwenye thamani yako..otherwise ur the BEST.VIC

sauda said...

siku zote huwa nakubali sana kazi za kanumba,japo kuna nyingine zinakuwa zinakosa vitu fulani,ila kanumba unakipaji sana Mungu akubariki na watu wako ambao mnashirikiana katika kazi

sauda said...

siku zote huwa nakubali sana kazi za kanumba,japo kuna nyingine zinakuwa zinakosa vitu fulani,ila kanumba unakipaji sana Mungu akubariki na watu wako ambao mnashirikiana katika kazi

Anonymous said...

kanumba your the real Great in film production.Nikiona any new film huwa natazama kama sura yako ipo ili nitoe pesa ninunue.Dogo unatisha sana na endelea kumtanguliza Mungu hatakuacha kamwe coz ni kimbiliola wote.umenikamata masikio!.Mwambulupulu, Mbeya

Monica said...

Siosiri kaka unatisha! kwakweli unakonga mioyo yetu mwanawane mungu akubariki sana kaka upo juu kama nyota!

Anonymous said...

hongera sana kaka, najitahidi sana mtaa kukutetea kwa watu wasio jua hata kazi ugumu wake ukoje ila mmfekia hapo mlipo.. kaza buti kaka mtoe mo quality movies.. all the best.

Anonymous said...

mimi ni kati ya mashabiki zako ambao wanazimia na kazi zako!!!!ila kuna jambo lanishangaza,,,,,, mbona hamuigizi na coletha na ni msanii mnzuri, ana mvuto, na kipaji kikubwa ktk sanaa?????ss mashabiki wako tungependa kuwaona pamoja tena mtamech sana sababu wote ni wajuzi kuliko hao unaogizanao ss.mungu akupe moyo wa upendo...

Anonymous said...

kakawe noma ila tunapenda sana siku ukiwa na coletha kitika filamu zako itakua tamu niaje

Anonymous said...

kakawe noma ila tunapenda sana siku ukiwa na coletha kitika filamu zako itakua tamu niaje

PANDEHIZI said...

BIG UP SANA MTU MZIMA

phiniasgeita@blogspot.com said...

Ukweli mkubwa wangu unafanya kazi nzuri ila ujue uster ni mzigo utapata kashfa sifa ila we kaza mwendo tupate vitu vizuri cheza kama hollywood Peter wa Mkoa mpya Geita

Tina wa ukweli said...

kaka kanumba, mdogo wangu mi napenda sana unavyokuwa na ushirkianomzuri na wasanii wengine. Inanipa raha nakufanya nikpende zaidi. Big up bro na Mungu atakubaliki zaidi kwani roho ya kwanini haijengi?

Anonymous said...

hakuna mtu asiyejua kuwa kanumba ndiye maji ktk tasnia ya flm tz so km ucpo kunya utaya oga ucpo yaoga uta nawa! ila kaka najua hunifaham but nina shida sana na ww co plz,plz naomba unitafute tafadhali, mm nimoja kt ya wanaohitaj mabadiliko ktk tasnia ya film tanzania my number ;0654507049.