Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Mar 22, 2010

SWAHIBA WANGU THE GREATEST ATEMBELEA LOCATION KWANGU LEO KUONA KAZI INAVYOKWENDA.

Mkurugenzi wa GRM PRODUCTION Ndg GABRIEL MAKUBA nae alikuepo kusaidia mambo kadha wa kadha katika kuhakikisha movie yangu inakuwa na ubora wa kisasa.kama unavyoona hapo picha yangu ukutani ni moja ya kazi alizonisaidia upesi katika scene za ofisini kwangu na kuhakikisha kunakuwa na picha ukutani ili kujenga uhalisia.

Mara baada ya swahiba kufika nilimkabithi kiti cha u director ili anidirectie scene mojawapo hapo nae alikubali kufanya hivyo,hii ni kampeni tuliyoianzisha ya kutembeleana location ili kutiana moyo na kuifanya tasnia ya filamu kusonga mbele kwa ubora na kwa umoja hasahasa tukifahamu kuwa"There is nothing can't be done if we raise our voice as one"


Swahiba akichukua picha za matukio kwa ajili ya blog yake ya www.raythegreatest.blogspot.com

Swahiba akiwa makini katika kudirect scene niliyompa ambayo nilikuwa nikicheza mimi.

Lusubiro Mwanguku akiwa makini na camera

Swahiba alidirect kwa moyo wote na kwa furaha hakujali kama movie ni yangu bali alifanya kama ni yake au ya RJ COMPANY nilijisikia furaha sana moyoni nikakumbuka enzi za filamu zetu za mwanzo za Game 1st quality Tz Ltd kama Johari 1&2,Sikitiko langu,na Dangerous desire.

Baada ya kumaliza scene hiyo tulipata picha ya pamoja

Mara nyingi tukikutana huwa ni lazima vicheko vitawale na utani wa hapa na pale maana tumetoka mbali jamani ukweli tunaujua wenyewe.

MAYA production manager wangu, make up artist wangu na continuity manager wangu huwa makini sana katika kazi yake chini ya kampuni yake ya vipodozi ya MAYA ENTERTAINMENT kama mnavyomuona hapo akiandika kila shot inayopigwa katika scene na miendelezo yake hii humsaidia editor wakati wa kuhariri movie kazi kuwa nyepesi maana hutambua ni shot zipi zitumike na zipi ziliharibika kwa kutumia hilo daftali analoandika Maya.

Kaka yangu kiumri na kaka yangu kiroho(JB) nae alikuepo pamoja na swahiba kuona jinsi The great ninavyosukuma gurudumu la filamu Africa na kuendeleza kampeni yetu ya kutembeleana location,jamani ukiujua ugumu wa kazi hii lazima utamtia moyo mwenzako pale alipokata tamaa,utamkosoa kwa njia ya amani ili kujenga na si kuponda au kutukana kazi yake na kutukuza za nje,utamshika mkono na kumwinua pale alipojikwaa ili asonge mbele na si kumkanyaga tena ili adidimie,utampa pongezi zinazomstahili pale alipofanya vizuri ili kumpa tumaini la kesho lakini haya yote hayawezekani kama hatuna upendo wa dhati kati yetu.Mungu atusaidie sana ili jamii yetu tupendane kwa dhati na kuwa wazalendo katika kazi za wasanii wetu wa Tanzania maana ni "Ni heri uzee wa simba kuliko ujana wa fisi"

2 comments:

Anonymous said...

Kanumba uko very childish, period. Grow up

Anonymous said...

UPO JUU KANUMBA, MUOMBE MUNGU AZIDI KUKUFUNGULIA, NA PIA AKUPE REHEMA ZAKE UWEZE KUA NA HEKIMA KATIKA ULICHOKIPATA IKIWA NI PAMOJA NA MAISHA YAKO YA NDOA KUA SALAMA, UMPATE WA KWELI KUTOKA KWA MUNGU,AMBAYE BILA SHAKA ATAKUA AMETENGENEZWA KWA AJILI YAKO HIVYO INAKUPASA UOMBE HILO MUNGU AJIFUNUE KWAKO AKUONYESHE, MAANA NI KWA NEEMA KUJUA HILO,
mUNGU AKUBARIKI NA AKUKUMBATIE!

DADA- FROM TANGA